Wasanii nyota wa filamu ‘Bongo Movie’ wakiongozwa na mwenyekiti wao
Steve Nyerere wamenusurika katika ajali mbaya ya gari iliyotokea maeneo
jirani na Chalinze wakiwa njiani kuelekea Dar wakitokea mjini Dodoma
walipoenda kuhudhuria Tamasha la Uzalendo pamoja na Uzinduzi wa video ya
wimbo wa miaka 50 wikiendi iliyopita.
Chanzo cha ajali hiyo
kimetajwa kuwa ni kupasuka kwa matairi mawili ya gari walilokuwa
wakisafiria aina ya Toyota Brevis lenye nambari za usajili T 200 CRY
hata hivyo Hakuna mtu aliyeripotiwa kufa wala kujeruhiwa. Vicent Kigosi
‘Ray’, Shamsa Ford, Irene Uwoya, Johari na Jaccob Steven ‘JB’ ni
miongoni mwa wasanii waliokuwepo eneo la tukio.
Maisha Matamu, Johari na Shamsa Ford katika pozi, baada ya kunusurika ajalini
No comments:
Post a Comment