Mara baada ya mauzo na kununua mahitaji,wanawake na watoto
hulazimika kurudi nyumbani huku wanaume wakibaki wakistarehe ,huzitumia
siku ,ni nadra mwanaume kuwahi kurudi nyumbani .
Mei 19, Rhoda Nyangi Mtatiro (24) mkazi wa Kitongoji cha Kenyana
kijiji cha Masangura kata ya Ring’wani wilayani Serengeti, licha ya
ujauzito wa miezi sita alionao alikubali kuongozana na mumewe Wang’enyi
Sabai(30) kutoka kijijini kwao hadi Rung’abure umbali wa kilometa zaidi
ya 15 kwa mguu.
Huku wakiswaga kondoo wanne walifanikiwa kufika mnadani na kuwauza
wakajipatia fedha za mahitaji hakujua kuwa kuna balaa lingemkuta
siku hiyo, pamoja na kuswaga na kutembea umbali mrefu na ujauzito wake
hakuambulia kitu zaidi ya kipigo ambacho leo hajui hatima ya maisha
yake.
“Nilizunguka kutafuta nguo za mtoto, wakati huo mume wangu alikuwa nyumbani kwetu anamsalimia mama mkwe…. Saa 11:30 jioni nilifika nyumbani na kuwaambiwa ameishaondoka kurudi kijijini kwetu….nilishindwa kuondoka pekee yangu kwa muda huo na hali niliyonayo nikalala kwetu, ikawa mwanzo wa matatizo,”anasema.
Anasema alilazimika kutoka saa 12 alfajiri na kufika kwake saa tano asubuhi akiwa amechoka ,na kwenda kumsalimia mume wake dukani, hata hivyo alivyopokewa akahisi atapata adhabu kwa kuwa mume wake hana namna nyingine ya kuwasilisha hisia zake zaidi ya kutembeza kipigo, akaamua kuaga na kurejea nyumbani.
“Nilishangaa kuona mume wangu akifunga duka huku akiwa ameshikilia panga na kamba ananifuata …mita kadhaa akanifikia na kuniamru nisimame, eneo lenyewe limejaa vichaka….niliingiwa na hofu, ghafla akauliza nilikolala…kwa kujiamini nikamwambia nililala nyumbani kwetu baada ya kuogopa kutembea pekee yangu jioni,” anasema na kuongeza:
“Akasema ameambiwa nilikuwa na mwanaume gesti….nilimtaka anielewe kuwa nililala kwetu baada ya kuniacha…na ujauzito huo ninawezaje kwenda na mwanaume gesti….ikawa kama amechokozwa maana aliniamuru ninyanyue mikono juu na kuanza kunishambulia kwa mateke tumboni, kama vile haitoshi akaanza kunikata miguu kwa panga ili niseme kuwa nilikuwa na mwanaume gesti,” anasema kwa masikitiko.
Afungwa kwenye kiti
Pamoja na maumivu ya kupigwa tumboni na kukatwa miguu, alifungwa
kwenye kiti na kuendelea kuadhibiwa mbele ya mama mkwe wake Rhobi Sabai
na mke Mwenzake Rhobi Kibina(20), hadi akapoteza fahamu, hata hivyo
alijikuta amefungiwa ndani ya nyumba na kuambiwa kuwa aliokolewa na
jilani yao Moya Marwa.
No comments:
Post a Comment