MUIGIZAJI Bora wa Kike 2014 kupitia Tuzo za
Zanzibar Film Festival (Ziff), Esha Buheti ameapa kuwa iwapo atakuja
kujichora tatuu au kufanya mapenzi ya jinsia moja, Mungu aingamize
familia yake na kizazi chake chote.
Esha alitoa kiapo hicho juzikati alipokuwa akijibu swali aliloulizwa
na paparazi wetu kuhusiana na tuhuma za kudaiwa kujihusisha na mapenzi
ya jinsia moja zilizotua kwenye dawati la Risasi Jumamosi.
“Mimi ni
mtoto wa Kiislamu na nina maadili yote ya dini, siwezi kujihusisha na
mapenzi ya kinyume cha maumbile, mapenzi ya jinsia moja,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment