WAZIRI MKUU, PINDA AMVAA DUDE, KISA KUTOFUNGA NDOA

Neno la mkubwa! Habari ikufikie kwamba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda anadaiwa kumvaa staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, kisa kikielezwa kuwa alikuwa akimhoji kwa nini hataki kufunga ndoa?
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akiwa kwenye picha ya pamoja na staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mwishoni mwa wiki iliyopita Dude alikwenda nyumbani kwa Pinda maeneo ya Oysterbay, Dar kwa ajili ya kumsalimia kiongozi huyo.
Katika ‘mtoko’ huo, staa huyo aliambatana na mwanamke wake ambaye hajafunga naye ndoa, Eva.
Ilielezwa kwamba jamaa huyo na ‘mai waifu’ wake walipokelewa kwa bashasha kubwa na mke wa Pinda, mama Tunu Pinda.

Chanzo hicho kilinyetisha kuwa katika mazungumzo yao ndipo ‘mzee’ akambana Dude akitaka kujua kwa nini hafungi ndoa na badala yake anaishi na Eva isivyo halali hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani?
Hata hivyo, mazungumzo yao yaliishia kwa wawili hao kukubaliana kuwa Dude afunge ndoa na Eva ili mambo yaende vizuri.Ilielezwa kwamba wakati Dude na mkewe wanaaga kuondoka nyumbani hapo, mama Tunu Pinda alimzawadia staa huyo jogoo mkubwa kwa ajili ya Sikukuu ya Iddi.
Baada ya kuzitia kibindoni ‘niuzi’ hizo, Ijumaa Wikienda lilimwendea hewani Dude na kumbana kuhusu ishu hiyo ndipo akafunguka kila kitu:
“Ni kweli mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda aliniita mimi na mke wangu, alinibana sana. Mzee alitaka kujua kwa nini hadi umri huu sijaoa?

“Kwa kweli amenisisitiza sana, anaonekana hapendezwi na mimi kutofunga ndoa lakini kweli kabisa sasa naifunga.
“Kuhusu kuku ni kweli mama Tunu Pinda amenipa zawadi ya bonge la jogoo, shukrani kwa mama Pinda ingawa mzee Pinda alilalamika kuku wake ambae ni dume la mbegu kupewa mimi (kiutani zaidi).”
Dude na Eva wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Naima huku jamaa akitangaza mara kwa mara kuwa anaoa bila kutimiza ahadi hiyo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger