
Shuhuda
mmoja jina kapuni akiri kumuona mzee huyo akiwa na `PF3′ akitembea kwa
shida huku mkono wake ukiwa umevimba akipatiwa matibabu katika moja ya
zahanati ya wilayani hapo

Mbunge huyo amefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na ulevi huo na kupelekea kumpa kichapo kilichosababisha kuteguka kwa mkono sanjari na kumtupia nguo zake nje na hatimaye mzee huyo kukimbilia kwa Balozi wa nyumba kumi Dickson Joaqim kwa msaada wa kisheria.Awali Julai ,15, 2014 usiku mzee alichelewa kurudi nyumbani na alipomgongea mwanae afungue mlango ndipo akapata kichapo kutoka kwa mbunge huyo baada ya kuona adha hiyo ni sugu kwa mzee wake.Akiongea kwa njia ya simu na mtandao huu mbunge huyo alisema mzazi wake anapenda kunywa pombe kupindukia hali inayomfanya kila wakati wagombane juu ya tabia hiyo ambapo kwa upande wa pili kisiasa inamuathiri katika uwajibikaji wake kwa wananchi.Alisema baba yake anatumiwa na chama cha ccm kwa lengo la kumdhoofisha kisiasa hasa katika kipindi hiki cha majeruhi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwakani na kumtaja balozi wa mtaa wa mwilavya Dickson Joaqim ni miongoni mwa watu wanaomshawishi mzee wake kituo cha polisi kumshtaki.“sijafikia hatua ya kumpiga mzee wangu,najitambua ndio maana namsihi baba achane na pombe ambapo mimi najiskia vibaya kuona analewa sasa tukiwekana sawa baadhi ya watu wanadai nampangia sheria na ndo hivyo wanazusha ya kuzusha” alibainisha Machali.Alisema kwa kuthibitisha hilo umma kuwa hajampiga mzee wake na kwenye mkutano wa hadhara wilayani hapo, atakuwa sambamba na mzee huyo na kukiri mzee wake amefuta kesi dhidi yake na kusisitiza ccm watumie mbinu za ziada na kudai hawana jipya.
No comments:
Post a Comment