skip to main |
skip to sidebar
SAKATA LA UBAKAJI WA MBASHA: MIKE, DUDE WAFUNGUKA
WAIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Michael Sangu ‘Mike
Sangu’ na Kulwa Kikumba ‘Dude’ wamelizungumzia tukio la mume wa mwimba
Injili, Flora Emmanuel Mbasha kubaka na kudai wanashindwa kumuelewa
aliyeshtaki.
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Wakizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, waigizaji hao walisema
wametatizika na binti huyo kushtaki polisi kama alibakwa kweli.
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Michael Sangu ‘Mike Sangu’ akipozi.
“Yaani ni utata mtupu juu ya hili tukio, sasa hatuelewi kama kabaka
kweli au la maana tuna wasiwasi kwa nini tukio hilo lirudie mara mbili
bila makubaliano?” walishadadia mjadala huo mastaa hao.
Shemeji
wa Emmanuel Mbasha aliyekuwa akiishi naye nyumbani kwake,
Tabata-Kimanga jijini Dar, ambaye anadai kubakwa na Emmanuel Mbasha.
Mbasha anadaiwa kumbaka shemejie aliyekuwa akiishi naye nyumbani
kwake, Tabata-Kimanga jijini Dar, mpaka sasa bado anasakwa na jeshi la
polisi ili kujibu tuhuma hizo.
No comments:
Post a Comment