Mimi nakukubali sana Sandra, kwanza nakupa hongera kwa kazi zako
nzuri, ila nakupa tahadhari, jitahidi hivyohivyo kuwa na msimamo wa
kutopata skendo, vinginevyo utajiharibia katika sanaa pia jamaa
atakumwaga kwani utapoteza sifa. Selemani Alifa, Dar, 0718803204
SANDRA: Asante, nitajitahidi.
UCHUMBA
Sandra nakuzimia sana jinsi ulivyo na
umbo zuri, naomba uwe mchumba wangu wa kuniliwaza kimapenzi. Salim
Liundi, Dar, 0659601205
SANDRA: Utanisamehe, nimeshaolewa, siwezi kuwa tena mpenzi wako.
MAFANIKIO
Nakukubali sana Sandra ila nataka
kujua ni mafanikio gani uliyoyapata kutokana na tasnia hii ya uigizaji?
Amiri Salumu, Dar, 0653252416
SANDRA: Mafanikio nimepata mengi sana
kubwa zaidi nimeweza kufahamiana na watu wengi. Nimepata mume kupitia
sanaa na mengine mengi ambayo siwezi kuyataja kwa sasa ila mashabiki
wangu watayaona.
ELIMU YA SANAA
Dada Sandra bila shaka kipaji
unacho lakini je, kuhusu elimu ya sanaa unajiendeleza au unategemea
kipaji tu? Rama Nuru, Dar, 0682885844
SANDRA: Napenda sana kujiendeleza kielimu lakini bado sijapata fursa zaidi ila nimesoma kozi fupifupi za sanaa.
SWALI
Hivi mumeo bado uko naye na mna watoto wangapi? Vipi mumeo anapendezwa na kazi yako ya sanaa? Muddy Madley, 0652672805
SANDRA: Mume wangu nipo naye, tuna watoto wawili na mume wangu anapendezwa na kazi yangu kwa sababu alinikuta kwenye sanaa.
HISTORIA
Mimi ningependa kujua historia yako kwa ufupi. Neema, Dar, 0717579055
SANDARA: Nimezaliwa Shinyanga, nina elimu ya kidato cha nne pia
nimesomea usekretari katika Chuo cha Magogoni, Dar. Nilianza sanaa mwaka
2002 katika Kundi la Kaole.
NDOA
Dada Salma mimi napenda sana kazi yako ila
nakushauri kuichunga na kuilinda ndoa yako kwani heshima ya mwanamke ni
ndoa, Mungu akujalie upeo zaidi. Emmanuel George, 0765171432
SANDRA: Asante nami naipenda sana ndoa yangu jamani na ninamuomba Mungu anisaidie.
NI KWELI SANAA IMESHUKA?
Kwa mtazamo wangu sanaa yenu imeshuka kutokana na kuendekeza uhuni, je, wewe kama mkongwe unaionaje? Prince Dulla, 0652749414
SANDRA: Siwezi kujua kwa sababu kila mtu ana malengo yake
yaliyomfanya aingie kwenye sanaa. Wasanii walioanzia kwenye vikundi
wanajua thamani ya sanaa ndiyo maana wanajiheshimu lakini wale ambao
hawakupita kwenye vikundi wengi ndiyo wana tabia hizo. Mimi naipenda
sana sanaa na ni kazi yangu ninayoiheshimu.
BIFU NA BATULI VIPI?
Pole na majukumu dada
Sandra, hivi lile bifu lako na Batuli bado hamjalipatia ufumbuzi?
Yaongeeni myamalize ili muwe kitu kimoja. Said, Dar, 0718000790
SANDRA: Sina bifu na Batuli wala msanii yeyote maana maisha yenyewe
mafupi haya, mimi na Davina tuligombana lakini tulishayamaliza.
ETI HAKULIPWA NA DUDU BAYA?
Sandra eti ni kweli hukulipwa na Dudu Baya kwenye ile video ya Nakupenda Mpenzi? Manuely Cimmario, Tanga, 0652153571
SANDRA: Alinilipa hela ya kawaida siyo nyingi.
UKIMYA
Sandra wewe ni mmoja wa wasanii wakali
sana wa maigizo kwenye runinga enzi hizo na akina Kanumba, imekuwaje
jina lipotezwe na watoto, nini shida? Noel Kibere, Moshi, 0714300280
SANDRA: Jina langu halijapotea bado lipo, unajua niliolewa baada ya
hapo nikawa nalea nilivyorudi nikawakuta wasanii hao wapya na
hawajaolewa ndiyo maana wanawika kutokana na kwamba hawana majukumu.
ANAZIKWEPA VIPI SKENDO?
Kwanza napenda
kukupongeza dada Sandra kwa kazi nzuri, pili nataka kukuuliza unawezaje
kuepuka skendo wewe kama mtoto wa kike? Amisa, Dar, 0655603091
SANDRA: Ni kujiheshimu tu.
HUYU ANAMJUA SANA
Nakufahamu Salma, ulikuwa
unasoma Alharamain Secondary na rafiki yako mkubwa alikuwa ni Amina
mdogo wake MwanaFA (Hamis Mwinjuma), vipi unakumbuka viboko vya Ustadh
Abdallah? Mrs Thomas, Dar, 0719353468
SANDRA: Yote ni kweli na hivyo viboko navikumbuka sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment