STAA
wa filamu Bongo, Mike Sangu, amefungukia ishu nzima ya kuvuliwa cheo
cha Uenyekiti wa Vijana Taifa chini ya Shirikisho la Filamu Tanzania
(Taff) na kusema shirikisho hilo halikumtendea haki.Mike alisema hayo alipozungumza na Risasi Jumamosi, ambapo alisema alishangaa kuona anavuliwa cheo baada ya kujiunga na Klabu ya Bongo Movie Unity akitokea Taff kitu ambacho si sahihi kwani aliamini shirikisho na klabu hiyo ni kitu kimoja.
“Shirikisho la filamu hawakunitendea haki hata kidogo, nijuavyo Bongo Movie Unity na Taff walishamalizana tofauti zao na Rais wa Taff, Simon Mwakifwamba alishawahi kulithibitisha hilo, hivyo sioni sababu ya kuenguliwa,” alisema Mike.
Nafasi ya Mike katika ngazi shirikisho hilo imechukuliwa na Ramadhani Kingalu ambaye alikuwa makamu wake wakati wa uongozi wake.
Alipotafutwa Mwakifwamba, alimchana vibaya Mike:
“Ameondoka kwa ubadirifu wa fedha, anadaiwa fedha kibao kutoka katika vyanzo tofauti, sisi tumemfukuza kabla hata hajajiunga na Bongo Movie sema yeye anatumia hicho kama kisingizio tu.

No comments:
Post a Comment