Ugomvi uliompelekea kubadili maisha yake.
Una habari kuwa kuna sababu
zilizompelekea diamond kuzidi ku-make headlines siku hadi siku?, kama
ilivyo kwa msanii yeyote yule mwenye mafanikio duniani, kuna ishu mbili
tatu zilizowahi kumtokea katika maisha yake, ambazo ndio zilimpelekea
kumsukuma, pamoja na jitihada za kujituma, kuweza kumfikisha hadi kwenye
mafanikio yake. Kama ulikuwa hujui, basi bila Diamond kufanya haya, hii
leo, hizo tuzo zote, kuanzia ya mtv na kili zingekuwa bado ni ndoto, na
kwa hapa Tzee angekuwa na-hit tu kinyumbani nyumbani kama ilivyo kwa wasanii wengi wa bongo fleva.

Rumors
has it kwamba, bila Diamond kugombana na aliyekuwa manager wake wa
zamani, hii leo asingekuwa amefikia hapa alipo, manyanyaso aliyoyapata
hapo nyuma, akiwa na uongozi wake wa zamani, ndio
iliyomsukuma kufanya vitu kwa bidii na kufikia hadi hii leo, mbali na
struggle zake za kila siku katika kujitangaza kimuziki.

Inasemekana
kuwa management yake ya sasa ndio inayompa sapoti kubwa sana katika
kufanya vitu ki-international zaidi, na jina lake kuzidi kukua
ulimwenguni, hadi kwa hivi sasa watu wamesha msahau Diamond wa mbagala.
Alipoamua kufaya jambo la hatari katika muziki wake.

Kama
ilivyo katika kila biashara, bila risk huwezi kupata kile ulichokuwa
unatarajia, na wala huwezi kuendelea, utabaki hapo hapo siku zote, hii
ndio mchezo aliofanya Dangote, kuanzia kutoka kufanya video za milioni
mbili hadi kufikia mahali na kufanya video za zaidi ya milioni ishirini,
kitendo hichi ndicho kilichopelekea Diamond Platnumz aweze kujulikana
zaidi nchi mbali mbali, haswa kwa nyimbo yake ya “my Number1”. Ni moja
kati ya vitu ambavyo matunda yake yanaonekana hadi leo, kwa kuendelea
kukaa on top kwenye charts, hadi kumpelekea tuzo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment