Ni
wiki mbili zilizopita tangu mwanadada huyo achezee kichapo
toka kwa mwanamuziki wa bongo fleva Rashid Makwilo maarufu
kama Chid Benz akimtuhumu kumpotosha mkewe....
Ikumbukwe
kuwa kabla ya tukio hilo la Chid, Ray C alikwaruzana na
Legend wa bongo fleva TID baada ya kuposti kwenye mtandao
wake ujumbe wa kumuomba waongee....
TID alimuijia juu mrembo huyo kwa matusi kibao na kumtaka akae mbali nae na asimfuatefuate....
Ni
hivi karibuni Ray C ameanza harakati za kuokoa wasanii na
watu ambao wanahisiwa kutumia madawa ya kulevya, hali ambayo
imemfanya ajijengee maadaui wengi kwenye jamii ya watumiaji wa
madawa ya kulevya ambao wameapa kumsambaratisha....
"Ray
C anajisumbua bure tu, anashindana na sisi, sisi kama anaona
tumepotea atuache,kwanini asihangaike na mabwana zake kwanza?
huyu demu vipi?," alisikika teja mmoja maarufu kwa jina la Lima wa Tandika.
Lima
aliyekuwa akipewa sapoti na wenzake waliokuwa pembeni yake
aliendelea kufunguka kuwa Ray C asiendelee kuumiza kichwa kudili
nao, kama yeye ni mwanaharakati wa kweli basi adili na
wanaowafikishia hayo madawa....
"Mi
nashangaa kumuona akihangaika na sisi wakati kuna watu ambao
anapaswa adili nao. Awatafute wale kama kweli yeye ni shujaa," aliongeza kijana mmoja aliyeonekana kuzidiwa na kilevi.
Kijana
huyo alimuonya mwanadada huyo asiwafuatilie, lasivyo atahatarisha
maisha yake kwani wakubwa wakijua watakasirika sana na
wanaweza kumfanyia chochote.
"Mngemshauri tu aachane na sisi, wakubwa wetu wakijua ni kesi kubwa mno, sijui kama anaweza kupambana nao,"aliongeza kijana huyo.
Teja
huyo alienda mbali zaidi na kudai kuwa alichofanyiwa na TID
na Chid Benz ni trela tu, akitaka picha kamili aendelee
kuwafuatilia.
No comments:
Post a Comment