BASI LATUMBUKIA MTONI MKOANI IRINGA.

Basi la Japanese lenye namba za usajili T 261 CMK aina ya YUTONG likiwa limetumbukia mtoni na kusababisha abiria kadhaa waliokuwa wakisafiri na basi hilo kutoka Ikonda wilayani Makete kwenda Makambako mkoani Njombe kujeruhiwa. Hadi tunaondoka eneo la tukio hakuna abiria aliyepoteza maisha na majeruhi wote waliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi. Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa nane mchana.
Majeruhi wa ajali hiyo akizungumza na mwandishi wetu muda mchache kabla ya kuwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi. Mmoja wa wafanyakazi wa basi hilo ambaye naye amejeruhiwa kidogo katika ajali hiyo akiwa katika hali ya huzuni.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger