skip to main |
skip to sidebar
SAJENTI AFUNGUKIA MANENO MAZIYO CHAZ BABA, YASOME HAPA
BAADA ya mkali wa Bongo Dansi kutoka Bendi ya
Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ kudai ana mpango wa kumchukua
mwanaye ili akaishi naye, hatimaye mzazi mwenzake, Husna Idd ‘Sajenti’,
amesema hawezi kumtoa mwanaye.
Mkali wa Bongo Dansi kutoka Bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ akiwa kwenye ofisi za Global Publishers.
Akistorisha na paparazi wa kona hii, Sajenti alisema: “Mimi siwezi
kumpa Chaz Baba mtoto wangu kwa sababu tangu akiwa mchanga namlea
mwenyewe.
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo Husna Idd ‘Sajenti’,
“Isitoshe mimi nimelelewa na mama yangu aliyenizaa, kwa nini nimtoe
mwanangu kwa mama ambaye hajamzaa? Nasema nitamlea mwenyewe, hata nikifa
ataendelea kulelewa na dada yangu, siyo mke wa Chaz.”
No comments:
Post a Comment