FLORA AJIBU TUHUMA ZA ‘UKOBE’

FUNGUKA! Staa wa filamu za Kibongo, Flora Mvungi ambaye ni mke wa ndoa wa msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ amefunguka kwamba mwaka huu ameshindwa kufunga Mwezi Mtukufu (ukobe) kwa sababu ananyonyesha.
Staa wa filamu za Kibongo, Flora Mvungi.
Akijibu minong’ono ya watu iliyohoji kwa nini hafungi, Flora alisema kutokana na mwanaye kuwa mchanga na kila mara anataka kunyonya, ameshindwa kufunga kwani imekuwa vigumu kutokana na kupatwa na njaa ya mara kwa mara.
“Jamani ngoja tu nimnyonyeshe mwanangu maana bado mdogo na mimi ni mzazi hivyo sikuweza kufunga, ninatakiwa nile kila wakati kwa sababu mwanangu ananyonya sana, msinitafsiri vibaya,” alisema Flora ambaye amekuwa kibonge kupindukia.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger