MAWIFI WAMKERA SANA CATHY

MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa anakerwa na tabia za mawifi kuwachukia wake za kaka zao bila sababu za msingi.
Msanii mkongwe wa filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’
Akichonga na paparazi wetu, Cathy alisema mawifi wengi huwachukia na kuwawekea vinyongo wake wa kaka zao hata kama hawajawakosea, kitu ambacho kinamkera na anaamini siyo yeye peke yake, bali jamii nzima inachukia tabia hizo.
“Ukweli nakerwa sana, yaani utakuta wanakuchukia bila sababu, muda mwingine wanakuwa na vinyongo mioyoni na kusema maneno yasiyofaa ya kukuponda, hawajui kwamba nao ni binadamu kama walivyo wao, naomba waache tabia hii, siyo nzuri,”alisema.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger