skip to main |
skip to sidebar
MSANII wa filamu ambaye
pia ni mweka hazina msaidizi wa klabu ya Bongo Movie Unity, Sabrina
Rupia ‘Cathy’ amefunguka kwamba anaona kundi hilo linakwenda kufa na
halitakuwepo kabisa kutokana na kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Steven
Mengere ‘Steve Nyerere’.
Msanii wa filamu Bongo Movie Unity, Sabrina Rupia ‘Cathy’.
Akistorisha na paparazi wetu, Cathy alisema amejisikia vibaya Steve
Nyerere kujiuzulu na wao kama viongozi hawakuwa na taarifa hivyo
kutokana na kwamba kiongozi huyo alikuwa mpiganaji Bongo Movie itakufa
kwani hakuna mtu anayeweza kuongoza kama Steve.
“Steve yeye kama binadamu ana mapungufu kidogo lakini mazuri
aliyofanya ni mengi kwani alikuwa mpenda maendeleo lakini kujiuzulu
kwake ni pigo na ninaona kama kundi hili halitakuwepo tena, yaani
ninajisikia vibaya sana na amejiuzulu ghafla mno,” alisema Cathy.
Read more >>
MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Sabrina Rupia
‘Cathy’ amefunguka kuwa anakerwa na tabia za mawifi kuwachukia wake za
kaka zao bila sababu za msingi.
Msanii mkongwe wa filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’
Akichonga na paparazi wetu, Cathy alisema mawifi wengi huwachukia na
kuwawekea vinyongo wake wa kaka zao hata kama hawajawakosea, kitu
ambacho kinamkera na anaamini siyo yeye peke yake, bali jamii nzima
inachukia tabia hizo.
“Ukweli nakerwa sana, yaani utakuta wanakuchukia bila sababu, muda
mwingine wanakuwa na vinyongo mioyoni na kusema maneno yasiyofaa ya
kukuponda, hawajui kwamba nao ni binadamu kama walivyo wao, naomba
waache tabia hii, siyo nzuri,”alisema.
Read more >>
MSANII maarufu katika tasnia ya filamu Bongo,
Sabrina Rupia ’Cathy’ amewataka wasanii wenzake kutofanya ustaa kwenye
ndoa zao kwani ndiyo chanzo cha kuvunjika kwa ndoa nyingi.
Msanii maarufu katika tasnia ya filamu Bongo, Sabrina Rupia ’Cathy’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Cathy alisema kabla ya kuolewa lazima
uwe na utayari wa kuolewa na kujuana kwa undani zaidi na mwenzio kabla
ya kufanya uamuzi pia usiweke neno kuachika katika ndoa kwa sababu tu
unaweza kupata mwingine.
“Uvumilivu ndiyo nguzo muhimu katika ndoa, unapojifanya staa na
kuishi maisha ya kistaa katika ndoa, mambo yanaharibika kabisa,” alisema
Cathy huku akikataa kutoa mifano ya walioachika kwa kuendekeza ustaa
katika ndoa akidai wanajijua.
Read more >>
TUNAMALIZIA makala haya ya Sabrina Rupia ‘Cathy’
tuliyoyaanza wiki tatu zilizopita, mwigizaji huyu alifunguka mambo mengi
kuhusiana na maisha yake, bila shaka kupitia mfululizo wa makala haya,
msomaji utakuwa umejifunza vitu vingi kutokana na hatua ambazo amepitia
maishani na leo hapa anafunguka kuhusu anavyofurahia maisha ya ndoa kwa
kuolewa na mume ambaye amemzidi umri SHUKA NAYO…
Msanii mkongwe katika fani ya maigizo Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’
Mwandishi: Kwa nini ulipenda mumeo akuzidi umri?
Cathy: Kwanza
nilipenda busara zake na namna anavyonilea kama mtu wake wa karibu, si
mtu wa mbwembwe kama walivyo wengine, namfurahia kwa sababu tunafanya
maisha ya kweli, lakini nilitaka kupata mwanaume mwenye huruma ambaye
hatoniumiza kama wafanyavyo vijana kwa sababu ya maisha ambayo
nimeyapitia ya kuwa mpweke baada ya kufiwa na baba yangu.
Mwandishi: Una watoto wangapi kwa sasa?
Cathy: Sipendi kutaja watoto ila fahamu ni mama wa familia.
Mwandishi: Je ndoa uliyonayo ni ya ngapi kwako?
Cathy: (Anatahamaki kidogo) We! Ndoa ya ngapi? Hii niliyonayo ni ya kwanza na mwisho!
Mwandishi: Vipi kuhusu mameneja wako katika kazi za uigizaji hawakusumbui suala la kukusimamia bila kuwapa tunda la mumeo.
Cathy: Hapana najitambua lakini pia najivunia kuwa mme wangu ndiye meneja wangu kwa hiyo tunda ni halali yale kabisa.
Mwandishi: Ni kweli Bongo Muvi hamko tayari kuwatoa wasanii wachanga?
Cathy: Kwa kifupi hela zinaenda kwa wenye hela, hata mimi naweza
kulalamika lakini nikipata nitachukua waliopata wenzangu na kuwaongezea
na wale wapambane kutoka.
Mwandishi: Kwa nini msibebane?
Cathy: Ninachojua cha msingi ni kufaiti unavyojua mwenyewe lakini
usikae kwa kumsubiri flani atoke ili akupe kiki hakuna mtu wa kukufanyia
hivyo.
Mwandishi: Duuh! Kwa hiyo kila msanii anatakiwa kujibeba kivyake?
Cathy: Nafasi huwezi kupewa cha msingi ni kupigana na kutafuta upenyo wa kutoka iwe kwenye muvi au nje ya sanaa.
Mwandishi: Mpaka sasa una filamu ngapi?
Cathy: Kama nne au tano, kuna DNA, Wheel Chair nilifanya na Cloud, Saa Nne, Kaburi na Simu ya Mkononi ambazo hazijatoka.
Mwandishi: Nini ushauri wako?
Cathy: Watu wasibweteka hasa kina dada watumie nguvu zao kufanya kazi
lakini pia wasanii wachanga wafaiti wenyewe wasisubiri kuolewa, kila
mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.
Mwandishi: Unazungumzije suala la ajira kwa vijana?
Cathy: Wanyanyuke waache uzembe kwani hata kilema anatamani japo
anyanyuke kwa dakika kadhaa ili atembee, asiye na mikono anatamani
angekua nayo ili imsaidie japo kulima sembuse wewe uliyekamilika
unashindwa kujisaidia mpaka usubiri kutolewa!
Mwisho.
Read more >>