KESI ya
ubakaji inayomkabili mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa
nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23
2014 katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo Mbasha amesomewa tena
mashataka yake huku akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa.Akisoma
hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, mwendesha mashtaka wa serikali
Nasoro Katunga alisema May 23 2014 mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye
Yerusalemu Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie
mtu yoyote ambapo wakati akitenda kosa hilo
mkewe Flora hakuwepo nyumbani.Katunga
aliendelea kufafanua kuwa May 25 2014 Mbasha alirudia tena kitendo cha
ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake
ambae hakuwepo nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha
alimbaka tena binti.Hizo sentensi zote mbili za juu Mbasha amezikana Mahakamani kwa kusema sio kweli.Hata
hivyo iliendelea kuelezwa kwamba tukio hilo la ubakaji liliripotiwa
katika kituo cha polisi Tabata ambako Boazi alipewa PF3 kwa ajili ya
kupata matibabu ambapo uchunguzi uliofanywa ulionyesha ni kweli binti
huyo aliingiliwa kimwili.
Katika
kesi hiyo ambayo Mbasha anatetewa na wakili Mathew Kakamba, Mbasha
alikubali sentensi mbili na kuzikataa mbili zilizobaki kwamba alimbaka
binti huyo.
Alichokubali
ni kusema ni kweli alimuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake
ambaye hakuwepo nyumbani na pia alikubali ni kweli Mei 23 2014 mke wake
Flora Mbasha hakuwepo nyumbani.
Baada
ya kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashataka wa serikali, Jaji
Luago aliahirisha kesi hiyo hadi August 22 2014 baada ya wakili
anayemtetea Mbasha kudai atakuwa na safari kwa siku za karibuni nje ya
Mkoa.
No comments:
Post a Comment