Showing posts with label SHILOLE. Show all posts
Showing posts with label SHILOLE. Show all posts

SHILOLE: SIWEZI KUACHANA NA NUH KAMWE

KUFUATIA varangati lililotokea Tabora katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,  baada mpenzi wa mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,  Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kukataliwa na mashabiki, Shilole ameamua kufunguka kuwa Nuh atabaki kuwa mpenzi wake katika hali yoyote.
Mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akizungumza na paparazi wetu, Shilole alisema lengo lake lilikuwa ni kumtambulisha mpenzi wake kwa mashabiki wake japo walimkataa kuwa shemeji yao.
‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake 'Nuh Mziwanda'.
“Wakati namtambulisha Nuh kwa wakazi wa Tabora kuwa shemeji yao kiukweli nilishindwa kuelewa kwa nini nilizomewa ila ninachoweza kusema tena wakubali, wakatae Nuh atabaki kuwa shemeji yao tu,” alisema Shilole.
Read more >>

NUHU MZIWANDA HANA CHAKE TENA, SERENGETI BOY MWINGINE AMUOPOA SHISHI BABY SHILOLE,

Baada ya kutokuwa na maelewano mazuri kati ya nuhu mziwanda na mpeni wake shilole hivi sasa tetesi zimeibuka upya kwamba wawili hao hawako pamoja tena , hii imefatia kuzagaa kwa picha ambayo shilole amepiga akiwa na njemba mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja,


Read more >>

SHILOLE ATOA KAULI HII "KWA NILIYOYAONA, NIMEKOMA KUJICHUBUA"

Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara ambaye pia ni msanii wa filamu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa kwa alichokiona, amekoma kutumia mkorogo.
Akipiga stori na Ijumaa, Shilole alisema mwanzo alikuwa akitumia mkorogo aina ya ‘karolaiti’ lakini amegundua badala ya kumfanya awe mzuri zaidi, umemletea matatizo kwenye mwili wake.
“Niseme tu kwamba nimekoma na ningejua nisingefanya jaribio la kujichubua, nimeathrika sana na sijaona faida yoyote, zaidi umeniharibia ngozi yangu,” alisema Shilole na kuongeza:
“Imefika wakati natamani niirudishe ile ngozi yangu ya asili lakini siwezi, sasa hivi nikiumia kidonda kinachukua muda mrefu kupona sababu ya huu mkorogo, warembo wanaojipenda ni bora wakaachana na mambo hayo.
Read more >>

"SINA MPANGO WALA MALENGO YOYOTE NA SHILOLE NAMTUMIA TU" MANENO YA MZIWANDA



Mwaka 2013 ni watu wachache tu waliokuwa
wakilifahamu jina la Nuh Mziwanda kwakuwa
alikuwa msanii mchanga anayetafuta nafasi yake
kwenye muziki wa Tanzania. Wimbo wake ulioanza
kumtambulisha uliitwa ‘Otea Nani’ ambao ulipata
nafasi kiasi kwenye vituo vya redio.
Lakini jina la muimbaji huyo lilikuja kuwa kubwa
zaidi baada ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi
na Shilole, uhusiano ambao umekuwa wa wazi
katika mitandao yao ya kijamii. Kuonesha kuwa
ana mapenzi ya kweli kwa Shilole ambaye ni
mama wa watoto wawili, Nuh alijichora tattoo
mkononi yenye jina la Shilole.
Shilole pia aliamua kumpa shavu mpenzi wake kwa
kuonekana kwenye video ya wimbo wake
‘Msondongoma’ na hivyo kumwongezea wigo
zaidi. “Yeye ndo Mama watoto Mungu akijaalia,”
aliandika Nuh kwenye picha ya Shilole aliyoiweka
kwenye akaunti yake mtandao wa Instagram yenye
followers zaidi ya 19,000.
“Ukichagua kitu roho yako inapenda raha
sana.sasa kwa mfano mimi Mziwanda nna haja
gani ya kucheat wakati mtoto ana kila kitu,
kiukweli napenda mke wangu alivyojaa jaa mie
hoooooi,” aliandika kwenye picha nyingi ya
Shilole.
Naye Shilole kwenye picha aliyoiweka kwenye
mtandao huo akiwa na Nuh Mziwanda aliandika,
“Ilove my baby,” kudhihirisha upendo wake.
Hakuna shaka kuwa uhusiano huo umemwezesha
Nuh Mziwanda kukuza jina lake na ameutumia
vizuri kujitambulisha zaidi.
Read more >>

SHILOLE: MPENZI WANGU AMBAYE NI SERENGETI BOY WANGU NDIYE ANAYENITIBU VIZURI

STAA wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefungua kinywa chake na kusema mpenzi wake wa sasa, Nuh Mziwanda ndiye anayemtibu vizuri kunako ‘sita kwa sita’ japokuwa watu wengi wamekuwa wakiudharau mwili wake.
Staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akizungumza na gazeti hili bila kung’ata maneno, Shilole alisema wengi wanashindwa kujua kwamba mtu anaweza kuwa na mwanaume mwenye umbo kubwa lakini akawa hayajui mapenzi lakini mwenye umbo dogo kama Nuh, akawa ni bingwa wa mapenzi.
Akiendelea kumwaga data mbele ya kinasa sauti cha Amani, msanii huyo anayetamba na wimbo wa Nakomaa na Jiji alisema kuwa katika mapenzi, umri wala ukubwa wa umbo hauna maana yoyote.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
“Yaani kwa kweli Nuh ananimudu na tunaenda sawa katika suala zima la mapenzi, kwa hiyo sioni udogo wake kwangu, kwa upande wangu Nuh ni mkubwa sana watu wasiangalie mwili,” alisema Shilole pasipo kutaja umri wa mpenzi wake huyo.
Shilole aliongeza kuwa, kutokana na mahaba ya nguvu anayoyapata kutoka kwa mpenzi wake huyo, anapata nguvu ya kufanya kazi vizuri siku hadi siku hivyo hapati tamaa.
“Sina stress za mapenzi na mara nyingi nafanya kazi zangu zinaenda sawa kabisa,” alimalizia Shilole.
Read more >>

SHILOLE ATAJA SABABU ZA KURUDIANA NA MZIWANDA, SOMA ZAIDI HAPA

STAA wa wimbo wa Nakomaa na Jiji, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema sababu kubwa ya yeye kurudiana na mpenzi wake waliyegombana, Nuhu Mziwanda ni kuombwa msamaha.
Staa wa wimbo wa Nakomaa na Jiji, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
Shilole alisema mpenzi wake huyo aligundua kwamba aliteswa na wivu na kusababisha wagombane hivyo alipotambua kosa lake, aliomba msamaha wakarudiana na mambo yakawa swari.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’
“Kikubwa ni kwamba ameomba msamaha ndiyo maana na mimi sikuwa na hiyana, nikapatana naye siku chache tu baada ya kugombana,” alisema Shilole.Hivi karibuni wawili hao waliripotiwa kuwa wamegombana na kila mtu kuchukua hamsini zake.
Read more >>

SHILOLE, MCHUMBA’KE MZIWANDA WAZICHAPA!

Lile penzi lililopata ‘promo’ ya kutosha ndani ya muda mfupi kati ya mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na Nuh Mziwanda limeingia shubiri baada ya juzikati wawili hao kuzichapa. Kisa cha wawili hao kuzibuana kinadaiwa ni baada ya Nuh kukuta sms tata ya mwanaume kwenye simu ya Shilole ambapo inadaiwa baada ya jamaa huyo kumtaka mchumba wake huyo ampigie aliyetuma meseji hiyo kukawa na kusuasua.
Mwanamuziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
Chanzo chetu cha habari kilichoomba jina lake lisichorwe gazetini kilitiririka: “Shilole na mchumba’ke walikuwa chumbani, mara ikaingia sms kwenye simu ya Shilole.
“Nuh alipoiona alimlazimisha Shilole ampigie jamaa aliyetuma sms na aweke ‘loud speaker’, Shilole alipoipiga ile namba, akajichanganya kidogo licha ya kuwa, jamaa alikuwa anamjua na wala hakuwa mpenzi wake ila ni washikaji tu.
Mwanamuziki na mpenzi wa Shilole, Nuh Mziwanda akipozi.
“Kuona vile si Nuh akaanza kumpiga na hapo ndipo timbwili lilipotokea. Wote waliumia ila Nuh ndiye aliyeumia zaidi, ilikuwa ni vurugu kweli, baada ya ugomvi Nuh akaondoka na mfuko kama wa rambo hivi akiwa na vitu vyake kana kwamba katimuliwa,” kilidai chanzo hicho.Baada ya kuzipata nyeti hizo, Ijumaa lilimtafuta Nuh na alipopatikana alikiri kutokea kwa ugomvi lakini hakuwa tayari kuuzungumzia kwa kirefu.
Shilole alipopatika alisema: “Ni kweli tukio lilitokea. Ni hivi, aliyenitumia ile meseji ni mdau wangu, aliniambia kuwa yuko Dar tutafutane na wala si kwa mambo ya mapenzi lakini nikashangaa Nuh analazimisha nimpigie.
“Ile napiga naongea naye, si akanipiga kofi, hapo vurugu ikatokea. Kimsingi sikutarajia, ni kweli nampenda lakini mimi nadhani bora kila mmoja achukue hamsini zake.“Nilimheshimu sana, wamekuwa wakinitongoza wanaume wengi lakini nikawa nawakatalia kwa kuwa nampenda lakini leo anakuja kunipiga kwa mtu ambaye wala sina mpango naye. Amenikasirisha sana, acha aende zake, unajua mapenzi hayaendi hivyo,” alisema Shilole.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa, baada ya ugomvi huo Nuh alichukua kila kilichokuwa chake na kuondoka kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na Shilole kwani alikuwa ni kama kahifadhiwa.
Read more >>

SHILOLE NA SERENGETI BOY WAKE, NUH MZIWANDA WAONYESHANA MAPENZI UPYA

Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake Shilole.
  Mapenzi ya Nuh Mziwanda na Shilole yaliripotiwa kuvunjika hivi karibu yamerudi kwa nguvu zaidi siku ya jana wamesambaza  picha kupitia account zao Instagram wakiwa pamoja kama ishara ya mapenzi yao kuongezeka zaidi.
Nuh na Shilole wote waliweka picha instagram kuonyesha wamepatana na mapenzi yatadumu zaidi ya miezi kadha iliyotabiriwa.
Read more >>

SHILOLE NA SERENGETI BOY WAKE WAMWAGANA, SIKILIZA MWENYEWE HAPA MZIWANDA AKIFUNGUKA, KISA KIZIMA HIKI HAPA

Stori ya Nuh Mziwanda kujichora tatoo yenye jina la Shilole ilisambaa sana na wengi walikua wakijiuliza siku ikitokea wameachana itakuaje hasa upande wa Nuh ambaye ndiye aliyejichora tatoo hiyo.
Maelezo ya Nuh Mziwanda yamedai kuwa sababu zilizosababisha waachane ni msg ambayo aliikuta kwenye simu ya Shilole ambayo inasemekana ilitumwa na mwanaume,Nuh alipomwambia Shilole apige alionekana kunikanyanga.

Nuh Mziwanda kaongea na Soudy Brown kwenye You heard na kazungumza mambo mengi ambayo yametokea kwenye uhusiano wao.

Kusikiliza.Bonyeza Hapa.
Read more >>

SHILOLE APIGA PICHA CHUMBANI AKILIWA URODA LIVE


KABANG! Picha za staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’ zinazomuonesha live akiwa chumbani tena kitandani kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda zimevuja, Risasi Jumammosi linazo kwenye makabrasha yake.
Staa wa sinema na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Shilole, picha hizo walijipiga wenyewe wakiwa kitandani nyumbani kwa mwanadada huyo, Kinondoni jijini Dar.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha hizo walijipiga baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani kabla ya hapo wasingefanya hivyo.
Katika picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa katika mahaba niue, Shilole anaonekana akiwa amemlalia Mziwanda ambaye naye amejiachia vya kutosha.
‘Shilole’ akipozi kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda.
Habari za ndani zinadai kwamba mmoja wa watu wa karibu alishika simu ya Shilole kisha akajifowadia picha hizo ndiyo chanzo cha kumfikia sosi wetu huyo.
Baada ya kuzidaka picha hizo, gazeti hili lilimtafuta Shilole ambaye kwa sasa anakimbiza na ngoma yake mpya ya Namchukua ambapo alipopatikana kwa njia ya simu alisomewa mashitaka yake ndipo akafunguka namna alivyochezewa na mtu wa karibu yake.
‘Shilole’akiendelea kula ujana na mpenzi wake.
kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda“Kweli hizo picha ni zangu na Nuh (Mziwanda), tulijipiga kwa ajili ya kumbukumbu na tulikuwa na muda mrefu hatujiachia si unajua tena Mwezi Mtukufu?
“Unajua simu yangu haina password na nina watu wengi wa karibu so nahisi ndiyo wamezivujisha na nikimjua namtoa kabisa kwenye network yangu maana siku nyingine anaweza kunifanyia jambo kubwa baya.”
Mbali na hilo, Shilole amesema yupo kwenye mazoezi ya kufa mtu akitamba kwamba atamkimbiza vilivyo staa wa Nigeria, Yemi Alade watakapokutana jukwaa moja kwa ajili ya shoo kubwa kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini, Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Read more >>

AIBU!!! SHILOLE AACHIA PICHA AKIWA ANALIWA URODA NA MPENZI

HUYU NI SHILOLE NA KISERENGETI CHAKE......Ukiona walichokuwa wanafanya hapa utazimia. Wameachia picha wakiwa wanakulana URODA
Read more >>

SHILOLE ATANGAZA RASMI NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IGUNGA 2015




Shilole si mgeni katika kuota vitu vikubwa. Kutoka kwenye ndoto yake ya kufanya kolabo na Jennifer Lopez, awamu hii ameenda mbali zaidi.
 Muimbaji huyo amechoka ‘Kuchuna Mabuzi’ na sasa anataka kuingia mjengoni. Mrembo huyo ambaye jina lake halisi ni Zuwena Mohamed, amepanga kugombea ubunge kwenye jimbo analotokea la Igunga mkoani Tabora katika uchaguzi wa mwaka 2015!

Akizungumza kwenye kipindi na Sizi Kitaa cha Clouds TV, Shilole amesema yupo serious na nia hiyo na kama Mungu akipenda atakuwa mbunge wa jimbo hilo.
 
“Baada ya Dokta Dalali Kafumu anayefuata ni mimi,” amesema Shilole. 

 “Mimi nadhani napenda jimbo langu na napenda wakazi wangu wa Igunga wananiona toka nakua mpaka sasa hivi, kwahiyo wanafurahi. Sasa wananiambia ‘sisi hatutaki kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa wananipa changamoto. 

"Vitu viwili vya kwanza ambavyo nitavifanya nikiingia kwenye lile bunge nikiwa kama msanii, kwanza nitatetea haki za wasanii, cha pili Igunga yangu wapo wakazi wa Igunga vijana wapate kazi, yaani akina mama, wale mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. Kwahiyo nitawatafutia kazi, nitajenga chuo cha muziki,” alijinadi muimbaji huyo.
 
“Mimi jimbo langu nalijua na nimekua pale mpaka nimekuwa mkubwa lazima nilitimize sitaki wananchi wangu wapate tabu. Mimi nadhani wanaoenda kugombea majimbo yasiyo ya kwao wanaweza fanya chochote, lakini kama ni wa hapo lazima itakuuma. 

"Lakini unakuta mtu wa Dar es salaam anakwenda kugombea Mtwara huko nani anamjua? Mimi nitaenda kugombea kwangu lazima nitapata kura lazima watanipa! Kwahiyo kaeni tayari Shilole ni mbunge mtarajiwa Igunga,” alitamba.
 
Read more >>

SHILOLE NA NUHU MZIWANDA WAFUMWA LIVE MLIMANI CITY. TAZAMA HAPA


Kama kawaida shilole na Kipenzi chake Utamwambia nini shilole akuelewe kwa huyo Nuhu.. Pamoja na kukataliwa Ukweni, Shilole atakufa na kuzina na na Nuhu. je wewe mdau unaona Shilole wameendana na Nuhu??
Read more >>

SHILOLE NA BABY MADAHA WAANZISHIANA BIFU ZITO, CHEKI ZAIDI HAPA

MTIFUANO mzito umeibuka kati ya mastaa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Baby Madaha baada ya kurushiana vijembe.
Staa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Awali katika gazeti la Amani toleo la wiki iliyopita, Baby Madaha alinukuliwa akisema kuwa Mwezi wa Ramadhani unambana kiuchumi, kwa vile kumbi nyingi za starehe zimefungwa, hivyo anakosa shoo.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Shilole alisema anamshangaa Madaha kwa kukosa hofu ya Mungu, huku akimchana kuwa, haweki akiba, anaishi maisha ya kutegemea shoo ndiyo maana anaulalamikia mwezi huu.
Baby Madaha.
Madaha alivyoelezwa kuhusu maoni ya Shilole, alikuja juu na kutema cheche: “Shilole anatafuta kiki kupitia jina langu, kwanza si hadhi yangu. Siwezi kujibishana na msanii anayetegemea shoo za kwenye vigodoro, akatafute pa kutokea.”
Read more >>

SHILOLE: HATA MKIMUITA SERENGETI BOY, MZIWANDA WANGU ATANIOA TU ILI WANAFIKI WAFUNGE MIDOMO YAO


Msanii  wa  maigizo  na  muziki  wa  kizazi  cha  leo, Zena  Mohammed  ‘Shilole’  amekuja  juu  na  kusema  anashangazwa  na  habari  zilizozagaa  mjini  kuwa  yeye  amekataliwa  ukweni.


Akiongea  na  Mpekuzi, Shilole  amesema: “Nashangaa  watu  wanasema  eti  nimekataliwa  ukweni  kisa  umri  wangu  kuwa  mkubwa  kuliko  wa  mwanaume. Ninachokijua  mimi  umri  haujalishi  katika  mapenzi, kikubwa  ni  upendo  wa  kweli  na  kuheshimiana.


“Habari  za  mimi  kukataliwa  ukweni  hazina  ukweli  wowote, na  wala  hakuna  mtu  niliyezungumza  naye  kuhusiana  na  hilo  swala  na  wala  hakuna  ndugu  yeyote  wa  Nuh Mziwanda  aliyeonysha  kutonipenda. 

“Nilipokelewa  kwa  furaha  sana  Ukweni  na  habari  njema  ni  kwamba  hivi  karibuni  mtarajie  kuona  ndoa  ili  wanafiki  tuwafunge  midomo  yao,”  alisema  Shilole.
Read more >>

BAADA YA KUKATALIWA UKWENI, SHILOLE AMTETEA SERENGETI BOY WAKE

MWANADADA anayefanya vizuri kunako gemu la muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametetea maisha yake ya kimapenzi na Nuh Mziwanda, akisema madai kwamba ni kijana mdogo kuliko yeye, siyo kweli kwani wanalingana umri.
Mwanadada anayefanya vizuri kunako gemu la muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
“Mimi na Mziwanda wangu tunalingana kiumri lakini nawashangaa sana wanaonisema kila siku eti ninatembea na Serengeti boy, jamani mpenzi wangu siyo mdogo kwangu, tunalingana umri, ninampenda na yeye ananipenda, hatujali maneno ya watu,”alisema Shilole.
Nuh Mziwanda
Katika kuonyesha mapenzi yake kwa mwanadada huyo ambaye pia ni muigizaji wa filamu, Mziwanda amejichora tattoo yenye jina la msanii huyo, ambalo haliwezi kufutika.
Read more >>

SHILOLE AKATALIWA UKWENI KWA SABABU ANAUMRI MKUBWA KULIKO MWENZA WAKE



Haijakaa poa! Habari zinadai kwamba baadhi ya ndugu wa msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda ambao ni wakwe wa staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ hawamtaki kwa madai kuwa ana umri mkubwa kuliko ndugu yao.
Staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
Wakizungumza na Ijumaa Wikienda kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanandugu hao (majina yanahifadhiwa) walisema umri wa Shilole siyo wa kuishi na ndugu yao, Mziwanda kwani hawaendani.
“Ukweli ni kwamba mapenzi hayaingiliwi lakini tunaumia kuona ndugu yetu katika penzi zito na Shilole ambaye hawaendani kiumri,” alidai mmoja wa ndugu hao.

‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda
Alipotafutwa Shilole ili kufikishiwa ujumbe wa ndugu hao kwamba hawamtaki, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Read more >>

SIRI NZITO ILIYOFICHUKA KUHUSU MWANADADA SHILOLE

SIRI imefichuka! Kwa muda mrefu mwigizaji ambaye pia ni msanii wa muziki wa mwambao, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amekuwa akinukuliwa akisema kuwa ana mtoto mmoja lakini sasa mambo hadharani, ukweli ni kwamba ana watoto wawili.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo aliyepo mkoani Tabora anakotokea Shilole, watu wanaomjua wamekuwa wakisikitishwa na matamshi yake kuwa ana mtoto mmoja.
“Tumekuwa tukisoma na kumsikia akisema ana mtoto mmoja anayeitwa Rahma, lakini ukweli ni kwamba ana mwingine anayeitwa Joyce na wote kazaa na wanaume tofauti,” alisema ‘sosi’ huyo kutoka mkoani humo.
Ili kupata mzani wa habari hiyo, The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shilole na baada ya kumpa mkanda mwanzo, mwisho, alikiri kuwa ana watoto wawili.
“Ni kweli nina watoto wawili, Rahma na Joyce, wote wanasoma The Click International School,” alisema Shilole na alipoulizwa kwa nini amekuwa akisema ana mtoto badala ya wawili, alikosa jibu.

Read more >>

HAWA NDIO MASTAA WA KIBONGO WANAOMEGWA NA WANAUME WENYE UMRI MDOGO, WEMA NDIO KIONGOZI, SHILOLE ANAFUATA

ms
Mara nyingi tunaishia kusikia rumors tu, kuwa msanii fulani amemzidi umri mpenzi wake na mara nyingi mwisho wa siku rumors zinabaki rumors tu, hadi pale wawili watakapofunguka wenyewe juu ya suala hilo, basi hii ni list ya wasanii wachache tu maarufu na wenye majina hapa town, ambayo inasemekana kuwa wamepigana gape kiumri.
 
Diamond Platnumz Vs Wema Sepetu.
 
Kutokana na wikipedia Diamond Platnumz amezaliwa mwaka 1989 wakati Wema Sepetu amezaliwa mwaka 1988,  wawili hawa walioshibana wamepishana miezi michache tu, huku Wema Sepetu ndio inaonyesha amemuacha Diamond Platnumz kwa miezi michache tu. Hii ni moja ya couple maarufu sana Africa, huku kila mmoja akiwa ana-shine bila kutegemea mgongo wa mwenzie, Diamond akiwa anakimbiza kwenye anga za muziki wakati Wema akiwa ndio actress maarufu anayependwa zaidi na watu na anayeongoza kuwa na mashabiki wengi East Africa.
 
Shilole Vs Nuh Mziwanda.
 http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/03/mzuwanda1.jpg?resize=430%2C430
Rumors had it kuwa Shilole amempiga gape(amemuacha kiumri) Nuh Mziwanda, na siku ilipofika wawili hao walipoamua kufunguka juu ya mapenzi yao, story zilizagaa kuwa Shilole amepata serengeti boy, ingawa hadi hivi sasa haijulikani wameachana kiumri kwa miezi au miaka mingapi.
Irene Uwoya Vs Msami.
 
Ni juzi kati tu, wadau walibaini kuwa wawili hawa wapo katika mapenzi moto moto, na mwisho wa siku ikabidi wafunguke na ku-confirm ukweli huo kuwa wao ni wapenzi kwa sasa, ila rumors had it kuwa Irene Uwoya amemzidi umri Msami, na watu kuanza kuamini rumors hizo hadi pale Msami juzi kati alipoamua kufunguka kuwa yeye amemzidi umri Uwoya kwa miezi mingi tu, ingawa hakufunguka kuhusiana na miezi mingapi.
Read more >>

MAPENZI: MZIWADA UTAFICHA WAPI SURA YAKO SHIOLE AKIKUPIGA CHINI?


Siku chache baada ya mpenzi wa Zuwena Mohamed 'Shiole'  Nuhu  Mziwanda  kuweka kwenye mtandao   wa  'instagram' picha zikionyesha tatoo aliyojichora yenye jina la mpenzi wake huyo, wadau wa filamu nchini wamesema kijana huyo atakuja kujuta siku akitemwa na kubaki na alama zake hizo kama kumbukumbu.

Wakizungumza na mwanahabari  wetu kwa nyakati
tofauti, wadau hao walisema kuwa Shiole aliwahi kusema  kuwa yeye huwa anaacha wanaume na hajawahi kuachwa hivyo kitendo cha Mziwanda kudatishwa na penzi la msanii huyo, siku akitemwa atatamani kuikata miguu yake aliyoichora neno 'shishibaby' aliyodai haiwezi kufutika maisha yake yote.

''Kijana kashikwa pabaya na shishi baby wake, ngoja tuone hii muvi nayo itaishia wapi maana shilole alishawahi kusema yeye ameshawazoea kuacha na si kuachwa hivyo penzi lao likiingia dosali atatemwa na kubaki na majuto ya kuwa na tattoo hizo'' alisema mdau  mmoja  huku  akigoma  kuanikwa  jina  lake.
Mdau  Mwingine alisema ni kweli kwa sasa anaweza kuona sifa  kuwa na alama hizo kwa sababu penzi lao bado liko moto lakini atambue mapenzi huwa yanachuja na kama watu wako nje ya ndoa kuachana huwa si jambo gumu na kila mmoja kuanza maisha yake mapya.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger