Showing posts with label CHAZ BABA. Show all posts
Showing posts with label CHAZ BABA. Show all posts

CHAZ BABA UKIENDEKEZA KUMPIGA MKEO, JELA INAKUHUSU

Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.
KWAKO jembe, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’. Mwalimu wao kwenye muziki wa dansi Bongo. Uwezo wako nautambua, nimekuwa shabiki wako kwa muda mrefu kidogo.Ni matumaini yangu uko poa, unaendelea na mishe zako kama kawaida.
Mimi mzima, namshukuru Mungu maisha yanasonga. Jukumu langu la kuandika na kukosoa linaendelea na leo nimekukumbuka wewe.Dhumuni la kukumbuka leo kwanza ni kukukemea kwamba suala la kuthubutu kushika kitu kizito, kunyanyua mkono na kumtwanga mtu si jambo jema, halifai kuigwa hata kidogo.
Ndugu yangu, hivi kwanza unafikiria nini ukichukua kitu kizito na kumpiga nacho mwenzako?Mbona zipo njia nyingi za kufikisha ujumbe wako kwa mtu na akajua umekasirika, lakini si kumtwanga na kitu kizito au chenye ncha kali ambacho unajua fika kwamba utamsababishia maumivu makali mwilini.
Kwa kitendo ulichokifanya kwa mkeo hivi karibuni hakikuwa cha kiungwana. Ulimtwanga kiasi ambacho kwa macho ya kawaida tu, inaonesha aliumia sana.Sitaki kujua alikuudhi nini, lakini ustahimilivu unatakiwa katika maisha ya kila siku.
Hata iweje yule ni mkeo. Unajisikiaje kumuona akiwa na majeraha chungu nzima mwilini ambayo umesababisha wewe? Si sawa kabisa!Wewe ni kioo cha jamii, unategemea jamii itajifunza nini kupitia tukio kama lile ulilolifanya? Unavyotakiwa kujichunga wewe ni mara mia zaidi ya vile anavyojichunga mwenzangu na mimi kule Tandale Kwa Mtogole.
Jamii inawatazama mastaa kama kioo chao, wanaamini kwamba nyinyi ni watu wema. Wanaamini mnajua kujitoa, mna upendo na mna nguvu ya kukemea maovu kwenye jamii na watu wakabadilika.
Umeshindwa kustahimili hasira zako, ona sasa jamii nzima ilijua kwamba umemdunda mkeo kiasi cha kuwafanya hata wale mashabiki wanaokufuatilia waone kuwa hukumtendea haki mkeo.Kumpiga mtu siyo dawa ya kutibu tabia au tatizo lake.
Unaweza ukampa mtu adhabu nyingine ambayo kwa macho ya kawaida inaweza kuonekana ndogo lakini kumbe ni nzito na ikamfanya mtu aone aibu kwa kipindi kirefu kama si maisha yake yote.Kunyanyua mkono na kumpiga mtu ni tabia.
Ukiiendekeza unaweza kufika pabaya ambapo pengine hata hujawahi kutegemea kama ipo siku unaweza kufika. Hatupendi itokee lakini sheria zipo.Utakuja siku ujibiwe vibaya na mtu sehemu, ukachukua silaha na kumdunda kama ulivyofanya kwa mkeo, sheria ikachukua mkondo wake, jela itakuwa inakuhusu.Achana na desturi ya kupiga, tumia njia mbadala kumuadhibu mtu.
Kupiga hakusaidii. Kwa leo acha niishie hapo lakini ni matumaini yangu utabadilika na kuwa mtu safi kama macho ya wengi yanavyokuangalia. Ni hayo tu!
Read more >>

ROSE NDAUKA NA CHAZ BABA BIFU ZITO, SOMA ZAIDI HAPA

TIFU! Ni dhahiri kuwa sasa, staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka na Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ wapo kwenye bifu zito.Habari kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa, chanzo cha bifu hilo ni fedha, ambapo Rose alikodisha gari la Chaz Baba kwa ajili ya matumizi yake lakini akalirudisha likiwa limeharibika na kumuomba Chaz alitengeneze kisha angemlipa fedha zake, lakini hakufanya hivyo.
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka
“Alikodi gari kwa Chaz, lakini aliporudisha lilikuwa bovu, akamuomba Chaz alitengeze angemlipa, baada ya hapo akaingia mitini. Chaz alikasirika sana, maana hata Rose alipopigiwa simu alikuwa hapokei.
“Imefikia hatua Chaz ametoa kiapo kibaya, amesema hata akifa, maiti yake isizikwe mpaka Rose alipe fedha zake kwanza,” kilitiririka chanzo hicho.

Akizungumzia ishu hiyo, Chaz alisema, kitu alichokifanya Rose si kizuri na kamwe hawezi kumsamehe mpaka amlipe fedha zake.
Huyu hapa anafafanua zaidi: “Unajua Rose alikuja kwangu na kukodi gari yangu aina ya Toyota Noah, akarudisha likiwa halitamaniki kabisa, nilipomwuliza akasema walipata ajali, nikamtaka akalitengeneze, akasema hana pesa kwa hiyo nitengeneze atanilipa.
Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’
“Tangu siku hiyo sijaona simu yake wala meseji, hata nikimpigia hapokei. Nimeingia hasara ya kwenda kutengeneza kwa shilingi laki tano, pesa yangu inaniuma, nataka anilipe.
“Hata kama nikifa leo, maiti yangu isizikwe mpaka Rose alipe haki yangu kwanza. Akitangulia yeye utaratibu utakuwa hivyo sitokubali azikwe hadi ndugu zake wanilipe fedha zangu,” alisema Chaz Baba.
Baada ya kupata habari hiyo Risasi Jumamosi lilimhoji Rose kulikoni ameshindwa kulipa deni la watu hadi mdai anatoa kiapo kibaya kama kile, akaruka vikali.

“Ni kweli kabisa mimi nilikodi gari ya Chaz nikawa natembelea na ilivyokuja kuharibika nililitengeneza mimi na kwenda kumkabidhi lakini hakuridhika na namna lilivyotengenezwa  ndiyo maana anasema ananidai lakini mimi sijui hilo deni,” alisema Rose.
Read more >>

SAJENTI AFUNGUKIA MANENO MAZIYO CHAZ BABA, YASOME HAPA

BAADA ya mkali wa Bongo Dansi kutoka Bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ kudai ana mpango wa kumchukua mwanaye ili akaishi naye, hatimaye mzazi mwenzake, Husna Idd ‘Sajenti’,  amesema hawezi kumtoa mwanaye.
Mkali wa Bongo Dansi kutoka Bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ akiwa kwenye ofisi za Global Publishers.
Akistorisha na paparazi wa kona hii, Sajenti alisema: “Mimi siwezi kumpa Chaz Baba mtoto wangu kwa sababu tangu akiwa mchanga namlea mwenyewe.
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo Husna Idd ‘Sajenti’,
“Isitoshe mimi nimelelewa na mama yangu aliyenizaa, kwa nini nimtoe mwanangu kwa mama ambaye hajamzaa? Nasema nitamlea mwenyewe, hata nikifa ataendelea kulelewa na dada yangu, siyo mke wa Chaz.”
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger