skip to main |
skip to sidebar
HUU NDIO UKWELI WA MAMBO YALIYOVYOKUWA KWENYE KIPINDI CHA XXL, AMBAPO UGOMVI WA DJ FETTY NA MCHOMVU ULITOKEA
Jumatano July 02 kupitia kipindi cha XXL zilisikika kelele za ugomvi
hewani ambazo asilimia kubwa tuliamini kuwa ni za kweli hasa kutokana na
baadhi yao kusikika kama wamekabwa huku wengine wakitaja majina ya
viongozi kuja studio kuamulia ugomvi huo.
kila mmoja kwa nafasi yake anatamani kujua chanzo hasa cha kugombana
lakini kupitia kipindi cha XXL leo July 04,wameeleza ukweli juu ya
kilichotokea na kusema hii wamefanya kwa ajili ya kampeni ambayo Clouds
Media Group wanaiendesha kwa sasa waliyoipa jina la Paza Sauti.
Kampeni
hii inalenga kuhamasisha utoaji wa taarifa ambazo unaziona mtaani kwako
kama haziko sawa kutoa taarifa hasa kwa vyombo vya dola ikiwemo Polisi
ili kwa pamoja tuidumishe amani tuliyonayo Tanzania,Paza Sauti,Ukimya
Hausaidii..
Bonyeza play kusikiliza maana halisi ya Paza sauti.
No comments:
Post a Comment