B , RICH SASA KUMUIGA STEVE NYERERE

Stori: Shakoor Jongo
NYADHIFA! Bongo Movies Icons, Jacob Steven ‘JB’ na Single Mtambalike ‘Rich’ wako mbioni kufuata nyayo za Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wakitaka kushika nyadhifa mbalimbali.
Bongo Movies Icons, Jacob Steven ‘JB’.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Ijumaa Wikienda hivi karibuni, maeneo ya Kinondoni, Dar, waigizaji hao walisema wanampongeza mwenyekiti wao kuwa Kamanda wa Vijana Tawi la Bwawani, Kinondoni na kutangaza kuwa yuko mbioni kugombea cheo kimojawapo kati ya ubunge au udiwani.
Staa wa Bongo Movies Single Mtambalike ‘Rich’.
“Unajua kuingia kwenye siasa ni utashi wa mtu hivyo inategemea anataka kufanya nini kwenye siasa. Mfano hai ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alivyoingia kwenye siasa hakuna aliyeamini kama angekuja kuwa mbunge, lakini sasa anawakilisha Jimbo la Mbeya Mjini,” alisema Rich.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger