MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ameibuka na ubunifu mpya
wa sabuni ya kuogea inayokwenda kwa jina la Mo hiyo ikiwa ni baada ya
kutesa na bidhaa ya ndala.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Jokate alisema uzinduzi wa
sabuni hiyo unatarajiwa kufanyika leo Jumatano, Juni 18, mwaka huu
ambapo yeye na timu yake watatembea kwa miguu kutokea mjini (Posta)
kuelekea Mbagala huku wakigawa zawadi kwa akina mama.
“Nashukuru nimeweza kubuni tena bidhaa nyingine, nataka kuwaambia
wasichana wenzangu, wasilale. Tukitaka tunaweza kufanya makubwa.
Nawashauri wapenzi wangu wakae barabarani kunisubiria nitapita na kundi
langu la Kidoti ili niwapatie zawadi,” alisema Jokate.
Jokate amekuwa akibuni mitindo mbalimbali kama nguo, nywele na ndala lakini pia ni mwigizaji wa sinema za Kibongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment