HUU NDIO UKWELI KAMILI KUHUSU KIFO CHA DR SLAA

Kumeibuka baadhi ya jumbe fupi za maandishi (meseji) zilizosambaa mitandaoni zikisema kuwa Dk. Wilbroad Slaa amefariki dunia kutokana na ajali ya gari aliyoipata siku ya leo asubuhi na mapema.

Baadhi ya meseji hizo zilizosambaa zaidi katika mitandao ya kijamii zilisema,

"Roho ya marehemu Dk. Slaa ipumzike kwa amani”, “Bwana ametoa na Bwana ametwaa…”. Na nyingine ziliandikwa kama habari kabisa,

“Breaking news:
Dk. Slaa hatunaye tena! Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la taifa (TBC) Dk. Slaa amefariki dunia majira ya saa 3:25 asubuhi hii katika ajali mbaya ya gari iliyohusisha gari ndogo aina ya Rav 4 na basi la abiria. Dk. Slaa na dereva wake walifariki hapohapo.

Marehemu Dk.  Slaa ameacha mke na watoto watano. Roho ya marehemu ilale mahali pema peponi. Amina"

Taarifa kamili  na ya uhakika kabisa ni kuwa Dk. Slaa ni mzima wa afya na hajapata ajali yeyote. Pia TBC haijatoa taarifa kama hiyo kwani ni uzushi tuu. Tunachowaomba ni kupuuzia taarifa hizo za uongo!

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger