Ommy
amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa yeye na msichana huyo
waliweza kukaa kwa muda wa mwaka mmoja wakichati bila kuonana.
“Social
network zilisaidia kutuunganisha lakini matokeo yake mpaka tukaja
kuonana. Mpaka nikaja kwenye tour tukaonana, si unajua kuna zile mzee
unashangaa ma Instagram mtoto ka like picha kama tisini hivi, halafu
ukichekecha unaona mbona kama umechorwaee ,bahati nzuri ilipoanzishwa
instamessage kwahiyo kama unajiiba hivi. Ni Mtanzania, mpaka kuonana
ilichukua kama mwaka, tumechat tumechat mpaka ikafikia time, sina haraka
kwanini niwe na haraka, kufahamiana kunakuja automatically,” alisema.
“Unajua
mambo ya mapenzi Mungu mwenyewe ndio anajua, pengine wengine anaweza
wewe ukawa muuza mkaa demu akaja kununua mkaa. Lakini lile kopo
unavyolishika kimachejo wakati wa kupima yeye anapenda ule upimaji wako,
kwahiyo kuna kitu kama hivyo haijalisha mnakutana wapi, ikiwa tu
mmewekea mipaka yenu, masharti hivi na hivi maisha yenu yanaenda.”


No comments:
Post a Comment