RAISI JK ATUMIA DAKIKA 15 KUMFAGILIA DIAMOND

Rais Jakaya Kikwete alianza kwa kusema: “Watanzania hawapaswi kumbeza Diamond kwani pamoja na kukosa tuzo ya MTV lakini kuna juhudi kubwa alionyesha kwa kufanya shoo kubwa ya kwanza na ya kimataifa ambayo niliishuhudia mwenyewe na niliona watu walifurahia sana,”
Rais Jakaya Kikwete akimpa mkono wa pongezi Msanii mkali katika miondoko ya Bongo Fleva, Abdul Nassib, Diamond kwa hatua aliyofikia.
 “Diamond alilitangaza taifa letu kupitia shoo hiyo na muziki wetu wa Tanzania, hivyo hatupaswi kuwa mbali na wasanii wetu kwani natambua wazi Diamond bado yuko kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za BET ambazo ni tuzo kubwa sana nchini Marekani na naweza kusema kuwa hata kutambuliwa kwake kuwepo kwenye tuzo hizo nalo ni jambo la kujivunia kwani uwepo wake ni njia moja ya kulitangaza Taifa letu hata kama hatabahatika tena kuchukua tuzo hizo,”
Diamond (kushoto) akiwa na mkali mwingine wa muziki kutoka Nigeria, maarufu kwa jina la Davido (aliye mbele pichani).
“Najaribu kuwatia sana moyo na kumwambia Diamond kuwa awe na uvumilivu kwani nimeshaanza kuonyesha njia ya kumsaidia maana juzijuzi nilimkuta Marekani na nilimkutanisha na mdau mkubwa sana wa muziki duniani ambaye ndiye alimtoa Jay z, Usher Raymond  na wasanii wengine wakubwa na nilimuomba amsaidie kumwelekeza namna anavyoweza kukua kwenye ulimwengu wa muziki”,
“Nimeshaongea na mmiliki wa kituo cha televisheni ya E ambayo ni kubwa sana Duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha naukwamua muziki wetu, hivyo wanatarajia kuja Tanzania hivi karibuni akiwa ameambatana na Usher Raymond na wadau wengine ambao watakuja kukutana na kina Diamond na wasanii wa filamu ili wawape mbinu za kukuza sanaa yetu,” alisema Rais Kikwete.
Diamond akiwa na Mpenzi wake Wema Sepetu.
Diamond alianza kubezwa na baadhi ya mashabiki na wasanii wenzake siku chache baada ya kukosa tuzo na wengine walifanya hivyo siku ya uzinduzi wa Wimbo wa Tulinde Utanzania ambapo walimtania kwamba hana uwezo wa kuchukua tuzo hizo hivyo hata kwenye tuzo za BET asihangaike kwani hatapata chochote.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger