Angelina Jolie ni mmoja wa wanaharakati maarufu wanaopinga dhuluma za kingono ikiwemo ubakaji
Viongozi wa kimataifa wanakutana jijini London kwa wiki nzima, kwa
kongamano la kumaliza dhulma za kimapenzi katika mataifa yanayokabiliwa
na mizozo.
Mkutano huo, wa siku nne umeandaliwa na Waziri wa masuala ya nchi za
kigeni wa Uingereza, William Hague na muigizaji maarufu na mjumbe maalum
wa Umoja wa mataifa, Angelina Jolie.
Kongamano hilo linajiri huku mataifa kadhaa barani Afrika yakikabiliwa
na changamoto ya kumaliza ubakaji unaotumiwa kama silaha ya kivita.
Ni mwanzo wa kuidhinishwa kampeni ya miaka miwili kutoa uhamasisho
kuhusu kutumiwa kwa ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi kama silaha
wakati wa vita.
Waandalizi wa kongamano hilo wanasema wanataka huu uwe wakati ambapo
ulimwengu utazinduka na kutangaza kwamba unyanyasaji wa kimapenzi sio
jambo lisiloweza kuepukika wakati wa vita.
Ujumbe

ni ubakaji sio jambo lisiloweza kuepukika wakati wa vita.
Tangu William Hague na Angelina Jolie wazinduwe kampeni hiyo, mataifa mia moja na arobaini na nane yameidhinisha azimio la uwajibikaji wa kumaliza unyanyasaji huo wa kimapenzi katika mizozo.

Tangu William Hague na Angelina Jolie wazinduwe kampeni hiyo, mataifa mia moja na arobaini na nane yameidhinisha azimio la uwajibikaji wa kumaliza unyanyasaji huo wa kimapenzi katika mizozo.
Lakini lengo sasa ni kuchukua hatua madhubuti, kuendeleza uchunguzi na kuripotiwa kwa visa hivyo vya unyanyasaji wa kimapenzi.
Pia katika kutoa usaidizi zaidi kwa waathiriwa na kuhakikisha kuwa usawa
wa kijinsia unahimizwa katika operesheni za siku zijazo za kulinda
amani.
Kiwango cha jukumu hilo ni kikubwa: katika miaka ya tisaini, vita vya
Bosnia vilisababisha kuwepo takriban waathiriwa elfu hamsini wa
unyanyasaji wa kimapenzi.
Takriban miongo miwili tangu vita hivyo vimalizike, ni wahalifu wapatao 60 pekee walioshtakiwa 

No comments:
Post a Comment