ILIBAKI kidogo mastaa wa sinema za Kibongo, Vincent
Kigosi ‘Ray’, na Salum Mchoma ‘Chiki’, wazichape baada ya kutokea mzozo
kati yao uliodumu kwa dakika tatu wakirushiana maneno.
Tifu hilo lilitokea wikiendi iliyopita, Lamada Hotel – Ilala, Dar
ambapo Chiki alimshukia Ray akidai kuwa (Ray) haungi mkono uongozi wa
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ ndiyo maana
alikacha sherehe yake hivi karibuni.
Maneno ya Chiki yalimchoma Ray ambaye alionekana dhahiri kupaniki
lakini akajibu mapigo: “Siwezi kuacha kazi location ili niwahi sherehe,
huo ndiyo utaratibu wangu, hata hapa (kwenye birthday ya Dk. Cheni)
nimekuja kwa sababu sina kazi yoyote inayoendelea.
“Siwezi na sina sababu ya kumpinga Steve Nyerere, sikwenda kwenye
shughuli yake kwa sababu nilikuwa narekodi... filamu ndiyo maisha yangu,
acha kuropoka wewe.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment