Showing posts with label MBASHA. Show all posts
Showing posts with label MBASHA. Show all posts

FRORA MBASHA ATOA UFAFANUZI KUHUSU MIMBA ALIYONAYO, SOMA ZAIDI HAPA

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ambae pia ni Mke wa Emmanuel Mbasha amefunguka na kusema kuwa hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na na Mchungaji wa Kanisa la kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima...

Flora amesema hayo leo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa Sita kamili.

Flora amesema kuwa hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu ambae ni ndugu yake hivyo Mchungaji Gwajima ni mjomba wake na si mpenzi wake kama ambavyo watu wamekuwa wakizusha kwa lengo la kumchafua na kumshushia hadhi.

"Hayo ni maneno tu ya watu mtaani ila Mchungaji Gwajima ni mtumishi wa Mungu na ni uncle wangu ninawezaje kuwa na mahusiano na uncle wangu..? " Alihoji Flora wakati akijibu  maswali ya mashabiki ambayo mengi yao yalikuwa yakimtuhumu na huku watu wengi wakitaka kujua ukweli juu ya ugomvi uliopo kati yake na Mumewe kama ni kweli au ni skendo tu za magazeti..

Flora aliweka wazi kuwa kuna vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na lengo la kumchafua na kumharibia sifa ndio maana walitumia gharama kubwa kufanya wanavyoweza ili kutimiza malengo yao.Amedai kuwa alimua kukaa kimya kwa kuwa hakukuwa na ukweli wowote.

"Hizo stori mnazosikia hazina ukweli wowote na ndio maana niliamua kukaa kimya, sikutaka kujibizana kwenye vyombo vya habari kwa uongo wa baadhi ya magazeti ya udaku ila ninasikitika sana kwani kuna watu wamekaa na kujipanga kisawa sawa kwa ajili ya kuhakikisha wanaharibu huduma yangu kwa gharama zozote...

"Lakini bado ninasonga mbele kwani mwanzilishi wa huduma yangu ni Mungu na huyo ndiye atakayeimaliza na sio mwanadamu. Hata hivyo ninawashukuru kwa kuwa wamenitabilia ntakuja kumiliki jumba na magari ya kifahari ingawa yote ni ubatili"

SIJAACHANA NA MBASHA KISA GWAJIMA
Flora Mbasha amesema kuwa watu wengi wanasema kuwa ameachana na Mumewe kisa Gwajima hilo swala halina ukweli wowote, hajaachana na Mbasha sababu ya Gwajima na amedai kuwa bado anampenda sana ila anampenda Mungu zaidi.

Amekiri kuwa na matatizo katika ndoa yake kati yake na mumewe lakini akasema kuwa  hayo ni matatizo yao ya ndani, hivyo asingependa kuyaweka wazi katika vyombo vya habari maana kufanya hivyo ni sawa na kumvunjia heshima mumewe maana mambo ya chumbani ni siri yao wenyewe.

"Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu"

Wakati anazungumzia suala hili Flora ameweka wazi kuwa kwa sasa ni mjamzito na ujauzito huo ni wa Mume wake ambae ni Emmanuel Mbasha maana ameishi nae katika ndoa zaidi ya miaka kumi na katika kipindi chote hicho hajawahi hata siku moja kumsaliti Mumewe na kwenda kwenye michepuko hivyo huo ujauzito ni wa Mume wake Emmanuel Mbasha na siyo Gwajima.
Read more >>

MDOGO WAKE FLORA MBASHA ASIMULIA KUBAKWA KWAKE NA MUME WA FLORA MBASHA, SOMA ZAIDI HAPA

Shahidi wa kwanza katika kesi ya kubaka inayomkabili mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha, ameieleza mahakama jinsi mshtakiwa alivyomkaba shingo na kumziba mdomo kwa kutumia nguo, kisha kumbaka.

Shahidi huyo ambaye ni shemeji yake, mwenye umri wa miaka 17, aliyasema hayo jana wakati akitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Hata hivyo, kesi hiyo ilisikilizwa kwa faragha(Chamber Cort) baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali Nassoro Katuga kuiomba mahakama kesi hiyo kuendeshwa kwa faragha kwa kuwa imefikia hatua ya kusikilizwa na sheria inaonyesha kuwa mtoto huyo yupo chini ya miaka 18.

Ombi hilo lilikubaliwa na pande zote mbili na kesi hiyo kuendeshwa katika mahakama ya faragha na Hakimu, Wilbaforce Luhwago aliomba watu wote walikuwepo ndani ya mahakama hiyo kutoka nje ili kupisha upande wa mashtaka kutoa ushahidi.

Akiongozwa na mwendesha Mashtaka wa Serikali Nassoro Katuga, shahidi huyo alidai siku ya tukio, Mei 23, mwaka huu, mshtakiwa aliondoka na mke wake kwenda kufuatilia mkanda wa video lakini ghafla alirudi nyumbani kwake Tabata Kimanga akiwa peke yake.

Alidai siku hiyo ya tukio mshtakiwa alifanikiwa kufanya mapenzi na binti huyo na kumwambia asimwambie mtu wakati mke wake akiwa hayupo nyumbani hapo.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12,2014.
Read more >>

MME WA FLORA MBASHA NA STAA HUYU BONGO MOVIE SIO SIRI TENA MAPENZI YAO

msanii wa bongo movie anaejulikana kwa jina la irene paul amepost picha akiwa na mume wa flora mbasha na kuzua minong'ono miongoni mwa mashabiki ambao wengi wameenda mbali na kudai kuwa wawili hao ni wapenzi kwa sasa, hata hivyo irene paul hakuweza kuwajibu mashabiki wake hvyo wengi kubaki njia panda
Read more >>

MBASHA AFUNGUKA MANENO HAYA MAHAKAMANI

KESI ya ubakaji inayomkabili mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23 2014 katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo Mbasha amesomewa tena mashataka yake huku akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa.Akisoma hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro Katunga alisema May 23 2014 mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye  Yerusalemu Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote ambapo wakati akitenda kosa hilo
mkewe Flora hakuwepo nyumbani.Katunga aliendelea kufafanua kuwa May 25 2014 Mbasha alirudia tena kitendo cha ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambae hakuwepo nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha alimbaka tena binti.Hizo sentensi zote mbili za juu Mbasha amezikana Mahakamani kwa kusema sio kweli.Hata hivyo iliendelea kuelezwa kwamba tukio hilo la ubakaji liliripotiwa katika kituo cha polisi Tabata ambako Boazi alipewa PF3 kwa ajili ya kupata matibabu ambapo uchunguzi uliofanywa ulionyesha ni kweli binti huyo aliingiliwa kimwili.
Katika kesi hiyo ambayo Mbasha anatetewa na wakili Mathew Kakamba, Mbasha alikubali sentensi mbili na kuzikataa mbili zilizobaki kwamba alimbaka binti huyo.
Alichokubali ni kusema ni kweli alimuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambaye hakuwepo nyumbani na pia alikubali ni kweli Mei 23 2014 mke wake Flora Mbasha hakuwepo nyumbani.
Baada ya kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashataka wa serikali, Jaji Luago aliahirisha kesi hiyo hadi August 22 2014 baada ya wakili anayemtetea Mbasha kudai atakuwa na safari kwa siku za karibuni nje ya Mkoa.
Read more >>

ISHU YA FLORA MBASHA KUNASA MIMBA, GWAJIMA AKIMBIA NCHI..!! WAUMINI SASA KUGAWANA MPAKA MBAO ZA KANISA



Kufuatia  sakata  la  Flora  Mbasha  na  mumewe  likumuhusisha  moja  moja  kiongozi  wa  kiroho  Mchungaji  Gwajima, habari  tulizozipata  ni  kwamba  mchungaji  huyo  amekimbia  nchi….

Habari  toka  chanzo  cha  kuaminika  kilichopo  ndani  ya  kanisa  la  mchungaji  huyo  ni  kuwa  Gwajima  hivi  sasa  ameshauza  karibia  robo  tatu  ya  mali  zake  na  kwamba  moja  kati  ya  magari  yake  ya  kifahari  huenda  likanunuliwa  na  mwanamuziki  Diamond.

“Jamaa  hivi  tunavyoongea  anaweza  akawa  ameshatoroka  tayari, maana  hili  sakata  limeanza  kumwendea  hovyo  na  wiki  iliyopita  kuna  madalali  walikuja  hapa  wakiitaka  gari  yake  aina  ya  Hammer, wakidai  kuwa  inataka  kununuliwa  na  mwanamuziki  Diamond,”  kilisema  chanzo  cha  habari  hii.


Kikaendelea  kumwaga  data  kuwa  karibu  wiki  zima  lililopita  mchungaji  huyo  alikuwa  kwenye  mipango ya  kuuza  baadhi  ya  nyumba  zake  na  kwamba  hata  familia  yake  hivi  sasa  haiko  kwenye   makazi  yake  anayoishi  siku  zote…

“Hata  familia  yake  sijaiona  karibu  wiki  mbili  hapa  kanisani  na  taarifa  tulizonazo  karibu  waumini  wengi  tu ni  kwamba  jamaa  anataka  kuhama  nchi  lakini  hatujui  ni nchi gani  anayotaka  kwenda  kufanya  makazi  yake  tena  ya  kudumu,” alisema.

Habari  hizo  zinadai  kuwa  baadhi  ya  waumini  wamepanga  kugawana  mali  kadhaa  za  kanisa  pamoja  na  za  Gwajima  mwenyewe  endapo  itagundukia  kuwa  ametoroka  kweli….

“Kuna  baadhi  ya  waumini  wamekerwa  sana  na  hii  skendo ya  Flora  Mbasha, wamekuwa  wakijiapiza  kwamba  hata  zile  mali  zake  ni  halali  yao  kwani  zinatokana  na  sadaka  wanazotoa  kila  siku, inasikitisha  sana  kwa  kweli.” alisema  mtoa  habai  hii.

Inasemekana  kuwa  mchungaji  Gwajima amepanga  kuwaaga  waumini  wake  kama  vile  anakwenda  kueneza  neno  katika mataifa  mengine, lakini  ukweli  ni  kwamba  anataka  kuondoka  ili  kukwepa  aibu  kutokana  na  mambo  yanayoendelea…
hummer
“Jamaa  yupo  kwenye  hali  ngumu, hii  ishu  ya  Flora  Mbasha imemuweka  katika  wakati  mgumu  sana  kwa  sababu  amekuwa  akinyooshewa  vidole  sana, na  kuna  baadhi  ya  wazee  wamekuwa  wakimtaka  atoe  tamko  rasmi  ili  kukwepa  hiki  kikombe  cha  aibu,” kilisema  chanzo  hicho.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima,
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima,
Read more >>

GWAJIMA ASHITAKIWA NA MBASHA

Mambo juu ya mambo! mvumo mkali wenye kuogofya unaendelea kutamalaki katika ndoa ya wanamuziki zao la upako wa Injili Bongo, Emmanuel na Flora Mbasha, safari hii ‘topiki’ siyo zile tuhuma za ubakaji zilizopo mahakamani.
Wanamuziki zao la upako wa Injili Bongo, Emmanuel na Flora Mbasha,
Mbeba ‘niuzi’ wa awamu hii ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, baada ya Mbasha kuona isiwe tabu, hivyo kuamua kupambana na mtumishi huyo wa Mungu kwa njia ya kiroho zaidi. 
Mbasha baada ya kulieleza gazeti mama la hili, Uwazi lililoandika habari yenye kichwa “Mbasha: Gwajima Niachie Mke Wangu”, akiidadavua dhana yake kwamba hapendi ufadhili wa Gwajima kwa mkewe, yaani Flora sasa ameamua kwenda mbele zaidi.
Habari zinadai kuwa, mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Mkoa wa Dar es Salaam, Bruno Mwakibolwa ambalo Gwajima ni memba hai, ameshapokea mashitaka kuhusu mchungaji huyo kuhusika kuitikisa ndoa ya waimbaji hao wa Neno la Mungu na mlalamikaji ni Mbasha mwenyewe.
Wikiendi iliyopita, Mbasha aliketi na kiongozi huyo na kushusha tuhuma zake dhidi ya Gwajima kama zilivyothibitishwa na mlalamikaji mwenyewe, nazo ni hizi zifuatazo;
MOSI; Gwajima ni kiongozi wa kiimani wa Mbasha na Flora lakini tangu matatizo ya ndoa yao yalipojitokeza, mchunga kondoo huyo wa Bwana hajawahi kufanya lolote kunusuru muunganiko huo uliohalalishwa kwa jina la aliye juu.


Emmanuel Mbasha
PILI; Gwajima anajua kila kitu kuhusu mgogoro wa Mbasha na mkewe lakini kipindi chote cha matatizo, Kanisa la Ufufuo na Uzima limekuwa mfadhili wa Flora kwa sehemu kubwa. Hapa anauliza, huu ufadhili una kipi nyuma yake?
TATU; Gwajima anatambua kuwa Flora ni mke wa mtu, mwenye mali ameshaomba aachiwe mwandani wake bila mafanikio. King’ang’anizi kina msukumo upi?
NNE; Gwajima amekuwa akimuumiza Mbasha kihisia, kiakili na kiroho kwa sababu yeye anagombana na mkewe lakini mchungaji huyo bila kufikiria maumivu aliyonayo, humwita Flora madhabahuni katika ibada na kumpa nafasi ya kuimba.

TANO; Flora anaishi hotelini na yeye mwenyewe alishakiri kuwa fedha za kulipia hoteli alizipata kutokana na michango ya waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima. Hapa Mbasha analalamika, inakuwaje kanisa limfadhili mke wa mtu kuishi hotelini ikiwa mumewe hajui?
SITA; Katika hoja zote hizo, Mbasha amelieleza Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste kuwa hana imani na Gwajima kwa vile kama ni busara baada ya kuona ndoa hiyo imetikisika yeye (Gwajima) angekaa pembeni kwa namna yoyote ile, hivyo Mbasha akaiomba menejimenti ya baraza hilo kumpa adhabu kali mwenzao.
Mbasha alipozungumza na Amani, Jumanne iliyopita, alisema baraza hilo liliahidi kushughulikia shauri lake na uamuzi utachukuliwa baada ya kumwita Gwajima na kumsikiliza kwa upande wake.
WENYE KWENU KWAHERI!
Kesi ya Mbasha kudaiwa kumbaka shemeji yake ilipoanza, mume huyo wa Flora alikimbilia mafichoni, kwa hiyo swali kwamba anaabudu kwenye kanisa gani halikuwa na mashiko kwa sababu mhusika mwenyewe hakuwa akionekana.

Baada ya Mbasha kujitokeza na kufikishwa mahakamani, kupelekwa mahabusu kwenye Gereza la Keko kabla ya kuachiwa kwa dhamana, ndipo swali kuwa anaabudu kanisa gani lilipoanza kutokana na ukweli kuwa yupo uraiani kwa ‘bondi’.
Swali hilo lilitokana na hoja kwamba kabla ya mgogoro na mkewe walikuwa wakisali kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Gwajima ambaye alishamtuhumu kumfadhili Flora na akamtaka amwachie ‘waubani’ wake huyo ili maisha yaendelee.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima,
Jawabu la swali hilo, lilijibiwa Jumapili iliyopita baada ya Mbasha kutinga Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), maarufu kama Mito ya Baraka, linaloongozwa na Mchungaji Bruno Mwakibolwa, na kukamilisha haja zake za kuabudu pale.
Mbasha alipozungumza na Amani kuhusu kusali kwa Mchungaji Mwakibolwa badala ya kwa Gwajima, alijibu: “Nimehama Kanisa la Ufufuo na Uzima, sisali tena kule. Kuanzia sasa shughuli zangu za kuabudu nitazifanyia Mito ya Baraka kwa Mchungaji Mwakibolwa.
“Siwezi kwenda kwa Gwajima kwa sababu simuelewi na ndiyo maana nimeamua kumshtaki kwa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste. Roho yangu ya kuabudu isingekuwa timilifu, ingejaa mashaka kwenda sehemu ambayo imenijeruhi na nisiyoiamini.
“Kwa kifupi si kwamba nimeanza kuabudu Mito ya Baraka hili ndilo kanisa letu tangu zamani, mimi na mke wangu. Tulihamia Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya Gwajima kutushawishi, kwa hiyo nimerejea kundini.
MCHUNGAJI MWAKIBOLWA
Juzi, Amani lilimsaka Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Mwakibolwa lakini simu yake ilipokelewa na kusikika sauti za watu wakiwa kwenye maombi kama si ibada.

GWAJIMA
Baada ya hapo, Amani lilimsaka Mchungaji Gwajima kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini yeye hakupokea hata pale alipopigiwa kwa kurudiarudia.

KESI YA MBASHA
Kesi ya Mbasha kudaiwa kubaka itatajwa tena Julai 17, mwaka huu kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

VIPI KUHUSU KUPATANA?
Wiki iliyopita katika Gazeti la Risasi Jumamosi kuliandikwa habari yenye kichwa; MBASHA, FLORA WAPATANA. Katika habari hiyo ilidaiwa wawili hao walipatana lakini walibakiza kikao kimoja cha kumalizia taratibu zote.

Habari zinasema, taratibu hizo zinandelea licha ya Mbasha kumshitaki Gwajima kwenye Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Mkoa wa Dar es Salaam.   
Read more >>

BARUA YA WAZI KUTOKA KWA MUME WA FLORA MBASHA KWENDA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA

"MCHUNGAJI ...YAPATA KAMA WIKI MBILI ZILIZOPITA NILIHOJI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI JUU YA ‘UTAJIRI' WA GHAFLA WA MKEWANGU MARA BAADA YA MGOGORO KUTOKEA KATI YANGU NA YEYE, BILA KUPOTEZA MUDA MKEWANGU AKANIJIBU KUPITIA GAZETI MOJA LA UDAKU KUWA AMECHANGIWA FEDHA KIASI CHA MILIONI 9 NA WAUMINI KANISANI KWAKO.

Mchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!

Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??

Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??

Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!

Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!!

Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!

Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!

Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!

Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!

Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!

Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda

Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!

Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe

Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu??

Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!

Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!

Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!! 
Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!

Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!

Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!

Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!

Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!

Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!

Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda.."
Read more >>

HATIMAYE MBASHA NA MUMEWE WAPATANA, HII NDIO SABABU YA WAO KUPATANA

HAKUNA neno zuri la kusema zaidi ya Mungu mkubwa! Ule mtafaruku ndani ya ndoa ya mwimba Injili mahiri Bongo, Flora na mumewe, Emmanuel Mbasha umedaiwa kumalizika kwa wawili hao kupatana, Risasi Jumamosi linakuwa nambari wani kukuhabarisha.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, wawili hao walikalishwa kikao cha upatanishi mapema wiki hii kilichokuwa chini ya familia.
Mume wa Flora Mbasha, Bw. Emmanuel Mbasha.
MANENO YA CHANZO
“Kikao cha familia kilikaa, Mbasha aliitwa akafika, Flora naye aliitwa akatokea, mazungumzo yalikuwa marefu lakini kimsingi waliamua kuweka kando mtafaruku wao na kuijenga upya ndoa yao,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliongeza kuwa katika kikao hicho cha mwanzoni mwa wiki hii, miongoni mwa adidu za rejea ilikuwa kutokumbushia vikao vilivyopita ambapo hakukupatikana muafaka.
VIKAO VILIVYOPITA
Katika vikao vilivyopita, wahusika wakuu walikuwa wazazi wa Mbasha (mzee Maneno Mbasha, Zulfa Maneno), ndugu wa Flora na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Mwimbaji Injili mahiri Bongo, Flora Mbasha.
VIKAO VYA BAADAYE
Kwa mujibu wa chanzo, vikao vilivyofuata, wawili hao wakawa tayari kila mmoja ametema nyongo yake pembeni na kufikia makubaliano kwamba, ndoa yao isimame tena wakitumia maandiko kwenye Biblia kutoka kitabu cha Waebrania yanayosema:    Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
WAKORINTHO YAFUNGA KAZI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, maneno mengine ya Biblia yaliyotumika kwenye kikao hicho mpaka wawili hao wakaamua kurudiana ni 1 Wakorintho 7:1-10 ambapo maandiko yanasema:
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
Flora Mbasha akiwa kwenye picha ya pamoja na mumewe, Emmanuel Mbasha.
Mke hana amri juu ya mwili wake bali mumewe vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe. Msinyimane, isipokuwa mmepatana kwa muda ili mpate faragha kwa kusali, mkajiane tena shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza, wala hapo si mimi, ila Bwana (Mungu), mke asiachane na mumewe, lakini ikiwa ameachana naye na akae asiolewe au apatane na mumewe, tena mume asimwache mkewe.
KIKAO CHA JUMAMOSI KUMALIZIA
Chanzo kilisema kuwa, kikao cha mwisho ambacho kitamalizia kuweka mambo sawa ili wawili hao waanze ngwe ya pili ya ndoa yao ambayo inaaminika itakuwa ya mwisho mpaka kifo kiwatenganishe, kinatarajiwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam mahali ambapo hapakutajwa.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
MWANASHERIA ATAJWA
Mwanasheria wa Flora aliyejulikana kwa jina moja la Ado ametajwa kusimamia kikao hicho ili wawili hao waanze maisha mapya baada ya safari fupi ya mvurugano uliowafanya kuwa mbalimbali.
AONGEA NA RISASI JUMAMOSI
Juzi, Risasi Jumamosi lilimsaka mwanasheria huyo kwa njia ya simu yake ya mkononi ili kumsikia anasemaje kuhusu kutajwa kwenye usuluhishi wa ndoa hiyo ambapo alipopatikana alisema:
“Niko Arusha, Ijumaa nitarudi Dar. Kuhusu kikao cha usuluhishi siwezi kukwambia lakini suala la kuwapatanisha nalifahamu, nawaomba na ninyi msaidie kufanikisha jambo hilo zuri.”
VIPI KUHUSU KESI YA MADAI YA KUBAKA?
Hata hivyo, Wakili Ado hakutaka kugusia kuhusu kesi ya Mbasha iliyopo Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo anadaiwa kumbaka shemejiye mara mbili (jina tunalo) ambayo kwa mujibu wa mahakama, upelelezi umekamilika na itasikilizwa Julai 17, mwaka huu.
KWA UPANDE WAKE FLORA
Risasi Jumamosi lilimwendea hewani, Flora ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa upatanishi kati yake na mumewe, Emmanuel.
Huyu hapa: “Ongea na wakili wangu atakwambia kila kitu.” Ambapo majibu ya wakili yalikuwa: ”Ninachojua mimi ni kwamba Flora ameshamsamehe mumewe na yuko tayari kuanza ukurasa mpya.”
MBASHA SASA
Kwa upande wake, Mbasha alipozungumza na gazeti hili juzi alisema kurejea upya kwa ndoa yake ni jambo la kuupendeza moyo wake.
“Mimi sina neno nipo tayari, nimeshasamehe yaliyotokea, Flora ni mke wangu jamani, nampenda sana kutoka moyoni.”
Read more >>

UKWELI KAMILI WA FLORA MBASHA

MIMI ni mkristo wa dhehebu la Roma. Mafundisho mengi tunayopewa kuanzia Ubatizo, Komunyo ya Kwanza na Kipaimara, tunafundishwa kuhusu kutenda mema, kupendana wenyewe kwa wenyewe na hata kuwapenda maadui zetu.
Tunaambiwa, akija mtu akakupiga kofi shavu lako la  kushoto, wala hata usimrudishie, bali mgeuzie na upande ule wa kulia na akishakutundika hivyo vibao vyake, muombe Mwenyezi Mungu amsamehe. Tunafundishwa kusamehe, ndiyo maana katika moja ya maandiko yaliyo katika vitabu vya dini, kama Injili na Biblia, kuna mistari inayosema samehe saba mara sabini. 
Kwa wale ndugu zangu wasio wakristo, nitaomba niwaombe radhi kwa kuanza na utangulizi huu. Ni kwa sababu leo nazungumza na mtu ambaye wengi wetu tunaamini ni mtumishi wa Mungu. Mtu yeyote anayesambaza neno la Mungu, huwa ni mtumishi wake. Neno zuri la Mungu husambazwa kupitia mihadhara, misa, maombi na hata nyimbo kama Flora Mbasha anavyofanya. 
Leo nikiambiwa niwataje waimbaji wa Injili kumi bora nchini, jina la Flora Mbasha litakuwa katikati yao, likigawa kundi moja juu yake na lingine chini yake. Hii ni kwa sababu ni mmoja wa waimbaji wazuri wa muziki huu. Hujisikia furaha ninaposikiliza ujumbe uliomo katika nyimbo zao, ingawa baadhi ya kazi zake huchezeka, lakini ujumbe wake maridhawa hubakia kuwa fumbo. 
Familia ya watu wa muziki wa Injili nchini, imepata mshtuko mkubwa wiki chache zilizopita, baada ya waimbaji, ambao ni wanandoa, Emmanuel na Flora Mbasha kupamba vichwa vya habari baada ya kutokea mzozo wa kifamilia kati yao, ambao unadaiwa kusababisha mwanaume kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za ubakaji. 
Sitaki kuzungumzia suala lililopo kortini kwa sababu sheria zinakataza, isipokuwa nataka kuzungumza na mdogo wangu Flora kwa sababu alichokifanya katika kipindi chote cha mtafaruku baina yao, hakikupaswa kufanywa naye hasa kwa jinsi alivyofanikiwa kujitengenezea taswira ya kuheshimika mbele ya jamii. 
Huwa najaribu kusema mara nyingi, ustaa ambao baadhi yetu hatulali kwa kuutafuta una gharama kubwa. Ukishakuwa mtu maarufu, unajinyima baadhi ya haki zako za msingi, kama vile masuala yako binafsi kubaki kuwa ya kwako. 
Ninafahamu Flora, kama mke ana haki ya kukataa baadhi ya mambo kufanyika katika ndoa yake. Sisi tulio katika ndoa tunafahamu, kuna maisha magumu kweli, wakati mwingine mume na mke huweza kukaa hata mwezi mzima bila kuzungumza, lakini kwa sababu ya kuhifadhi matatizo yenu yasitoke nje, mnakaa kimya.  
Akija jirani, hawezi kujua kama hamzungumzi kwa namna mtakavyompokea kwa bashasha na kumpa ushirikiano. 
Kama kukaa kimya ili mambo hayo yaishe yenyewe kimyakimya mnashindwa, kinachotokea ni kuwafuata ndugu wa karibu, ambao mara nyingi huwa ni wale waliowazidi umri. Mnapeleka tatizo lenu, mnaitwa, mnajadiliana kwa pamoja, mnaondoka na muafaka! 
Haya mambo yangeweza kufanywa na Flora, hasa kwa kuwa jamii inamtambua kama mtu mwenye woga na Mungu. Sasa kama mtu anayetakiwa kuwa mfano, anaondoka nyumbani kwake na kwenda kusikojulikana, tena wakati mumewe akiwa katika matatizo, unataka watu wakutazame kwa macho yapi?  
 
itaki kusema nani mwenye makosa kati yao, ninachotaka kusema ni kitendo cha Flora kuifanya jamii ione ni kama anayefurahia matatizo yanayomzonga mumewe. Hii siyo sawa, hata kama ndani hatuongei, nje sisi ni kitu kimoja. 
Wakati akiwa madarakani, Rais wa Marekani, Bill Clinton aliwahi kukutwa na tuhuma za kumbaka mfanyakazi wa Ikulu, Monica Lewinsky. Katika kipindi chote cha sakata hilo, mkewe Hilary, alikuwa upande wake, hakumuacha, alikuwa tayari kufa naye, kuliko kuongeza petrol kwenye moto. Nani anajua waliishije wakiwa chumbani kwao? 
Flora anatakiwa kutambua kuwa kuna ndoa chache sana zinaishi kwa upendo kama tunavyoziona. Kitu kikubwa tunachopaswa kufanya, hasa kwa mastaa ni kuzilinda ndoa zetu kwa mikono yetu wenyewe.
Read more >>

FLORA MBASHA, JITAHIDI KUKUMBUKA MAANDIKO!

MIMI ni mkristo wa dhehebu la Roma. Mafundisho mengi tunayopewa kuanzia Ubatizo, Komunyo ya Kwanza na Kipaimara, tunafundishwa kuhusu kutenda mema, kupendana wenyewe kwa wenyewe na hata kuwapenda maadui zetu.
Tunaambiwa, akija mtu akakupiga kofi shavu lako la  kushoto, wala hata usimrudishie, bali mgeuzie na upande ule wa kulia na akishakutundika hivyo vibao vyake, muombe Mwenyezi Mungu amsamehe. Tunafundishwa kusamehe, ndiyo maana katika moja ya maandiko yaliyo katika vitabu vya dini, kama Injili na Biblia, kuna mistari inayosema samehe saba mara sabini.
Kwa wale ndugu zangu wasio wakristo, nitaomba niwaombe radhi kwa kuanza na utangulizi huu. Ni kwa sababu leo nazungumza na mtu ambaye wengi wetu tunaamini ni mtumishi wa Mungu. Mtu yeyote anayesambaza neno la Mungu, huwa ni mtumishi wake. Neno zuri la Mungu husambazwa kupitia mihadhara, misa, maombi na hata nyimbo kama Flora Mbasha anavyofanya.
Leo nikiambiwa niwataje waimbaji wa Injili kumi bora nchini, jina la Flora Mbasha litakuwa katikati yao, likigawa kundi moja juu yake na lingine chini yake. Hii ni kwa sababu ni mmoja wa waimbaji wazuri wa muziki huu. Hujisikia furaha ninaposikiliza ujumbe uliomo katika nyimbo zao, ingawa baadhi ya kazi zake huchezeka, lakini ujumbe wake maridhawa hubakia kuwa fumbo.
Familia ya watu wa muziki wa Injili nchini, imepata mshtuko mkubwa wiki chache zilizopita, baada ya waimbaji, ambao ni wanandoa, Emmanuel na Flora Mbasha kupamba vichwa vya habari baada ya kutokea mzozo wa kifamilia kati yao, ambao unadaiwa kusababisha mwanaume kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za ubakaji.
Sitaki kuzungumzia suala lililopo kortini kwa sababu sheria zinakataza, isipokuwa nataka kuzungumza na mdogo wangu Flora kwa sababu alichokifanya katika kipindi chote cha mtafaruku baina yao, hakikupaswa kufanywa naye hasa kwa jinsi alivyofanikiwa kujitengenezea taswira ya kuheshimika mbele ya jamii.
Huwa najaribu kusema mara nyingi, ustaa ambao baadhi yetu hatulali kwa kuutafuta una gharama kubwa. Ukishakuwa mtu maarufu, unajinyima baadhi ya haki zako za msingi, kama vile masuala yako binafsi kubaki kuwa ya kwako.
Ninafahamu Flora, kama mke ana haki ya kukataa baadhi ya mambo kufanyika katika ndoa yake. Sisi tulio katika ndoa tunafahamu, kuna maisha magumu kweli, wakati mwingine mume na mke huweza kukaa hata mwezi mzima bila kuzungumza, lakini kwa sababu ya kuhifadhi matatizo yenu yasitoke nje, mnakaa kimya.
Akija jirani, hawezi kujua kama hamzungumzi kwa namna mtakavyompokea kwa bashasha na kumpa ushirikiano.
Kama kukaa kimya ili mambo hayo yaishe yenyewe kimyakimya mnashindwa, kinachotokea ni kuwafuata ndugu wa karibu, ambao mara nyingi huwa ni wale waliowazidi umri. Mnapeleka tatizo lenu, mnaitwa, mnajadiliana kwa pamoja, mnaondoka na muafaka!
Haya mambo yangeweza kufanywa na Flora, hasa kwa kuwa jamii inamtambua kama mtu mwenye woga na Mungu. Sasa kama mtu anayetakiwa kuwa mfano, anaondoka nyumbani kwake na kwenda kusikojulikana, tena wakati mumewe akiwa katika matatizo, unataka watu wakutazame kwa macho yapi?
Sitaki kusema nani mwenye makosa kati yao, ninachotaka kusema ni kitendo cha Flora kuifanya jamii ione ni kama anayefurahia matatizo yanayomzonga mumewe. Hii siyo sawa, hata kama ndani hatuongei, nje sisi ni kitu kimoja.
Wakati akiwa madarakani, Rais wa Marekani, Bill Clinton aliwahi kukutwa na tuhuma za kumbaka mfanyakazi wa Ikulu, Monica Lewinsky. Katika kipindi chote cha sakata hilo, mkewe Hilary, alikuwa upande wake, hakumuacha, alikuwa tayari kufa naye, kuliko kuongeza petrol kwenye moto. Nani anajua waliishije wakiwa chumbani kwao?
Flora anatakiwa kutambua kuwa kuna ndoa chache sana zinaishi kwa upendo kama tunavyoziona.
Kitu kikubwa tunachopaswa kufanya, hasa kwa mastaa ni kuzilinda ndoa zetu kwa mikono yetu wenyewe.
Read more >>

MAPYA YALOIBUKA KWA FLORA MBASHA NA MUMEWE, YASOME HAPA

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Bongo Flora Mbasha.
HABARI zilizotua kwenye meza ya Uwazi juzi zinadai kuwa familia mbili, ya Emmanuel na Flora Mbasha zimeweka kikao kwa siku tatu mfululizo kutaka kuinusuru ndoa ya wawili hao lakini imeshindikana huku pembeni ikidaiwa kwamba ili mambo yakae sawa lazima Mbasha alipe shilingi milioni 60.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kikao hicho kiliitishwa na baba wa Mbasha kwa kushirikiana na ndugu wengine wa pande zote mbili.
“Mbasha na mke wake, Flora walikutanishwa sehemu fulani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatanishwa. Kikao kilikuwa kizito, wakubwa wa familia zote walikuwepo lakini Flora alikataa mara tano kurudi kwenye ndoa yake. 

UWAZI LAPIGA HODI NYUMBANI KWA MBASHA
Juzi Jumapili, Uwazi lilitia timu nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga jijini Dar na kubahatika kuzungumza na baba na mama wa Mbasha bila kumpata Mbasha mwenyewe.
 


Mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Maneno alikiri kuwepo kwa kikao kwa muda wa siku tatu tofauti lakini akasema mambo yalishindikana. 

“Mimi nilikuja Dar kutokea Dodoma wiki moja iliyopita baada ya kupata wito wa mwanangu kuhusu mgogoro wa ndoa. Nilipofika hapa, sikumkuta Flora, nyumba ilikuwa tupu. 

“Kikao kiliitishwa na pande zote mbili, akiwemo Mchungaji Gwajima ambaye alionekana kusuluhisha mgogoro wao lakini dalili za Flora hazikuonesha kuwa tayari kurudi kwenye ndoa yake,” alisema mzee huyo.
Emmanuel Mbasha.
KUNA MKONO WA MTU
Mzee Maneno aliendelea kusema: “Mimi kama mtu mzima, nilichokiona katika ndoa ya mwanangu kuna mkono wa mtu. Ila sasa ametumia mbinu kubwa sana kumrubuni Flora na yeye kakubali kurubunika.”
 


MAMA MZAZI NAYE
Kwa upande wake, mama mzazi wa Mbasha, Zulfa Maneno alisema kwake ni masikitiko makubwa kwa sababu mtoto wake alishakuwa na jina kubwa kimataifa na mkewe pia.

Alisema: “Mimi kwenye kikao nilipomwona Flora anakataa ndoa yake mara tano, kila akiulizwa anasema hataki kurudi mpaka mara tano, nikajua hakuna ndoa. 

“Ninachojua, mgogoro huo wa ndoa ulitengenezwa kwa makusudi kabisa ili ndoa ivunjike. Ila kama aliamua kumwacha mwanangu angefanya hivyo kwa amani na si visa kama hivi.”
Kuhusu kutakiwa shilingi milioni sitini ili Flora arejee kwenye ndoa yake, wazazi hao walisema hawajui kitu labda kama yanasemwa pembeni.

Baba mzazi wa Emmanuel Mbasha.
KULIKUWA NA MGOGORO
Habari zaidi zinadai kwamba, fedha zinazotakiwa kulipwa ni kwa sababu, ndoa hiyo ilikumbwa na mgogoro kabla ya kuibuka kwa madai ya Mbasha kumbaka shemeji yake.

Flora aliwahi kufungukia hilo kwamba, kabla ya kutokea kwa madai ya ubakaji, alitibuana na Mbasha na akaamua kuondoka nyumbani kwenda kuishi hotelini.  

DALILI MBAYA
Kuna madai kwamba, siku ambayo Mbasha alikwenda kujisalimisha polisi (Juni 16, 2014), Flora alipigiwa simu kujulishwa lakini hakutokea kituoni.
 


Ikazidi kuelezwa kwamba, siku Mbasha anapelekwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar kujibu madai ya ubakaji, pia Flora alijulishwa lakini hakutokea mahakamani hapo. 

Mbali na kupelekwa mahakamani, habari za uhakika zinasema hata pale Mbasha alipokosa dhamana na kupelekwa kwenye Gereza la Keko, Flora alijulishwa, lakini hakufanya lolote.
“Je, kwa hayo yote ni kweli Flora anaipenda ndoa yake? Si jibu lipo wazi kwamba  hakuna ndoa.” alisema mtu mmoja aliye karibu na familia hiyo.
Mama mzazi wa Emmanuel Mbasha
MBASHA BAADA YA KUTOKA JELA
Ushahidi wa majirani umeweka bayana kwamba, Mbasha alipotoka gerezani na kufika nyumbani kwake, Tabata-Kimanga, Dar, walimfuata na kuangua kilio mbele yake huku wakimpa pole kwa mkasa mzima.
 


Baadhi ya majirani waliozungumza na Uwazi juzi, walisema kuwa siku hiyo nyumbani kwa Mbasha kulikuwa na dalili zote za kuwepo kwa msiba kwani vilio vilitawala. 

MADAI
Mbasha, alipandishwa mahakamani Juni 17, mwaka huu kwa madai ya kumbaka mara mbili shemeji yake (jina tunalo).

Siku hiyo alikosa dhamana na kupelekwa Gereza la Keko ambapo Alhamisi ya Juni 19, mwaka huu alirudishwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya dhamana. Kesi yake itaanza kusikilizwa Julai 17, mwaka huu huku ikielezwa kuwa upelelezi umekamilika.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger