SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa
Salum ameonesha kukerwa kwake na mastaa wa Bongo ambao ni Waislam na
wanaishi na wenza wao bila ndoa, hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza na mwandishi wetu juzi, Shehe Alhad alisema kwa mujibu wa
imani ya Dini ya Kiislam, Muislam hupaswa kufunga mwezi mtukufu kama
hana matatizo ya kiafya.
Alisema kwa wale Waislam ambao wapo katika uhusiano usio wa ndoa nao
hutakiwa kujiandaa kwa mwezi huo wa toba kwa kutengana na wenza wao
mpaka mfungo utakapomalizika.
Shehe huyo aliongeza kuwa ni makosa
kwa Muislam kufunga akiwa anaishi na mpenzi wake pasipo ndoa na kuongeza
kuwa kwa kufanya hivyo ni sawa na kushinda na njaa.
“Mwislam yeyote asiye katika ndoa lakini akafunga mwezi mtukufu hali
akiwa anaishi na mpenzi wake ni bure na suala hilo ni sawa na
kujikalisha na njaa tu. Hata kama hawatashiriki zinaa lakini tunaambiwa
tusiikaribie zinaa.
“Hivyo lazima atengane na mpenzi wake huyo kwa kukaa naye mbali na kusiwe na mawasiliano ya kimapenzi kati yao,” alisema Alhad.
Kwa kusema hivyo, Shehe Alhad aliwagusa mastaa wa Bongo ambao
wanajulikana kuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini hufunga kila ufikapo
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya mastaa wasio kwenye ndoa lakini wamefunga mwezi huu
walizungumza na waandishi wetu ambapo walidai kutimiza masharti ya mwezi
huo kwa kutengana na wenzi wao, baadhi yao ni:-
Snura Mushi ambaye yupo katika uhusiano wa kimapenzi na Dj Hunter wa Maisha Club mkoani Mbeya, amesema:
“Mwenzangu yupo Mbeya hivyo tumetengana. Nilijiandaa miezi miwili
kabla kwa ajili ya kufunga mwezi huu. Huwa tunawasiliana tu kwa salamu
na mambo ya kawaida.”
Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ambaye pia yupo katika uhusiano na dogo
Mbongo Fleva, Nuhu Mziwanda naye amefunguka: “Naipenda sana dini yangu
ndiyo maana nimetengana na mwenzangu kwa sasa. Tunazungumza jioni tena
baada ya kufuturu.”
Rose Ndauka, yeye yupo kwenye uhusiano na mzazi mwenziye, Malick Bandawe:
“Yah mimi mwenyewe nimefunga na mwenzangu naye amefunga, tumetengana
mimi nimerudi kwa mama mpaka mwezi uishe. Huwa tunapigiana simu kwa
ajili ya kunijulia hali yangu na ya mtoto.”
Wema Sepetu hakupatikana
kwenye simu, lakini na yeye yupo kwenye uhusiano na Mbongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond’ wote wakiwa kwenye imani inayowataka kufunga
mwezi huu kama hawana matatizo ya kiafya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment