MSICHANA aliyewahi kupigwa na msanii wa Hip Hop
Bongo, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’, Mwanaisha Sued ‘Aisha’ ametimkia
nchini Afrika Kusini kuishi kwa muda.
Paparazi wetu alitia timu nyumbani kwa binti huyo Ilala-Bungoni,
jijini Dar ili kujua maendeleo yake ambapo mdogo wa Asha ambaye hakutaka
jina lake lichorwe gazetini, alijibu kwa kifupi:
“Aisha hayupo amekwenda Sauzi kwa muda, kuhusu alichokifuata mimi sijui. Ila hajambo na anaendelea vizuri.”
Aprili mwaka huu, Chid Benz alishtakiwa katika kituo cha Polisi cha
Pangani, Ilala kwa kosa la kumshambulia Aisha ambaye aliwahi kuwa mpenzi
wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment