ANGALIA JINSI MWIZI WA PIKIPIKI ALIVYOCHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA WANANCHI

Kijana anayedhaniwa kuwa ni mwizi akipigwa na wananchi wenye hasira kali
Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja amepigwa na kuumizwa na wananchi wenye hasira kali katika eneo la Msasani Bonde la mpunga jijini Dar es salaam baada ya kusadikika kuwa ni mwizi wa pikipiki.

Kijana akipakizwa kwenye pikipiki tayari kabisa kuelekea kituo cha polisi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kijana huyo alijaribu kuiba pikipiki iliyokuwa imepakiwa katika eneo la Msasani, jijini Dares salaam. Baada ya kushindwa kuiwasha pikipiki hiyo, alitokea mmiliki na kupiga mayowe ambapo watu walifurika na kuanza kumpiga.

Mwizi huyo alikimbilia katika Dispensari ya Bonde la mpunga kujificha lakini haikufua dafu kwani watu wenye hasira kali walizingira dispensari hiyo na kumtoa nje kwa lengo la kumpiga. Lakini baada ya muda kidogo walifika askari wa jeshi la Polisi na kumchukua hadi kituo cha polisi cha Oysterbay, jijini Dares saam ili sheria ifuate mkondo wake.



Wananchi wenye hasira wakimpiga kijana anayedhaniwa kuwa ni mwizi


Kijana anayedhaniwa kuwa ni mwizi

kijana huyo akiwa na majeraha mwilini kufuatia kupigwa na wananchi

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger