Showing posts with label DUDE. Show all posts
Showing posts with label DUDE. Show all posts

SAKALA JUU YA GARI LA DUDE: MASALA MAPYA YAIBUKA

Kumbe! Lile gari aina ya Toyota Vitz la staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambalo hivi karibuni lilikamatwa kwa msala wa kuhusika na ujambazi jijini Dar, limeibua mapya likiwa bado linashikiliwa na polisi kwenye Kituo cha Kijitonyama a.k.a Mabatini.
Gari aina ya Toyota Vitz la staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Habari za kifukunyuzi zinadai kwamba ndinga hilo si mali ya Dude kama ilivyoelezwa awali, bali ni la mwanamke ‘anayechepuka’ naye aliyetajwa kwa jina moja la Lily ambaye eti ni mke wa mtu (Samson).
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu kutoka Meatu mkoani Simiyu, Samson ambaye ni mume wa Lily alisema alistaajabu aliposikia Dude akisema gari ni lake wakati ni la mkewe aliyefunga naye ndoa mwaka 2011 na yeye alishiriki kulinunua.

“Huyo Dude anajua ukweli wa mambo, gari si lake, ni la mke wangu tena fedha ya kulinunulia haikutosha ikabidi nimuongezee laki nne kwa kuwa alikuwa akidaiwa kwa usumbufu mkubwa.
“Isitoshe katika vijana waliokamatwa na gari hilo, mmoja ni mdogo wa mke wangu na siri zote za yeye kutoka na Lily huwa ndugu zake wananisimulia.

“Mara kadhaa nimemuonya Dude lakini huwa anakana kuwa hatoki naye bali ukaribu wao ni kutokana na sanaa na kudai ni kama ndugu kwa kuwa alikuwa akijuana na mama yake,” alisema.
Baada ya madai hayo kuwa ‘hoti’, Ijumaa Wikienda lilimsaka Lily ambaye hakuwa tayari kuzungumza kama gari hilo ni lake au la Dude na kusisitiza aulizwe Dude ambaye alikiri kufahamiana naye huku akikubali kumfahamu Samson pia.

Kulwa Kikumba ‘Dude’ akiwa ndani ya ofisi za Global.
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Dude aliyekiri kuwafahamu Samson na Lily kuwa ni wanandoa japokuwa wana migogoro.
“Matatizo yao ya ndoa wasihamishie kwangu, gari ni langu na lilikuwa linauzwa, Lily nimemlea kisanii maana marehemu mama yake mzazi nilikuwa namuita dada, ndiye aliyenikabidhi Lily mwaka 2003.
“Nimejaribu kumsaidia kisanii, sitaki kuchafuka, Lily ni mwanangu nimemlea,” alisema Dude.
Read more >>

SAKATA LA UJAMBAZI; NDINGA LA DUDE NGOMA NZITO!

Lile ndinga aina ya Toyota Vitz la mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambalo lilidaiwa kutumika kwa ujambazi juzikati, bado lina ugumu wa kuachiwa kutokana na watuhumiwa walioka matwa nalo kuhusishwa na makosa ya mauaji.
Gari ndogo aina ya Toyota Vitz la mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka jeshi la polisi ambacho kiliomba hifadhi ya jina, Dude amekuwa akifuatilia mara kadhaa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama  ‘Mabatini’, Dar, lakini imeshi ndikana kutokana na kosa hilo.
“Hili suala limeshakuwa gumu, si jepesi kama anavyofikiria, hili gari halipati leo wala kesho atasubiri sana maana wale watuhumiwa waliohusika na lile tukio la kutaka kuiba Bajaj ni majambazi sugu, walikuwa wakisakwa kwa kesi ya mauaji,” kilisema chanzo hicho.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ akiwa ngani ya ofisi za Global.
Ndinga hilo lilikamatwa Julai 21, mwaka huu maeneo ya Kijitonyama likiwa na watuhumiwa waliohusika na tukio la wizi wa Bajaj waliojitambulisha kwa majina ya Seif na Longina.
Read more >>

DUDE AFUNGUKA JUU YA TAARIFA ZA GARI LAKE KUHUSISHWA NA UJAMBAZI JIJINI DAR

Baada ya gari la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ kukamatwa na polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama, amezungumzia nini kinaendelea kwenye madai hayo.
 

Akizungumza na Bongo na Matukio leo, Dude amesema kuwa ni kweli gari yake imedaiwa kuhusishwa na tukio hilo lakini uchunguzi unaendelea wa kuwatafuta wahusika aliyokuwa amewaachia gari hilo.
 
“Siwezi kulizungumzia suala hili kwa sababu uchunguzi unaendelea na polisi, lakini gari yangu inadaiwa kukamatwa kwenye tukio la ujambazi,” amesema.

“Kuna madogo walikuwa nayo hiyo gari, kwasababu nilikuwa naiuza kwahiyo hao madogo ndio walikuwa nayo. Lakini siwezi kulizungumzia suala hili kwa sababu kuna mtu wanamtafuta mpaka wamkamate ndo tujue hii kweli ilikuwaje. Kwahiyo kulielezea hili naonekana kama naharibu upelelezi wa polisi. 

Mimi hawakunikamata nilienda kwa sababu waliniita nikaenda kutoa tu maelekezo nikaachiwa. Sema tu gari yangu imeharibiwa kwa sababu wale vijana walipiga kelele za wizi wananchi wakabonda bonda lile gari. Nadhani kuanzia Jumatatu au Jumanne ninaweza nikalielezea hili kwa mapana zaidi kwa sababu nitakuwa nimeshajua polisi wanaendeleaje.”

Kwa mujibu wa Global Publisher, gari hilo lilihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu ni aina ya Vitz lenye namba za usajili T 360 BAJ.

 Lilikutwa likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya Seif Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za usajili T 296 CSC iliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.
Read more >>

DUDE AJIINGIZA KWENYE UJAMBAZI, KESI IPO POLISI

GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.
Gari la dude muda mfupi baada ya kukamatwa, Dude alitokea Polisi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, gari hilo aina ya Vitz lenye namba za usajili T 360 BAJ, lilikutwa likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya Seif Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za usajili T 296 CSC iliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.
Inadawa kuwa muda mfupi baada ya kukamatwa, Dude alitokea Polisi na kulitambua gari lake, lakini maelezo yake hayakuwatosheleza Polisi hivyo kumshikilia katika kituo kidogo cha Polisi Mabatini hadi kesho yake alipodhaminiwa.                                                              Muonekano wa gari hilo kwa nyuma.
Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Dude ili azungumzie taarifa hizo, lakini aliwataka kufuatilia jambo hilo katika kituo cha Polisi, akisema suala hilo lipo mikononi mwao.
Kulwa Kikumba ‘Dude’
Shauri linalomkabili msanii huyo limefunguliwa kwa Jalada namba .KJL/RB/6399/14 UNYANG’ANYI
Read more >>

WAZIRI MKUU, PINDA AMVAA DUDE, KISA KUTOFUNGA NDOA

Neno la mkubwa! Habari ikufikie kwamba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda anadaiwa kumvaa staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, kisa kikielezwa kuwa alikuwa akimhoji kwa nini hataki kufunga ndoa?
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akiwa kwenye picha ya pamoja na staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mwishoni mwa wiki iliyopita Dude alikwenda nyumbani kwa Pinda maeneo ya Oysterbay, Dar kwa ajili ya kumsalimia kiongozi huyo.
Katika ‘mtoko’ huo, staa huyo aliambatana na mwanamke wake ambaye hajafunga naye ndoa, Eva.
Ilielezwa kwamba jamaa huyo na ‘mai waifu’ wake walipokelewa kwa bashasha kubwa na mke wa Pinda, mama Tunu Pinda.

Chanzo hicho kilinyetisha kuwa katika mazungumzo yao ndipo ‘mzee’ akambana Dude akitaka kujua kwa nini hafungi ndoa na badala yake anaishi na Eva isivyo halali hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani?
Hata hivyo, mazungumzo yao yaliishia kwa wawili hao kukubaliana kuwa Dude afunge ndoa na Eva ili mambo yaende vizuri.Ilielezwa kwamba wakati Dude na mkewe wanaaga kuondoka nyumbani hapo, mama Tunu Pinda alimzawadia staa huyo jogoo mkubwa kwa ajili ya Sikukuu ya Iddi.
Baada ya kuzitia kibindoni ‘niuzi’ hizo, Ijumaa Wikienda lilimwendea hewani Dude na kumbana kuhusu ishu hiyo ndipo akafunguka kila kitu:
“Ni kweli mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda aliniita mimi na mke wangu, alinibana sana. Mzee alitaka kujua kwa nini hadi umri huu sijaoa?

“Kwa kweli amenisisitiza sana, anaonekana hapendezwi na mimi kutofunga ndoa lakini kweli kabisa sasa naifunga.
“Kuhusu kuku ni kweli mama Tunu Pinda amenipa zawadi ya bonge la jogoo, shukrani kwa mama Pinda ingawa mzee Pinda alilalamika kuku wake ambae ni dume la mbegu kupewa mimi (kiutani zaidi).”
Dude na Eva wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Naima huku jamaa akitangaza mara kwa mara kuwa anaoa bila kutimiza ahadi hiyo.
Read more >>

CHADEMA, CCM WAMGOMBEA DUDE. KISA AMETANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE

VITA! Baada ya kutangaza nia ya kugombea ubunge, staa wa sinema Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amesema anapata wakati mgumu kwa kuwa vyama vikubwa vya siasa vinamgombea.
Staa wa sinema Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Dude alisema kuwa awali alikuwa agombee kupitia Chadema, lakini baadaye CCM nao kupitia kiongozi mmoja mwenye wadhifa mkubwa serikalini alimtaka agombee kupitia tiketi ya chama hicho, jambo linalomfanya abaki njia panda.
“Nipo njia panda maana Chadema wamenipa jimbo la kugombea huku kwa upande mwingine CCM nao wamenitaka nigombee kupitia chama chao yaani kwa sasa sijui cha kufanya kabisa,” alisema Dude.
Read more >>

TINO NA DUDE WAKAMATWA NA POLISI

WASANII nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Hisan Muya ‘Tino’ hivi karibuni walitiwa mbaroni katika mji wa Kilifi ulio mbele ya Mombasa nchini Kenya baada ya kukutwa wakipiga picha za filamu yao bila kuwa na kibali.
Hata hivyo, waigizaji hao baadaye waliachiwa, ingawa hali ilikuwa ngumu kidogo kwa Tino, ambaye polisi wa Kenya walidai hakuwa Mtanzania, bali ni raia wa Somalia.
Dude alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema liliwatokea kutokana na mazoea ya huku nyumbani ambako hufanya shughuli zao za kupiga picha za filamu zao bila kuhitaji kibali.

Msanii nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Yaani tumepata aibu ya mwaka, kwani tulienda kushuti bila kuomba kibali kutokana na mazoea ya huku kwetu Bongo, tulipekuliwa sisi na gari letu, baada ya hapo kibali kikaletwa nikaachiwa lakini Tino waliendelea kumshikilia wakisema ni Msomali mpaka mkuu wa shirikisho la filamu Mombasa alipokuja kuokoa jahazi, ukweli Kenya hakufai, alisema Dude.
Via BongoClanTz
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger