SIRI
imefichuka! Kwa muda mrefu mwigizaji ambaye pia ni msanii wa muziki wa
mwambao, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amekuwa akinukuliwa akisema kuwa ana
mtoto mmoja lakini sasa mambo hadharani, ukweli ni kwamba ana watoto
wawili.
Kwa
mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo aliyepo mkoani Tabora
anakotokea Shilole, watu wanaomjua wamekuwa wakisikitishwa na matamshi
yake kuwa ana mtoto mmoja.
“Tumekuwa
tukisoma na kumsikia akisema ana mtoto mmoja anayeitwa Rahma, lakini
ukweli ni kwamba ana mwingine anayeitwa Joyce na wote kazaa na wanaume
tofauti,” alisema ‘sosi’ huyo kutoka mkoani humo.
Ili
kupata mzani wa habari hiyo, The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda
lilimtafuta Shilole na baada ya kumpa mkanda mwanzo, mwisho, alikiri
kuwa ana watoto wawili.
“Ni
kweli nina watoto wawili, Rahma na Joyce, wote wanasoma The Click
International School,” alisema Shilole na alipoulizwa kwa nini amekuwa
akisema ana mtoto badala ya wawili, alikosa jibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment