Mike Sangu akimlisha chakula mkewe kwa mahaba.
Ndoa
ya mastaa wa filamu Bongo, Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’
inaonekana kurudi na nguvu ya aina yake baada ya wawili hao hivi
karibuni kunaswa wakidhihirisha kwamba, licha ya yanayotokea,
wanapendana kinomanoma.
Hivi
karibuni wanandoa hao walinaswa kwenye mnuso ulioandaliwa na msanii
mwenzao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ndani ya Great Wall Restaurant
iliyopo Oysterbay ambapo kila wakati waliwarusha roho wenzao kwa
kuwaonesha ‘mahaba niue’ na ulipofika muda wa chakula ilikuwa ni mtindo
wa nilishe nikulishe.
Akizungumzia
mwenendo wa ndoa yao kwa sasa baada ya kuishi mbalimbali kwa muda
mrefu, Mike alisema: “Sasa nafarijika sana kuwa karibu na mke wangu,
hapa tunarejesha mapenzi yetu, kwa kifupi ndoa yetu ni mpya na tamu
kuliko watu wanavyodhani.”

No comments:
Post a Comment