skip to main |
skip to sidebar
WACHEZESHAJI KAMARI YA KOMBE LA DUNIA WAKIONA CHA MOTO
Polisi
wa Macau wanasema wamegundua magengi mawili ya kamari ambayo yamepokea
mamilioni ya dola katika kamari ya kubahatisha matokeo ya mechi za Kombe
la Dunia.
Maafisa wa polisi wamewakamata watu zaidi ya 20 kwenye hoteli katika mji huo wa kamari.
Watu hao wamekuwa wakipokea simu kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na mcheza kamari mmoja ametia dau la dola milioni-5.
Mwandishi
wa BBC mjini Hong Kong, jirani na Macau, anasema magengi hayo yakipata
dola mia-moja-milioni kila siku kwa wateja wanaobahatisha matokeo ya
Kombe la Dunia, na wateja wakiwasiliana nao kwa simu na kwenye internet.
Kati ya watu waliokamatwa 9 ni kutoka Malaysia, 4 kutoka Hong Kong na 13 kutoka Uchina bara.
No comments:
Post a Comment