DEVOTA ACHEKELEA OFISI BONGO MOVIE, HABARI KAMILI HII HAPA

Stori: mayasa mariwata
MUIGIZAJI wa filamu nchini, ambaye ni Katibu wa klabu ya Bongo Movie Unity, Devota Mbaga amesema amefurahi sana kuona kundi lao likipata ofisi za kuendeshea kazi zao.
Muigizaaji wa filamu nchini, ambaye ni Katibu wa klabu ya Bongo Movie Unity, Devota Mbaga (kushoto pichani).
Akipiga stori na paparazi wetu, alisema kwa kipindi kirefu klabu hiyo haikuwa na ofisi hivyo akiwa kama kiongozi muda wote aliumiza kichwa.
“Nina furaha mno maana siku siyo nyingi tutahamia rasmi kwenye ofisi zetu, naamini furaha hii si yangu tu bali ni kwa wasanii wote na wadau wa sanaa nchini, maana wengi walikuwa wakilalamikia kwani ilikuwa vigumu kutupata,” alisema.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger