SAGUDA NAYE ATESWA NA MZIMU WA RECHO

Stori: Erick Evarist
WAKATI Arobaini ikitarajia kufanyika jana, mchumba wa marehemu Sheila Haule ‘Recho’, George Saguda ameeleza kuwa bado aliyekuwa mchumba wake huyo anamtesa kwa kumtokea mara kwa mara.
Marehemu Sheila Haule ‘Recho’, akiwa na mpenzi wake George Saguda enzi za uhai wake.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Saguda alisema marehemu amekuwa akimtokea akiwa usingizini na kumsisitiza kuhusu kazi.“Najitahidi sana kuondoa mawazo juu yake lakini bado ananitokea, sijui hali hii itaisha lini,” alisema Saguda.
Recho kabla hajapatwa na umauti, walizalisha filamu mbili katika kampuni yao ya Sara Entertainment ambazo ni Vanessa na Fedheha ambayo imetoka hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger