Mwanamuziki ambaye ni zao la Jumba la Vipaji Tanzania ‘THT’ Estalina
Sanga ‘Linah’ ameaga rasmi jumba hilo ambapo inadaiwa kwa sasa atakuwa
chini ya Kampuni ya No Fake Zone ‘NFZ’ inayoendesha shughuli zake nchini
Afrika Kusini.
Akizungumza na Ijumaa msemaji wa kampuni hiyo aliyewahi kushiriki
Shindano la Big Brother Africa 2003, Abergail Brigette Plaatjies ‘Abby’
alisema wamemchukuwa Linah ili kuendeleza kipaji chake kimataifa.
“THT imemlea vizuri Linah na kumfikisha hapa alipo sasa sisi kama NFZ
tumemchukua ili tuweze kumuingiza zaidi kwenye soko la kimataifa na kwa
kuanzia tumeanza kumtengenezea video ya wimbo wake mpya unaojulikana
kwa jina la Oleh Tembah,” alisema Abby.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment