MFUNGO WAMBADILI JOHARI KWA KUFAA MAVAZI YA KIHESHIMA, MUONE HAPA

MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema amewaunga mkono Waislamu kwa kuvaa mavazi ya kujistiri na kuziba sehemu kubwa ya mwili kuheshimu mwezi wa Ramadhani.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Johari alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu dini zote ni za Mungu na kwa kuwa ni kipindi cha Ramadhani, amebadilika kwa kila kitu.
“Kipindi hiki ni cha kumrudia Mungu, nimeacha kila kitu kibaya kwa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na nimeamua kutulia ili nipate muda mwingi wa kuomba,” alisema Johari.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger