DEVOTHA ANAUKUBALI KWA MOYO MMOJA UTABIRI WA VIFO VYA WASANII

MSANII wa filamu Bongo, Devotha Mbaga ambaye ni Katibu wa Klabu ya Bongo Movie Unity, amesema anayaamini maneno ya watabiri kwa kuwa wanayoongea mara nyingi huwa yanatimia.
Msanii wa filamu Bongo, Devotha Mbaga
Akipiga stori na paparazi wetu baada ya mtabiri mashuhuri, Hassan Yahya Husein kutabiri vifo vya mfululizo vya wasanii ambavyo kweli vimetokea, Devotha alisema ameamini utabiri huo na kuzidi kujikita katika ibada.
“Kufa kila mtu wakati wake utapowadia atakufa kutokana na mipango ya Mungu, isipokuwa maneno ya watabiri hatuna budi kuyaamini,” alisema Devotha.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger