WASTARA: NIMEGUNDUA WANAUME WENGI WANATAKA KUNIOA ILI WANITUMIE

Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma amefunguka kuwa tangu mume wake Juma Kilowoko ‘Sajuki’ afariki dunia, wamekuwa wakijitokeza wanaume kibao wakitaka kumuoa lakini amegundua wengi wana nia ya kunitumia tu.
Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kama mwanamke amekuwa akitamani kumpata mwanaume wa kumfariji lakini kinachomchanganya ni sampuli ya wanaume wanaotuma maombi kwake.
“Mpaka sasa wameshanitokea wanaume zaidi ya kumi lakini wengi wao nawaona wananitaka ili kujua nini nilichonacho na wengine wananifuata wakidhani watapata mali na si mapenzi ya dhati.
“Kimsingi wanataka tu kujua Sajuki alidata na nini kwangu, mimi siko hivyo. Siwezi kumruhusu mtu aingie kwenye maisha yangu kwa masilahi yake. Ninayemhitaji namjua moyoni na ipo siku nitampata kwani siangalii mfuko wa mtu, naangalia tabia,” alisema Wastara.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger