Showing posts with label RAY C. Show all posts
Showing posts with label RAY C. Show all posts

RAY C SASA ATAKA KUOLEWA NA MZEE, VIJANA KAWACHOKA

Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpenzi wala hajapata mtu wa kumuoa ila anataka kuolewa na mzee atakayeweza kumlea.
Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Akizugumza na wanahabari wetu kwenye mgahawa wake wa Ray C uliopo Mwananyamala, Dar, mwanadada huyo alisema yeye kama mwanamke anatamani kuolewa na kupata mtoto si na ‘serengeti boy’ bali mzee.
Aliendelea kutiririka kwamba akikosa wa kumuoa atatafuta mwanaume atamlipa kwa ajili ya kuzaa naye tu lakini ni pale atakapokuwa anaweza kulea  mwenyewe.
Ray C aliongeza kuwa, kwa sasa anatafuta wadhamini kwa ajili ya kuendesha taasisi yake ya Ray C Foundation kwani amefanikiwa kuwasaidia watu wengi kupata kazi na kuachana na dawa za kulevya.
Read more >>

RAY C ALA TENDA NONO, SASA KUTOKUMBUKA TENA MAISHA YA MUZIKI

Mungu mkubwa! Baada ya kupitia kipindi kigumu cha kutumia madawa ya kulevya ‘unga’ kisha kunusuriwa, super lady kwenye Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, hatimaye mambo yameanza kumnyookea baada ya kulamba shavu tenda nono ya kulisha Hospitali ya Mwananyamala, Dar.
Super lady kwenye Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa Wikienda, Ray C almaarufu Kiuno Bila Mfupa amefungua bonge la ‘restauranti’ maeneo ya Mwananyamala Hospital,  ambapo amepata tenda ya kuwahudumia chakula wafanyakazi wa hospitali hiyo na Idara ya Maji (Dawasa) ambapo anafanya kazi hiyo kwa saa ishirini na nne na muda mwingi anakuwepo yeye mwenyewe.
“Bidada sasa hivi yupo njema sana. Kalamba shavu la kulisha Hospitali ya Mwananyamala na Dawasa na hapo ni mchana na usiku so yupo bize kinoma.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu waliusaka mgahawa huo na kufanikiwa kuupata ambapo walimkuta Ray C akiwa bize kuhudumia wateja ambapo alisema: “Namshukuru Mungu kwani nimepata tenda ya kuwapikia chakula wafanyakazi wa Mwananyamala na wale wagonjwa ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya.”
Read more >>

PICHA ZA RAY C AKIWA MTAANI KUHAMASISHA MATEJA KUACHA UNGA





 Ray C Foundation Wiki iliyopita tuliwatembelea waathirika wa madawa ya kulevya Kinondoni!!!tumeongea nao sana na kuwahamasisha waje kupata Tiba ya Methadone Mwananyamala....nimefurahisana kusikia kutoka Kwao kwamba na wao wamechoka na Maisha ya utumwa.Tuko pamoja nao kuhakikisha tunawasaidia.


Read more >>

BAADA YA KUWA NA BIFU NA CHID BENZ, MAISHA YA RAY C SASA YAO HATARINI, WAVUTA BANGI WAAHIDI KUMSHIKISHA ADABU

Wiki  za  hivi  karibuni  mwanamuziki  wa  bongo  fleva  ambaye  pia  ni  mwanaharakati  wa  kupinga  matumizi  ya  dawa  za  kulevya  Rehema  Chamila  'Ray C'   amepatwa  na  misukosuko  mingi  ambayo  haikuwa    mbali  sana  na  mahusiano  na  dawa  za  kulevya....
Ni  wiki  mbili  zilizopita  tangu  mwanadada  huyo  achezee  kichapo  toka  kwa  mwanamuziki  wa  bongo  fleva  Rashid  Makwilo  maarufu  kama  Chid  Benz  akimtuhumu  kumpotosha  mkewe....
Ikumbukwe  kuwa  kabla  ya  tukio  hilo  la  Chid, Ray  C alikwaruzana  na  Legend  wa  bongo  fleva  TID  baada  ya  kuposti  kwenye  mtandao  wake  ujumbe  wa  kumuomba  waongee....
TID  alimuijia  juu  mrembo  huyo  kwa  matusi  kibao  na  kumtaka  akae  mbali  nae  na  asimfuatefuate....
Ni  hivi  karibuni  Ray  C  ameanza  harakati za  kuokoa  wasanii  na  watu  ambao  wanahisiwa  kutumia  madawa  ya  kulevya, hali  ambayo  imemfanya  ajijengee  maadaui  wengi  kwenye  jamii  ya  watumiaji  wa  madawa  ya  kulevya  ambao  wameapa    kumsambaratisha....

"Ray  C anajisumbua  bure  tu, anashindana  na  sisi, sisi  kama  anaona  tumepotea  atuache,kwanini  asihangaike  na  mabwana  zake  kwanza?  huyu  demu  vipi?,"   alisikika  teja  mmoja  maarufu  kwa  jina  la Lima  wa  Tandika.
Lima  aliyekuwa  akipewa  sapoti  na  wenzake  waliokuwa  pembeni  yake  aliendelea  kufunguka  kuwa  Ray  C asiendelee  kuumiza  kichwa  kudili  nao, kama  yeye  ni  mwanaharakati  wa  kweli  basi  adili  na  wanaowafikishia  hayo  madawa....
"Mi  nashangaa  kumuona  akihangaika  na  sisi  wakati  kuna  watu  ambao  anapaswa  adili  nao. Awatafute  wale  kama kweli  yeye  ni  shujaa," aliongeza  kijana  mmoja  aliyeonekana  kuzidiwa  na  kilevi.
Kijana  huyo  alimuonya  mwanadada  huyo  asiwafuatilie, lasivyo  atahatarisha  maisha  yake  kwani  wakubwa  wakijua  watakasirika  sana  na  wanaweza  kumfanyia  chochote.
"Mngemshauri  tu  aachane  na  sisi, wakubwa  wetu  wakijua  ni  kesi  kubwa  mno, sijui  kama  anaweza  kupambana  nao,"aliongeza  kijana  huyo.

 Teja  huyo  alienda  mbali  zaidi  na  kudai  kuwa  alichofanyiwa  na  TID  na  Chid  Benz  ni trela  tu, akitaka  picha  kamili  aendelee  kuwafuatilia.
Read more >>

RAY C: NAHAKIKISHA CHID BENZ ANAKWENDA JELA

NYOTA wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye hivi karibuni aliripotiwa kupokea kipigo cha maana kutoka kwa msanii mwenzake, Rashid Makwilo almaarufu Chid Benz, ameibuka na kudai kuwa atahakikisha rapa huyo anaozea jela kwa kitendo hicho alichomfanyia.
Nyota wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Akizungumza na gazeti hili, Ray C alisema amejikuta akipatwa na dhamira hiyo kutokana na msanii huyo, licha ya yeye mwenyewe na mama yake kumpigia simu za kutaka amsamehe, lakini anakana mbele za watu anapoulizwa, tena hadi redioni.
“Chid na mama yake wamenipigia simu kutaka nimsamehe lakini ninashindwa kwa sababu akiulizwa na watu anakataa hajanipiga, sasa kama hajanipiga anaomba msamaha wa nini, nimekwenda kwao na polisi kama mara tano lakini haonekani, inaonekana amejificha sehemu, mimi nasema awaonee haohao wasiojua sheria,” alisema msanii huyo ambaye hivi sasa anaendesha vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya.
Msanii wa Bongo Fleva, Rashid Makwilo almaarufu Chid Benz.
Alipoulizwa kuhusu kauli hiyo, Chid Benz mwenye tuzo tano za Kili, licha ya kukiri kumpigia Ray C simu pamoja na mama yake, alikataa kupiga kwa ajili ya kuomba msamaha kwa sababu hakumpiga msichana huyo mkongwe katika Bongo Fleva.
“Mimi nimpige Ray C? Halafu achubuke mguuni? Chid Benz angempiga angepasuka sura na angevimba kila sehemu. Yeye anajua nini kilitokea lakini anasema maneno yasiyokuwepo ilimradi apate huruma ya watu. Nilishamkataza kuwa karibu na mzazi mwenzangu kwa kuwa najua kampuni yake haina future.
“Mbona hasemi kama nilishawahi kwenda pale na kumweleza sitaki na akaniomba msamaha?
“Mimi sikumpiga, mchubuko alioupata ni mchecheto wake tu baada ya kujikwaa na kuanguka wakati akinikimbia, mimi nichukue cheni? Hayo ni mambo ya kizamani kwamba mtu ukimpatia sababu unasema amechukua pesa sijui na nini, siwezi kuchukua cheni ya Ray C, kwa maisha gani aliyonayo?

“Anasema nilimpigia simu kumuomba radhi, ni kweli lakini siyo kumwomba radhi, nilimpigia na kumwambia tuachane na haya mambo, sisi wote tunaonekana mateja tu mbele za watu ambao tumeshindwana huko sasa tunataka publicity.
“Wanaosema mimi ni mkorofi hawanijui, kama ni hivyo mbona ile kesi ya kumpiga msichana kule Ilala nimeshinda?” alihoji Chid Benz.
Read more >>

"KUZAA NAPENDA ILA NAOGOPA UCHUNGU WA KUZAA" RAY C

Husika na kichwa cha habari hapo juu!!
Kutoka kwenye mtando wa INSTAGRAM  dada yetu Rehema ameamua kufunguka yake ya moyoni kuhusu kutamani kuwa na mtoto.....Sina mengi  soma mwenyewe hapo chini.
Wako katika Udaku,
Mdadisi wa Mambo
"Yani nikiona watoto siku hizi natamani sana kuwa na mtoto nadhani umri umefikia wa kupata katoto hata tuwili tu...ni wangapi wangependa kumuona mwanangu mtarajiwa....yani nikiona MTU amebeba kachanga nachanganyikiwa na hamu sana ya kutoa kopi Yangu,niombeeni ingawa stori za labour zinatisha lakini na hamu sana....uwi sijui itakuwaje nikimuona mwanangu kwa Mara ya kwanza yani naeza zimia......"
By Ray C
Read more >>

CHID BENZ AMBUTUA MANGUMI RAY C, HABARI KAMILI IPO HAPA

evu! Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, anadaiwa kukwaa kisanga kingine kibaya baada ya kukurupuka kutoka nyumbani kwake na kwenda kumvamia staa mwenzake, Rehema Chalamila ‘Ray C’ nyumbani kwake anapoishi na kumtwanga makonde ikiwa ni siku chache tangu jamaa huyo apate msala mwigine wa aina hiyo.
Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.
TUJIUNGE NYUMBANI KWA RAY C
Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita nyumbani kwa Ray C, Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo ilisemekana kwamba Chid Benz alimvamia mishale ya saa 4:00 usiku kwa gia ya kumsaka mzazi mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Mariam.
Mwanaisha aliyepigwa na Chidi Benz hapo awali.
CHID BENZ ATAKA KUMUONA MWANAYE
Ilidaiwa kwamba Chid Benz alisema kuwa alizungumza na mpenziye huyo kwamba alitaka kwenda kumuona mwanaye ambapo Mariam alimjibu kwamba kwa muda huo alikuwa nyumbani kwa Ray C  Changanyikeni.
UNGA WATAJWA
Sosi wetu alidai kwamba baada ya kujibiwa hivyo, Chid Benz alianza kulalama na kumwambia anamfuata palepale kwa nini usiku ule alale kwa Ray C, wakati ana uwezo wa kwenda nyumbani au amekwenda kwa staa huyo ili kunywa dawa zao za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya ‘unga’, jambo ambalo jamaa huyo siku zote huwa hataki hata kulisikia masikioni mwake.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
CHID BENZ AWAVAMIA
“Huwezi kuamini baada ya muda kama wa saa moja, Ray C na Mariam wakiwa ndani wakitazama TV, ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu kisha akaingia Chid Benz na kumdaka Mariam na kuanza kumshushia kipigo.“Yaani huo mshtuko walioupata walidhani wamevamiwa na Al-Shabaab.
KIBAO CHAMGEUKIA RAY C
“Mungu mkubwa kwa sababu Mariam alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia chumbani ndipo kibao kikamgeukia Ray C.
Sehemu ya damu chumbani kwa Ray C kutokana na kipigo cha Chidi Benz..
“Ray C akiwa anashangaa ghafla naye alipokea kipigo kikali kutoka kwa Chid na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini.
RAY C AKIMBILIA KWA MAJIRANI
“Baada ya kuona maji yanazidi unga, Ray C alitafuta upenyo na kukimbilia kwa majirani huku akipiga kelele za kuvamiwa, mara moja majirani waliambatana naye mpaka nyumbani kwake.
“Walipofika Chid Benz alikuwa ametumia staili za kininja kwa kuruka geti na kutokomea kusikojulikana huku akiwaacha Ray C na Mariam wakiangua vilio kwa kipigo kikali walichopokea.
RAY C AVUJA DAMU
“Ray C aliumia mkono na mguu ambao ulionekana ukivuja damu. Mariam alikuwa akililia mbavu zake kuchakazwa kwa makonde mazito na upande mwingine baadhi ya vyombo vya ndani vikionekana kuvunjwa na vingine kusambaratishwa kufuatia tafrani iliyozuka muda mfupi baada ya Chid Benz kutia maguu nyumbani hapo,” chanzo kilishusha madai hayo mazito.
RAY C ATIRIRIKA SAKATA LILIVYOKUWA
Akizungumzia na gazeti hili Alhamisi iliyopita juu ya sakata hilo, Ray C alisimulia mkasa mzima: “Kweli Chid Benz alikuja nyumbani kwangu na kunivamia.
“Alinipiga vibaya sana na kuvunja baadhi ya vitu vya ndani kwangu, jambo ambalo lilinishangaza zaidi ni namna alivyopafahamu nyumbani kwangu hadi kuja kunifanyia fujo nikiwa na mzazi mwenzake, Mariam ambaye nilitoka naye ofisini kwangu.
“Ujue jana (Jumatano) tulikuwa na kazi sana ofisini kwangu mimi na Mariam, sasa kutokana na kubanwa na kazi kweli muda ulienda sana hivyo nikamwambia Mariam akalale kwangu.
“Kwa kuwa muda ule ilikuwa ngumu kwenda kwao Mbezi Beach, Mariam alikubali na tulikwenda wote nyumbani kwangu.
“Huko nyuma Mariam alikuwa mwathirika wa madawa ya kulevya lakini baada ya kusikia mimi nimeacha, naye aliachana nayo na kuanza kutumia dawa za kuondoa sumu.
“Tumeendelea kutumia naye dawa na sasa ameshapona kabisa hivyo kuna baadhi ya kazi nimekuwa nikimshirikisha kunisaidia kwenye ofisi yangu. Pia alishawahi kumshawishi Chid Benz ili aje kutumia dawa lakini jamaa alikataa na kumfanyia vurugu sana huku akimkataza kuwa na mimi kwa madai mimi ndiyo namfanya amwambie kuachana na utumiaji dawa za kulevya.
“Sasa jana alipojua hivyo nadhani Chid Benz alikuja kutimiza dhamira yake ambayo siku nyingi alikuwa akiahidi kunipiga.”
SOO LIPO POLISI
Ray C alisema baada ya tukio hilo alikwenda kuripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kufunguliwa jalada la kesi ambapo Chid Benz anasakwa na polisi.
Juhudi za kumpata Chid Benz hazikuzaa matunda kwani simu yake haikuwa hewani hivyo jitihada zinaendelea na kama ana ufafanuzi au utetezi anaweza kutupigia.
CHID BENZ NI TATIZO?
Chid Benz anadaiwa kuwa ni tatizo kwani tukio hilo la Ray C amelifanya wakati akiwa na tukio la pili kwa wanawake kwani kwenye Mahakama ya Mwanzo, Ilala ana kesi mbichi aliyoshitakiwa kwa kosa la kumpiga mrembo aitwaye Mwanaisha.
Mbali matukio hayo pia Chid Benz ana rekodi ya kukorofishana na wasanii wenzake kama Kalapina na marehemu Ngwea.
Read more >>

RAY C AMFUNGUKIA TID MANENO MAZITO



Baada ya kukaa kimya kufuatia kutukanwa na TID kupitia mtandao wa Instagram, Ray C amemjibu staa huyo.

“Hi everyone!!!Asanteni kwa maombi yenu!mama anaendelea vizuri Mungu ni Mwema…………(na kuhusu @tidmnyama -Nimeona post yako,Asante kwa matusi yako ila sikuwa na nia mbaya tofauti na ulivyofikiria anyway Nakuombea kwa Mungu akuepushe na majanga ya dunia!ubarikiwe sana babaa,” ameandika Ray C.

Ray C ametoa kauli hiyo baada ya siku kadhaa zilizopita TID kumtukana baada ya kucomment kwenye post yake: Come let’s talk Tid ur the best musician in east Africa pls lets talk @tidmnyama.” Hata hivyo Ray C hakufafanua anataka waongee kuhusu jambo gani na TID.

TID alijibu: “Bi*ch leave me alone am not ur type also I don’t need shit from you,ur mistake is yours nakuomba can u jus f*ck off,help ur boyfriend,I have never liked you,full stop,”
Read more >>

MASHABIKI WAMPONDA TID, KISA NI MATUSI YAKE KWA RAY C

Huu ni muendelezo wa story ya jana inayomhusu TID kumtusi sana Ray C baada ya Ray C kumwambia TID katikak intsgram kwamba aende kwa Ray C waongee maana TID ni msanii bora Afrika Mashariki.

Baada ya Matusi ya TID kwa Ray C, mashabiki wa muziki wamemshushia maneno (matusi) mazito TID. Maoni ya raia hao yanaonesha kwamba TID aliitwa na Ray C ili apewe ushauri wa kuachana na madawa ya kulevya kama alivyofanya kwa wengine ambao baadhi wapata matibabu na wanakaribia kupona. 
Kwa kutunza maadili ya tovuti yetu hatutaweza kuyaweka maoni ya mashabiki hao yaliyojaa matusi mengi sana kwa TID. Kama TID amebahatika kuyasoma maoni hayo atakuwa aidha kakasirika sana au atajifunza kitu.
Read more >>

DIVA NA RAY C WAJILAUMU BAADA YA KUMPONDA DIAMOND'' GK AHUSISHWA ''ETI KOFIA KAMA GANDA LA CHUNGWA

BALAA JINGINE LAMWANGUKIA DIVA WA CLOUDS NA RAY C HUKO INSTAGRAM BAADA YA KUMPONDA CHIBU (DIAMOND) KWA KUKOSA TUZO ZA MTV MAMA

Read more >>

RAY C ASIMULIA ALIVYOPONEA CHUPUCHUPU KUFA

MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya Dengue.
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, akiwa kwenye red carpet ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Akifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa huo.
Alisema kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari lake na kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.
Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu.
“Huwezi kuamini baada ya madaktari kunipima na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue, walinishangaa sana hata namna nilipofika pale na kwamba sikutumia dawa yoyote ya kutuliza maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni lazima utatafuta tu dawa ya kukufanya upoze maumivu.
“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’ unaweza kupoteza maisha mara moja.
“Katika magonjwa ya ajabu na yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja basi huu ni ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa iwe macho sana maana haufai hata kidogo.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.
“Mateso niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa Mwananyamala ni elimu tosha kabisa na kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa nchi basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada za haraka kuhakikisha wanapata chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol tu!” alimalizia Ray C.
Read more >>

UGONJWA LA RAY C, WAPUKUTISHA WATU MIL 2, MIL 100 WAAMBUKIZWA

MARADHI yanayomsumbua mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ni tishio, Gazeti la Mastaa, Amani limeelezwa.
Mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akiwa hoi hospitali.
Ray C anaugua ugonjwa wa Homa ya Dengu ambao kitaalam hujulikana kama Dangue Fever. Ulibainika baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni, Mwananyamala jijini Dar na baadaye kulazwa hospitalini hapo.
Staa huyo wa muziki ambaye pia hujulikana kama Kiuno Bila Mfupa alifikishwa hospitalini hapo, Jumapili iliyopita  mchana baada ya hali yake kuwa mbaya.
KUTOKA KWA CHANZO
“Ni kweli Ray C amelazwa hapa Mwananyamala. Ameletwa leo (Jumapili) saa tano mchana,” alisema mtoa habari wetu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

Mtoa habari huyo, naye alikuwa mgonjwa  alilazwa katika wodi namba tano, hospitalini hapo ambayo Ray C alikuwa amelazwa.
“Afya yangu si nzuri sana, lakini nimeweza kumtambua. Namfahamu sana Ray C. Nina hakika ndiye aliyelazwa hapa,” aliendelea kusema lakini hakueleza ugonjwa anaougua.
Ray C akiwa na Rais Kikwete
MAPAPARAZI WAINGIA KAZINI
Baada ya timu yetu kunasa taarifa hizo, Jumatatu jioni mapaparazi wetu walitinga hospitalini hapo na kuthibitishiwa kuwa Ray C alikuwa mgonjwa na kulazwa.

Hata hivyo, juhudi za kuingia wodini kuonana naye hazikuzaa matunda kwa vile muda wa kuwaona wagonjwa ulikuwa umekwisha kwa siku hiyo.
Hata pale walipojitambulisha kuwa ni waandishi, wahusika walijibu kwa kifupi: “Haiwezekani, anatakiwa kupumzika.”

DAKTARI ATHIBITISHA
Mmoja wa madaktari wanaoshughulikia afya ya msanii huyo alithibitisha kuwa Ray C ana dalili zote za ugonjwa huo, akasema: “Ni kweli ana dalili zote za dengu, lakini siruhusiwi kutoa taarifa za mgonjwa, labda kwa ruhusa yake mwenyewe au mama yake mzazi.”

AMANI TENA
Waandishi wetu hawakuchoka, siku iliyofuata, Jumanne asubuhi na mapema, mapaparazi walidamkia hospitalini hapo kwa lengo la kumjulia hali staa huyo lakini walipoingia wodi namba tano alipokuwa amelazwa, hakuwepo!

Ilikuwa ni muda wa kuwaona wagonjwa, waandishi wakakuta kitanda kitupu, walipouliza kulikoni wakaelezwa amehamishiwa wodi maalum.
“Amehamishiwa kwenye chumba maalum kwa sababu waandishi walikuwa wanasumbua sana kutaka kumuona. Kama unavyojua tena, wodi ya kawaida inakuwa haina uangalizi mkubwa.
“Mtu yeyote anaweza kuingia ikiwa tu muda wa kuwaona wagonjwa utakuwa umefika. Jambo hilo limewakera sana ndugu ndiyo maana wamezungumza na madaktari na kumhamisha,” mtoa habari mwingine alisema kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
UFAFANUZI
Daktari mwingine aliyezungumza na Amani hospitalini hapo kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini kwa vile si msemaji alisema: “Kuhusu kulazwa, ni kweli amelazwa na anaumwa, lakini kumuona ni ngumu.

“Unajua Ray C ni maarufu, kumuacha kwenye wodi ya kawaida ni kumsababishia usumbufu usio na maana, wengi wanataka kumuona hasa waandishi kama ninyi. Anahitaji kupata muda wa kutosha kupumzika.”
KWA NINI TISHIO?
Homa ya Denge (Dengue Fever) kama ilivyoelezwa hapo juu ni tishio. Virusi vya ugonjwa huu husabazwa na mbu aina ya Aedes ambaye yupo katika mgawanyiko wa jamii tisa;  Aedes Australis, Aedes Albooictus, Aedes Aegypti, Aedes Contator, Aedes Cinereus, Aedes Ructcus, Aedes Polynesiensis, Aedes Scutellaris na Aedes Vexans.

Mbu wa kike aina ya Aedes anapomng’ata binadamu mwenye maambukizi ya Homa ya Dengu huanza kuathirika mwenyewe na baada ya siku 8-10 huathirika zaidi kiasi cha mate yake  kubeba virusi vya homa hiyo.
Dengu pia husambazwa kwa njia ya kuongezewa damu au kupewa viungo vya mtu aliyeathirika. Inawezekana kwa mama kumwambukiza mtoto wakati wa ujauzito au kwenye kujifungua.
Yapo maambukizi ya mtu na mtu wakati wa kujamiiana au mwingiliano wa damu lakini kitaalam inafafanuliwa kwamba si kawaida hali hiyo kutokea.

Ugonjwa huo unadhibitiwa kwa kumpa mgonjwa dawa ili kuzuia kutapika, maumivu ya mwili na kupewa dripu za maji lakini hakuna dawa maalum za tatizo hilo na mgonjwa akipona huweza kuugua tena siku yoyote.
TAARIFA ZAIDI ZA KIDAKTARI
Gazeti hili liliwahi kufunga safari hadi Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni, Dar na kufanikiwa kuzungumza na mganga mkuu wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Alithibitisha kuwepo kwa gonjwa hilo baya ambapo wakazi wengi wa jiji wameugua na wapo wanaoendelea kuugua.
“Huu ugonjwa haujaanza leo, inaonekana kama hospitali hii inahusika kwa kiasi kikubwa na tatizo hilo kwa sababu mimi niliamua kuachana na habari za kuwatibu watu malaria tu nikawa makini kutazama na ugonjwa huu ambao wengi hawautilii mkazo,”alisema.
Daktari huyo alizidi kusema kuwa, ugonjwa huo unaenezwa na mbu weusi wanaorandaranda ambao wanapenda kukaa sehemu zenye uchafu na majimaji.
“Wale mbu weusi wanaeneza kwa kasi ugonjwa huu ni tofauti kabisa na wale wanaoneza ugonjwa wa malaria,” alisema.

Akielezea dalili za ugonjwa huo mganga huyo alisema zinafanana na zile za ugonjwa wa malaria, mtu kuhisi joto kali mwilini, maumivu ya kichwa, kutapika, tumbo, maumivu ya mwili na misuli.
Alisema ugonjwa huo ulizidi kushika kasi mwaka huu katika kipindi cha mafuriko hivyo idadi ya wagonjwa aliowatibu kwenye hospitali yake ikaongezea, kutoka wagonjwa 4 mwaka jana mpaka kufikia wagonjwa 20 tangu Januari, 2014 kutokana na mvua iliyosababisha kuwepo kwa madimbwi kila kona.
MPAKA SASA HAUNA TIBA
Ugonjwa huu mpaka sasa hauna tiba ya uhakika, kinachifanywa kwa wagonjwa wanaogudulika kuwa nao ni kutibiwa tu dalili ili usizidi kusambaa mwilini.

WALIOATHIRIKA
Taarifa kutoka kwa wataalamu wa afya zinasema kuwa, mpaka sasa takribani watu milioni 100 duniani kote wameambukizwa ugonjwa huo na wengine milioni 2 wamefariki dunia baada ya kuugua.

TUMUOMBEE
Hata hivyo, jambo muhimu kwa Watanzania wote na wapenda burudani ni kumuombea Ray C apate nafuu haraka na kurejea kwenye majukumu yake kama kawaida.

KUMBUKUMBU MUHIMU
Ray C kwa muda mrefu alikuwa na matatizo ya kiafya lakini hivi karibuni afya yake ilitengemaa na usiku wa Jumamosi ya Mei 3, mwaka huu (kuamkia siku aliyolazwa) alionekana akiwa mwenye afya njema katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar kwenye shughuli za tuzo za muziki za Kilimanjaro Tanzania Music Awads (KTMA).

Ilikuwa mara ya kwanza kwa msanii huyo kuonekana hadharani baada ya kujificha kwa muda mrefu kufuatia matatizo yake ya kuugua kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’.
GLOBAL ILISHAANDIKA KUHUSU DENGU
Kuibuka kwa ugonjwa wa Homa ya Dengu kuliripotiwa kwa mara ya kwanza kwenye gazeti la Risasi Jumamosi ya Mei 3,2014 likiwa na kichwa cha habari ukurasa wa mbele kisemacho:GONJWA LISILO NA TIBA YA UHAKIKA LAIBUKA.

Ray C aliruhusiwa kutoka hospitali juzi saa 9:50 baada ya afya yake kuimarika.
Read more >>

UGONJWA MPYA WAMUWEKA HOI KITANDANI MSANII RAY C

Nimepata Habari kuwa Mwanamuziki Ray C yupo hoi Kitandani Akiugua Ugonjwa Mpya Unaojulikana kama Homa ya Denge...

Inasemekana Baada ya kutoa tuzo ya Kill  Siku ya Jumamosi Kesho yake alianza kuumwa Kichwa na Baadae alipelekwa Hospitalini Mwananyamala Akidhani ana Malaria, Alipopimwa ikagundulika unaumwa huo ugonjwa wa Denge......

Ugonjwa huo inasemekana unaambikizwa kwa kung'atwa na Mbu
Get Well Soon
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger