KUTOKANA na hivi karibuni mumewe, Hamis Baba ‘H.
Baba’ kuugua ugonjwa wa homa ya Dengue ‘Dengi’ na kulazwa Muhimbili,
msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi amesema alijikuta kwenye wakati
mgumu kuhofia mumewe angepoteza maisha.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Flora alisema ni Mungu tu
mumewe kupona kwani alikuwa katika hali mbaya ambayo mpaka yeye kama
mkewe alikuwa na hofu kubwa ya kifo haswa ukizingatia vifo vya wasanii
vilivyotokea mfululizo.
“Nilipoona wasanii wenzangu wakifariki dunia na mume wangu kuzidiwa
mpaka kulazwa Muhimbili, nilikuwa nina hofu kubwa ya kifo lakini
namshukuru Mungu amepona na tunaendelea na maisha kama kawaida, dengue
noma sana,” alisema Flora.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment