Rafiki zangu, nazungumza juu ya kauli ambazo zina ishara mbaya kwenye uhusiano. Wakati mwingine unaweza kumsikia mpenzi wako akikuambia maneno ya ajabu sana, lakini usielewe maana yake ni nini.
Ngoja
nikuambie, kila kinachotoka kinywani mwa mpenzi wako kukuambia wewe
kina maana yake. Lengo ni kujifunza; kufahamu maneno hayo na maana zake.
Wiki iliyopita tulianza na maneno, huvutii na hupendezi
UNANUKA...
Mwenzi
ambaye hana mpango tena na wewe, ataanza kukuonea kinyaa. Maneno ya
kejeli kwake si suala la kujiuliza mara mbili. Ni rahisi sana kukuambia
unanuka!
“Ebwanae unanuka jasho sana, hebu kaoge kwanza,” anaweza kukuambia hivyo.
Katika
hali ya kawaida kabisa hii ni dharau, ila inawezekana labda mpo katika
hatua ya kuelekea kwenye mahaba, lakini ulipomsogezea kinywa chako,
ukakutana na maneno haya: “Aaaah! Mh...unanuka mdomo bwana, sitaki!”
Pia unaweza kumsikia akisema: “Ongea taratibu unanirushia mate bwana.”
Hizi si kauli njema na bila shaka anajaribu kukuonesha jinsi ambavyo umepungua thamani kwake.
Huwezi
kunuka kwa mpenzi wako, siku zote huwa unanukia, lakini kama ameona
dosari yoyote na yeye kama mwenzi wako wa karibu ana wajibu wa
kuhakikisha anatumia lugha nzuri kukurekebisha, lakini kwa kuwa hana
mapenzi na wewe, hana haja ya kuonesha mapenzi yake, anakubwatukia
atakavyo!
SINA MPANGO WA KUOA
Wengi wanapokuwa
katika uhusiano wanakuwa na ndoto zao, lakini ni aghalabu kukuta mtu
yupo kwenye uhusiano wa kula raha tu! Mara nyingi ndoto kubwa huwa ni
ndoa, ingawa ni vyema kupeana muda wa kuchunguzana kwa muda mrefu zaidi
kabla ya kufikia azimio hilo muhimu maishani.
Lakini unapokuwa na mpenzi wako
faragha, kwenye mazungumzo au katika matembezi ya jioni halafu ghafla
akakuambia hana mpango wa kuoa au kukuoa, ni kama anakupa tiketi ya
kukuacha.
Pima
kauli hii, kama anazungumza kwa mzaha utagundua na kama yupo ‘serious’
pia utajua. Angalia macho yake na namna anavyoweka mkazo kwa kauli yake
hiyo.
Lakini
hata kama hatakuambia hana mpango wa kukuoa lakini kusema kwamba hana
mpango wa kuoa kwa muda huu (huo) nayo ni alama kwamba hana ndoto ya
kuendelea nawe tena na kama ataendelea, anapoteza muda tu.
HUJUI MAMBO...
Hii ni mbaya zaidi maana inagusa eneo ambalo wengi hawapendi kuonekana hawawezi! Unaweza kuwa naye chumbani, ukijitahidi kadri uwezavyo kuhakikisha anafurahia, lakini ghafla unashangaa anakuambia hujui mambo!
Tena
wakati anakuambia, anatamka kwa kumaanisha huku akitaka uongeze ujuzi
maana muda wote mliokuwa naye hapo, ni kama mlikuwa mnacheza!
Tafakari anachokuambia, kama kinaingia akilini
No comments:
Post a Comment