Staa wa filamu za Kibongo, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’ juzi kati
alimfanyia sapraizi ya kumpelekea keki baba yake wa kufikia Alex Humba
Lumila ambaye ni mume wa mama yake Suzan Lewis ‘Natasha’ katika siku
yake ya kuzaliwa.Staa huyo alifanya kisherehe hicho cha kushitukiza
kilichochukua nusu saa ikiwa ni katika kuonesha upendo wake kwake, hali
iliyomfanya mzee Humba abaki amepigwa na butwaa huku akionesha furaha
aliyokuwa nayo.
Mzee Alex Humba akimlisha keki mkewe Suzan Lewis ‘Natasha’.
Akizungumzia tukio hilo, mama wa Mona, Natasha alisema: “Nimefurahi
sana, namshukuru mtoto wangu Mona kwani sikutarajia kama atamfanyia baba
yake sherehe hii kwani hata mimi alinificha ila imeleta upendo mkubwa
ndani ya nyumba kama hivi unavyoona tunasherehekea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment