Mwili wa mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake baada ya kukanyagwa na lori na kupoteza maisha.
Showing posts with label AJALI. Show all posts

AJALI ZAENDELEA KUFULULIZA, NYINGINE YAUA MBEZI JIJINI DAR
Mwili wa mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake baada ya kukanyagwa na lori na kupoteza maisha.AJALI NYENGINE MBAYA SANA MAENEO YA GAIRO BASI LA AIRBUS YATOKEA .
Basi la kampuni ya Airbus lililokuwa likitoka Dar es Salaam leo kuelekea Tabora limepinduka katika maeneo ya maeneo ya Kiegeya Gairo.Shughuli za uokozi zikiendelea muda mfupi uliopita
Haijulikani idadi kamili ya watu waliopoteza maisha lakini ni wengi na wengine wamejeruhiwa vibaya sanaaaaaaa!!
“Picha hazifai kuonwa na mimi niko eneo la tukio kwa ajili ya uokozi..viongozi mbali mbali wa serikali tunao hapa..kwakweli ni majonzi vilio nk,” ameandika shuhudu mmoja. Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana mara moja

Baadhi ya mili ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo

KIJIJI CHA NOUSHAD BAITRAIS CHA TEKETEA KWA MOTO HUKO ZANZIBAR,PICHA ZA TUKIO ZIKO HAPA

Hali ndiyo hilikuwa hivi huko Zanzibar katika kijiji cha Baitrais kinachomilikiwa na Noushad aliekuwa mfadhili wa timu ya Malindi ya Unguja. soma na hii Wema sasa afungua kinagaubaga kuhusu suala la kuajiriwa na Kajala msikilize hapa===>>http://mdadisitz.blogspot.com/2014/09/msikilize-wema-akifunguka-juu-ya-suala.html
KAZA MOYO WAKO USOME, MWANAMKE AGONGWA NA DALADALA UBUNGO MAJI
HiIi ndilo gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T454 BBV lililomgonga dada huyo.
Mwanamke mmoja (jina halijafahamika) aliyekuwa anavuka barabara ya
Morogoro maeneo ya Ubungo maji kutoka ng'ambo ya tank na kuelekea upande
wa Tanesco amegongwa na gari ya daladala aina ya Toyota Coaster
lililodaiwa kuvunja sheria likiwa linapita kwenye barabara ya magari ya
mwendo kasi.
Katika ajali hiyo dereva wa basi(daladala) hakupatikana kwani alikimbia baada ya ajali
AJALI: LORI LA MAFUTA LAANGUKA KIMARA, WANANCHI WAGOMBANIA KUCHOTA MAFUTA
Lori la mafuta baada ya kuanguka.
Foleni iliyosababishwa na ajali hiyo eneo la Kimara, Dar.
Polisi wakidumisha ulinzi eneo la ajali.
AJALI ENEO LA AFRIKANA JIJINI DAR
Zoezi la kulivuta gari hilo kutoka mtaroni likianza.
Zoezi la kutoa gari hilo mtaroni likiendelea.
Muonekano wa gari hilo baada ya kutolewa mtaroni likiwa limeharibika vibaya.
Dereva wa gari hilo la Nissan Hard Body akilitazama gari lake kwa karibu lilivyoharibika.LIONE GARI ALILOPATA NALO AJALI MBUNGE RAGE HUKO DODOMA JANA.

Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) Ismail Aden Rage, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, akiwa amelazwa kwenye hospitali ya Rufaa, Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014. Rage alipata ajali eneo la Chigongwe, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, wakati akielekea mjini humo tayari kushiriki vikao vya Bunge Maalum vinavyoanza Jumanne Agosti 5, 2014

Mbunge wa Sikonge mkoani Tabora kupitia CCM, ambaye pia ni Mujumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Said Nkumba, akimjulia hali Rage, hospitalini mjini Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014.
AJALI: HOOD LAUA WATANO ARUSHA
Muonekano wa basi la Hood kwenda Mbeya baada ya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha asubuhi ya leo.
Wananchi wakiwa wamekusanyika baada ya basi la Hood kwenda Mbeya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha.
Watu 5 wamekufa baada ya basi la Hood kwenda Mbeya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha asubuhi ya leo, wengi wajeruhiwa.
BASI LA MORO BEST LAUA WATU ZAIDI YA 17 LEO HII
Baadhi
ya Miili ya Marehemu muda mchache baada ya kupata ajali kabla ya
kupelekwa Hospitali.Basi hilo lilikuwa linatoka Mpwapwa kwenda Dar es
salaam

Watu
zaidi ya 10 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 56
wamejeruhiwa katika ajali ya basi la MORO BEST iliyotokea leo majira ya
saa mbili asubuhi.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio Basi hilo limegongana na lori
katika eneo la Pandambili Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma na kwamba
miongoni mwa waliofariki ni pamoja na madereva na Makondakta wa magari
yote mawili.
Hata
hivyo chazo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na majeruhi wote
wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kongwa na wengine katika
hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Baadhi
ya wasamalia wema wakiwa wanaendelea kuokoa majeruhi na kuwaondoa
waliofariki ,ambapo idaiwa watu zaidi ya watu 10 wamepoteza maisha
Hivi ndivyo basi lilivyo Haribika
BAHATI BUKUKU APONEA CHUPUCHUPU KUFARIKI.
NI kweli ajali haina kinga! Nyota wa nyimbo za
Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na maeneo kadhaa ya
mwili (nusu kifo) kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama wala kutembea
kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la Ranchi ya Narco
wilayani Kongwa, Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi, Ijumaa
Wikienda lina undani wa mkasa mzima.
Gari alilopata nalo ajali mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Bukuku aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945.
Kwa mujibu wa chanzo makini, katika ajali hiyo ambayo Bahati alikuwa
akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa gari
alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT
7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya miguu
na hawezi kutembea.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni wacheza shoo wa Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
ILIKUWAJE?
Habari zilidai kuwa gari hilo halikuwa na matatizo hivyo kumfanya dereva wake kukanyaga mafuta kwa wastani wa kilometa 120 kwa saa.“Sasa walipofika eneo la Kibaigwa, walikutana na lori likitokea Dodoma kwenda Morogoro, wakavaana kwa mbele. Nadia likatoka barabarani hadi porini likiwa limeharibika kuanzia kwenye shoo ya mbele, injini na siti za mbele halafu lori hilo likakimbia.
“Nadia ilipotulia, Bahati alijikuta hawezi kufanya chochote, dereva wake naye ameumia kwenye vidole vya miguu. Wale wawili waliokuwa siti ya nyuma, wote walijeruhiwa lakini mmoja si sana. Ilibidi yeye abaki pale na gari ili majeruhi wengine wakimbizwe Hospitali ya Wilaya ya Kongwa, Dodoma kwa matibabu,” kilisema chanzo hicho.
HABARI NYINGINE
Habari ambazo hazijathibitishwa na dereva wa Bahati zilisema kuwa, wakati gari hilo linakaribiana na lori, dereva wa lori aliwasha taa ‘full’ (mwanga mkali) hivyo kumfanya dereva huyo kushindwa kuona mbele vizuri, jambo ambalo ni kinyume na sheria za usalama barabarani.
ROSE MUHANDO, JENNIFER MGENDI WAFUNGA SAFARI
Ilidaiwa kuwa usiku huohuo, waimba Injili mahiri Tanzania, Rose Muhando na Jennifer Mgendi walipata taarifa za ajali hiyo na kufunga safari ya kwenda Kongwa kuangalia namna ya kuwahamishia majeruhi hao kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar.
ROSE MUHANDO
Rose Muhando alipotafutwa kwa simu juzi mchana na kuulizwa kuhusu kusafiri kwenda Kongwa, alikiri na kusema wameshafika na Jennifer Mgendi.
“Ndiyo tupo kwenye hekaheka ndugu yangu. Tuna dhamira ya kuwachukua majeruhi kuwapeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi,” alisema Rose.
JENNIFER MGENDI
Yeye alipopatikana alisema alishtushwa na simu asiyoijua usiku mnene na kuambiwa shoga yake huyo amepata ajali mbaya ya gari.“Kitu cha kwanza niliuliza hali yake, nikaambiwa ameumia mgongo, dereva wake mguu. Ndiyo nikaanza kuwataarifu wadau wengine na mimi kujiandaa kwa safari kutoka Dar kuja Kongwa usiku huohuo. Kwa kweli ameumia,” alisema Mgendi ambaye ni rafiki mkubwa wa Bahati.
Naye Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stella Joel alipozungumza na gazeti hili juzi, alikiri waimba injili hao kuondoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kumpa msaada mwenzao.
BAHATI BUKUKU AZUNGUMZA KWA TABU
Alfajiri ya juzi, mwandishi wa habari hizi alimpigia simu Bahati na kuongea naye kuhusu ajali hiyo ambapo huku akisikika kama anayepata tabu kwa maumivu, alisema:
“Ni kweli tumepata ajali, nimeumia mgongoni, dereva ameumia mguu. Namshukuru Mungu. Sijui nini kilitokea, nilishtukia kuona gari kubwa mbele yetu likituvaa, mara nikashtukia tuko porini. Lakini kabla ya safari Dar tulifanya maombi makubwa, najua Mungu ametunusuru na kifo kibaya,” alisema Bahati.
Mwandishi: “Unadhani nani alikuwa na kosa kati ya dereva wako na wa lori?”Bahati: “Sijui chochote. Halafu najisikia vibaya sana, tuwasiliane baadaye kaka ‘angu.”
UZOEFU WA DEREVA
Habari zinasema kwamba, Eddy ni dereva wa miaka mingi. Mbali na jijini Dar, pia amekuwa akiendesha magari kwenda nje ya Tanzania kama Burundi na Rwanda na katika ajali hiyo alikuwa akienda nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), hivyo ana uzoefu wa safari za usiku.
WATU WA INJILI NA AJALI ZA DODOMA
Kumbukumbu zinaonesha kuwa hii si mara ya kwanza kuripotiwa kwa ajali za magari mkoani Dodoma zikiwahusisha watu wa tasnia Injili Bongo.
Aprili, mwaka huu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama alipata ajali mbaya ya gari kwa kugongana na mwendesha bodaboda.Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Ipagala Mwisho, kilomita chache kabla ya kufika mjini Dodoma. Msama alikuwa kwenye gari lake aina ya Toyota Mark II GX 100.
Katika ajali hiyo, Msama na mwendesha bodaboda huyo waliumia sehemu mbalimbali za mwili na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.
Kabla ajali ya Msama haijapoa, Mei, mwaka huu, Edson Mwasabwite naye alipata ajali kwenye Barabara Kuu ya Dodoma–Morogoro. Alikuwa akitoka Dodoma kurudi Dar. Alinusurika.
Read more >>
Gari alilopata nalo ajali mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Bukuku aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945.Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni wacheza shoo wa Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

KIJANA WA MIAKA 26 AOZA MGUU, KISA AJALI
AMA kweli ng’ombe wa maskini hazai, kijana Peter Sitiwati (26),
mkazi wa Sinza ya Kwaremmy jijini Dar amejikuta akikatisha ndoto za
utafutaji maisha kufuatia kuoza mguu baada ya ajali mbaya ya gari.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzikati kwa sauti ya kukata tamaa, Peter alisema alipata ajali ya gari mwaka 2013 maeneo ya Sinza-Mori, Dar na kuumia vibaya mguu wa kulia.
’’Baada ya kugongwa na gari niliangukia mtaroni nikachomwa na kijiti kwenye mguu wa kulia. Nilikimbizwa Hospitali ya Palestina kutibiwa na baada ya muda mguu ulionesha kupona kwa juu, lakini kumbe ndani kidonda kilikuwa kibichi na kiliendelea kulika bila mimi kujua.
“Mwanzoni mwa mwaka huu (2014) nikaanza kushangaa usaha mwingi unatoka sehemu mbalimbali ya mguu tena na harufu mbaya, mguu ukaonekana umeoza tena una matundu matatu, si unauona ulivyo, hata watu hawapendi kukaa jirani na mimi,” alisema Peter huku akionesha mguu wake huo.
Peter alisema atashukuru kama atapata nauli ya kurudi kwao, Makambako, Njombe kwa vile ameona maisha magumu huku akiishi kwa kushindwa kula na kulala kwa shida.
“Ila namshukuru sana msamaria mwema anaitwa Louis, ndiye anayenisaidia kwa sasa,” alisema.
Aliongeza kuwa, baada ya kuhangaika kusaka nauli bila mafanikio, baadhi ya watu walimwambia atoe taarifa kwenye Magazeti Pendwa ya Global Publishers ambayo yanasomwa na watu wengi Tanzania, atasaidiwa.
“Napenda kuwaomba Watanzania mnaosoma Magazeti Pendwa ya Shigongo mnichangie pesa ili nipate matibabu na nauli ya kurudi kwetu. Wenye kukuguswa na tatizo langu wanaweza kunisaidia kwa kutumia namba ya simu 0716 122 780, Louis.”

BASI LATUMBUKIA MTONI MKOANI IRINGA.
Basi
la Japanese lenye namba za usajili T 261 CMK aina ya YUTONG likiwa
limetumbukia mtoni na kusababisha abiria kadhaa waliokuwa wakisafiri na
basi hilo kutoka Ikonda wilayani Makete kwenda Makambako mkoani Njombe
kujeruhiwa.
Hadi
tunaondoka eneo la tukio hakuna abiria aliyepoteza maisha na majeruhi
wote waliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi. Ajali hiyo imetokea jana
majira ya saa nane mchana.
Majeruhi wa ajali hiyo akizungumza na mwandishi wetu muda mchache kabla ya kuwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Mmoja wa wafanyakazi wa basi hilo ambaye naye amejeruhiwa kidogo katika ajali hiyo akiwa katika hali ya huzuni.

Subscribe to:
Posts (Atom)