Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts
Showing posts with label MAHUSIANO. Show all posts

JFUNZE MBINU NNE ZA KUFANYA ILI USIACHIKE AU KUSALITIWA NA MPENZI WAKO

Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, mapenzi yanachukuwa sehemu kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku.Tunafanya kazi usiku na mchana lakini pesa tunazopata tunazitumia kwenye kufurahia maisha na wapenzi wetu.Ndiyo maana ukiwa hauko sawa kimapenzi, namaanisha ukiwa huna mpenzi wakati unahitaji kuwa naye au unaye lakini anakukorofisha, hata mambo mengine huwezi kuyafanya kwa ufasaha. 


Lakini yule ambaye maisha yake ya kimapenzi yako sawa, anapata anachokitaka kutoka kwa mpenzi wake, utagundua anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na furaha haikauki.Wakati ukweli ukiwa hivyo, wapo ambao wanaachika kila siku kwa sababu ya kushindwa kujua namna ya kuwashika wapenzi wao. Kuna ambao kusalitiwa kumekuwa ni sehemu ya maisha yao kwa sababu hawajui yapi wayafanye ili wapenzi wao wasifikirie kutoka nje ya uhusiano wao.

Kimsingi nimegundua wengi hatuna elimu ya kutosha juu ya mapenzi. Unakuta mtu kaanzisha uhusiano na mtu ambaye yuko mbali lakini hajui wanawezaje kulidumisha penzi lao. Mmeoana wote mnafanya kazi na ni wanandoa, mnawezaje kuishi katika msingi sahihi? Hayo yote utayajua endapo tu utajua sehemu sahihi ya kuweza kujifunza na kuwa na ufahamu kuhusu mambo hayo.

Huenda wewe tangu umezaliwa hujawahi kujihusisha kimapenzi, leo umeingia kwenye uhusiano na hujui chochote, kama huna elimu ya mapenzi hata kama umzuri vipi, utaachika tu kama siyo kusalitiwa kila siku.

Ndiyo maana leo nimeleta mada hii ili kama ulikuwa hujui, uanze leo kujiimarisha kwenye masuala ya mahaba. Kumbuka hapa nazungumzia mapenzi ya kiutu uzima, yale ambayo huwezi kufundishwa shuleni, kusoma kwenye magazeti, kuona kwenye vipindi vya kawaida vya televisheni au kusikisiliza redioni. Mtandaoni
Mitandao imekuwa ni msaada sana katika ulimwengu wa sasa. Hakuna ambalo utalihitaji usilipate kwenye mtandao. Kwa maana hiyo basi, kama kuna jambo unataka kulijua kuhusu mapenzi, kuwa rafiki wa mitandao husika.

Kwa mfano unataka kujua jinsi unavyoweza kumfurahisha mpenzi wako mkiwa faragha. Ukiuliza mtandao, utakuletea.Licha ya kwamba lugha unayotumika ni ya Kiingereza, naamini wengi wetu tunajua hata kama ni cha kubangaiza. Ila zipo baadhi ya mada ukiandika kwa Kiswahili pia unaweza kuzipata.

Majarida maalum
Yapo majarida yanayozungumzia mapenzi kwa undani wake ambayo yanauzwa sehemu maalum kwa jili ya watu wazima tu. Kama kweli wewe ni mtu mwenye uhitaji wa majarida hayo, ukiulizia utayapata kwani huwezi kuyakuta yanauzwa kiholela.

Wakati mwingine yanauzwa bei kubwa lakini elimu utakayoipata ni kubwa na huwezi hata kujutia fedha uliyotoa. Kwa mfano unanunua jarida la shilingi 50,000 na ndani yake ukapata mada juu ya kuishi kwa furaha na mpenzi wako, namna na kuidumisha ndoa yako, jinsi ya kumpagawisha mpenzi wako muwapo faragha na kadhalika. Huoni itakuwa ni pesa ndogo ukilinganisha na gharama ulizotumia kwenye harusi yenu?

Ongea na wataalam
Kuna wataalam wa mambo ya mapenzi ambao wanaweza kukusaidia. Kwa mfano mimi nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi kushauri wasomaji wangu juu ya mambo yanayowakosesha furaha katika maisha yao ya kimapenzi.

Siyo mimi tu, wapo wengi wakiwemo baadhi ya akina mama ambao wamekuwa wakitumika sana kwenye kuwafunda wasichana kabla ya kuingia kwenye ndoa.Kikubwa ni kujua watu sahihi wa kuwauliza mambo sahihi kuhusiana na mapenzi. Nilichogundua mimi ni baadhi ya watu kuwa na aibu. Hivi unaonaje aibu huku unataka kujua mambo nyeti ambayo unajua kutokuyafahamu kunaweza kuihatarisha ndoa yako?

Angalia vipindi vya kikubwa
Kwa watu wenye uchu na elimu hasa hii nyeti, inabidi wakati mwingine wakubali kuamka usiku na kuangalia vipindi ambavyo vinazungumzia mapenzi kwa watu wazima.Mara nyingi vipindi hivi huwezi kuviona mchana, wanaovirusha husubiri muda ambao watoto wamelala. Ukiwa ni mpenzi wa kuvifuatilia vipindi hivi, ni lazima utakuwa bora kwenye uhusiano wako.


Ni hayo tu ila kama unataka kujifunza zaidi kupitia mimi, usisite kunitafuta. Kumbuka ujanja na ubunifu wako ndivyo vinaweza kudumisha ndoa yako lakini ukiwa unaendesha maisha yako kibubusa, kaa mkao wa kusalitiwa kama siyo kuachwa!

Read more >>

JINSI YA KUMTAMBUA MPENZI ALIYEKUSALITI MUDA MFUPI ULIOPITA


KUNA BAADHI YA WATU WANAYATENDEA HAKI MAPENZI; WAPO MAKINI KWA KILA KITU KATIKA UHUSIANO WAO NA HIVYO KUWA KAMA WANAISHI KWENYE PARADISO YA PEKEE. PIA, WAPO WENGINE AMBAO WANAYAONA MAPENZI MACHUNGU, WANAYACHUKIA NA KWA HAKIKA WANALAANI KUKUTANA NA WENZI WALIONAO.

Kwa nini? Kwa sababu kila siku ni ugomvi, hawana amani. Hawapati muda wa kukaa na kupanga mambo yao, kila wakikutana ni ugomvi. Kunyang’anyana simu na kupekua meseji ndiyo sehemu ya uhusiano wao.
Utakapoona wapenzi hawaishi ugomvi, ujue kwamba wanaishi kwa mashaka. Kila mmoja haamini kama mwenzake siyo kicheche. Pamoja na ugomvi wao, wengi wanashindwa kuwatambua wenzi ambao wamewasaliti muda mfupi uliopita.
Katika mada yetu ya leo, tutaangalia mambo 10 ya msingi ambayo yanaweza kukusaidia kumtambua mpenzi aliyekusaliti muda mfupi uliopita. Hapa namaanisha utaweza kumtambua mpenzi aliyekusaliti ndani ya saa 24.
Tafadhali weka mawazo yako hapa ili uweze kumgundua mwenzi ambaye ni mwizi wa haki yako. Sasa hebu twende tukaone.
RATIBA YA GHAFLA
Rafiki zangu, ukishaanza kuwa na wasiwasi na mpenzi wako kwamba huenda anataka kukusaliti, jambo la kwanza kabisa unalotakiwa kukumbuka ni sehemu aliyokuambia amepitia/anakwenda kama ilikuwa katika mipango yake au amefanya safari ya kushtukiza.
Hii ni dalili ya kwanza kabla hata hamjakutana nyumbani; “Sorry baby, kuna sehemu napitia mara moja, nitachelewa kidogo kurudi nyumbani,” kauli kama hii iangalie sana.
Mwingine anaweza kupiga simu na kusema: “Mume wangu, bosi ametupa ofa ya dina wafanyakazi wote, kwa hiyo nitachelewa kurudi nyumbani, samahani sana dear.”
Kauli hizo mbili ni alama ya kwanza katika kushibisha hoja yako ya kusalitiwa kama ni kweli atakuwa amefanya hivyo. Kumbuka kwamba, si lazima kila anayesema amepata dharura amesaliti.
ANAKWEPA KUWASILIANA
Mtu huyo ambaye ameshatoa taarifa kwamba amepata dharura, utashangaa hataki kuwasiliana na wewe. Pengine ukimpigia simu, anaweza asipokee na kama akipokea anaweza kukujibu: “Nitakupigia baadaye, samahani sipo sehemu nzuri.”
Unaweza kumwandikia meseji lakini pia asijibu. Wapo wengine vichwa ngumu zaidi, ambao wao kuacha kupokea simu na kujibu meseji si vitu muhimu sana, wanazima kabisa! Ukiona dalili hii, basi ujue unasalitiwa.
UCHANGAMFU KUPITILIZA
Pamoja na mambo hayo hapo juu, lakini mwenzi huyu akirejea nyumbani, huwa mchangamfu kupitiliza. Ana maneno mengi, anaanzisha mijadala ya ghafla na kuifunga mwenyewe. Atajifanya anataka kufanya mambo mengi kwa ajili yako.
Ahadi zake zinakuwa nyingi za ghafla na nyingi zipo wazi kabisa kwamba si rahisi kuzitekeleza. Alama hii ni kati ya zile 10 zinathibitisha kwamba ndani ya saa 24 umeibiwa mali yako.
UPOLE KUPITILIZA
Kinyume cha uchangamfu ni upole, kama mwenzi wako ametoka kimapenzi na patina mwingine kwa ile hofu yake moyoni, anaweza kuwa mpole kupitiliza. Anafanya hivyo kwa lengo la kutafuta huruma.
Hana sababu ya kuwa mpole, lakini anaweza kutumia ngao hiyo, ili maswali utakayomuuliza yawe kuhusu upole na ukimya wake, usahau mambo ya kuhisi kuwa umesalitiwa. Hata hivyo, majibu yake yanaweza kuwa ya mkato sana: “Sijisikii vizuri, siku yangu haikuwa nzuri kabisa leo. Kuna mtu nimetibuana naye ofisini, amenichanganya kabisa.”
Alama hii ni moja ya sababu zitakazokufanya uendelee kumchunguza katika hatua zinazofuata ili mwisho ugundue kuwa umesalitiwa au ni wasiwasi wako tu.
UGONJWA WA GHAFLA
Katika kukwepa usumbufu wa maswali mengi, mwingine huamua kujifanya anaumwa. Atarudi akiwa mkimya kuliko kawaida, ukimwuliza atakujibu kuwa anaumwa. Kama mpenzi wake, anajua wazi kuwa hutakuwa na muda wa kuanza kuhisi usaliti badala yake utamjali na kuuliza hali yake.
Mgonjwa huyu kwa kawaida huwa haumwi magonjwa siriasi, sana sana atakuambia hajisikii vizuri, kichwa kinamgonga au moyo unaenda mbio. Ukizungumza kuhusu suala la hospitali atakataa akidai hana hali mbaya sana. Mara nyingi hupenda kukimbilia kitandani, akitaka kupumzika.
Anafanya hivyo kwa sababu anakwepa aibu ya kukutanisha uso wake na wako. Ukitaka kwenda kumnunulia dawa za maumivu atakujibu: “Nimeshameza panadol baby.” Mwenzi wa aina hii unatakiwa umtilie mashaka, maana inawezekana ametoka kufanya kitu kibaya.
MAJIBU TATA
Mpenzi ambaye ametoka kukusaliti huwa hapendi kuulizwa maswali mengi, ukimwuliza majibu yake huwa tatanishi sana. Kwa kuwa ameshasingizia kwamba anaumwa, hivyo atafika na kulala moja kwa moja.
Ukitaka kujua zaidi kuhusu kuugua kwake au dharura aliyoipata iliyosababisha achelewe kurudi nyumbani, hukosa majibu yanayoeleweka. Wakati mwingine anaweza kujisahau na kukupa jibu ambalo linapingana na maelezo yake ya awali. Ukiona hivyo ujue kuna namna.

HATAKI FARAGHA
Kwa kuwa tayari ameshatoka kwa mtu mwingine, huhofia sana kukutana na wewe faragha. Kama tulivyoona katika vipengele vilivyopita, hutengeneza mazingira ya kukufanya msikutane kimwili, hofu yake ikiwa ni kukuficha usigundue mchezo wake mchafu.
Kisingizio cha kuumwa, bila shaka ni kikubwa na kitakufanya ushindwe kuwa na mhemko wa kimahaba, lakini kurudi nyumbani akiwa amekunja ndita au mpole kupitiliza, tafsiri yake ni wewe kuogopa au kuhamisha hisia zako kutoka kwenye mapenzi na kuanza kumfikiria yeye kama yeye.
Kwa vyovyote vile, kama ni mwenzi wako wa muda mrefu, zipo alama nyingi zitakazoweza kukufanya ujue kuwa ametoka nje, kwanza ni vyema kumkazania kukutana naye faragha. Hata kama atasingizia anaumwa, ng’ang’ania kukutana naye, maana hapa ndipo penye ukweli mkubwa zaidi.
Mchunguze anavyokupokea, halafu pima uwajibikaji wake. Huwa mvivu na asiyetaka kutoa ushirikiano. Anaweza kuishia kulalamika kuwa hajisikii vizuri na kusisitiza mhairishe zoezi hilo.
Mpenzi msomaji, njia unayopita kila siku unaijua. Sehemu yenye makorongo unaifahamu, yenye matuta pia utatambua, hata yenye makorongo yenye maji yaliyosimama pia unaijua vyema, sasa ukikutana na tofauti yoyote katika barabara unayoitumia siku zote, maana yake tingatinga limepita.
ANAKWEPA KUSOGELEWA
Akifika tu nyumbani, atahakikisha hupati nafasi ya kuwa naye karibu. Hataki kabisa kusogelewa. Hapo anakimbia vitu vitatu;
Kwanza kabisa, inawezekana huko alipotoka alitumia manukato tofauti na aliyotoka nayo nyumbani asubuhi.
Pili, manukato ya sabuni mpya aliyotumia, anaogopa usiyasikie, tatu, kila mtu ana harufu yake, unapokaa na mtu kwa ukaribu hasa faragha kwa saa mbili au zaidi, kila mmoja huhama na harufu ya mwenzake.
Kwa kuwa wewe unaitambua vyema harufu ya mpenzi wako, atahofia kukusogelea maana utashtukia. Mwisho kabisa, hata kama atakuwa amekwepa yote hayo, labda hajaoga, hajatumia manukato mengine, bado utaweza kumkamata kwa harufu ya manukato, sabuni au mafuta aliyotumia mtu aliyekuwa naye.
Kukwepa kukusogelea, tafsiri yake ni kwamba hataki usikie harufu ya tofauti kutoka kwake, maana anajua alichokifanya. Jiulize, kama kila siku huwa mnapokeana kwa mabusu na kukumbatiana, kwanini safari hii anakukwepa?
ANAKIMBILIA BAFUNI
Akifanikiwa kukuzuga katika kipengele kilichopita, basi safari yake huishia bafuni. Ataenda haraka na hatataka kwenda na wewe maana kuna kitu anajaribu kukuficha. Wengi wanaamini (kuna ukweli kwa asilimia chache) baada ya kuoga wanaweza kupoteza ushahidi wa kutoka nje ya ndoa/wapenzi wao.
Utakapomruhusu aoge, kwanza atatumia sabuni ya siku zote, ambayo anaweza kuitumia kwa wingi awezavyo ili kuficha ushahidi. Atajisafisha zaidi nyeti zake ili usijue kilichotokea muda mfupi.
Akitoka bafuni lazima atakimbilia kwenye meza ya kujipambia kisha hapo atajimiminia manukato ili kuzima kabisa ushahidi ambao ungeweza kumuumbua. Jiulize, kama kila siku huwa mnaoga pamoja, kwanini amekuja ghafla na kukimbilia bafuni bila wewe?
WASIWASI MWINGI
Atakuwa mwenye wasiwasi mwingi sana, hata kama akikubali kukutana na wewe faragha, ushirikiano huwa hafifu. Mwoga kupitiliza na muda wote huwa anahisi kwamba hatakufikisha salama safari yako.
Wasiwasi wake hauishii hapo, hata kupeana mikono tu na kukutanisha macho, kutakuonesha jinsi alivyo na wasiwasi. Si kama anapenda hali hiyo, ila anazidiwa na hisia za usaliti kwa kuwa anajua alichokifanya muda mfupi uliopita.
Kama utavifuatilia vipengele hivyo kwa makini, ni rahisi sana kumkamata mwizi wako. Acha papara, chunguza taratibu, ukiona angalau kuna nusu ya hizi nili zokupa hapo juu, ujue wazi kuwa unaibiwa tu.
Read more >>

SAWA UMZURI, LAKINI UNAJISIKIAJE UNAPOITWA JINA LA ‘MALAYA’?

Niwiki nyingine tena tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.
Mimi niko poa na kama ilivyo ada leo nimekuja na mada ambayo inawagusa wanawake kwa asilimia kubwa. Nazungumzia hii tabia ya baadhi ya wasichana kutumia uzuri wao vibaya kwa kuwapanga foleni wanaume bila kujali madhara yanayoweza kujitokeza.Wewe msomaji wangu utakuwa ni shahidi juu ya uwepo wa wasichana ambao hawawezi kusema ‘no’ pale wanapotamkiwa masuala ya mapenzi.
Katika uchunguzi wangu mdogo, wapo wasichana ambao wameridhika na maisha ya kutokuwa na mwanaume ‘pamanenti’, wao imekuwa ni fasheni kubadili wanaume kama nguo.
Ninapozungumzia wanawake wa sampuli hii, simaanishi machangudoa. Nawazungumzia wale ambao wanafanya kazi zao au wako mtaani lakini hawajabahatika kuwa na wanaume wa kuwashika.
Sasa kutokana na hisia zao za kimapenzi, anayetokea mbele yao ni halali yao na mapenzi yao huwa hayadumu. Unamkuta msichana mzuri mwenye kila sifa ya kuwa na mpenzi wake lakini yupoyupo tu.
Leo katembea na huyu, kesho na yule na wakati mwingine ni kwamba si tamaa ya pesa, ni tamaa ya mwili au kutafuta tu sifa kuwa katembea na flani. Hii ni sawa kweli?

Unajisikiaje pale unapopachikwa jina la cha wote mtaani kwenu au eneo lako la kazi? Hata kama hawakuiti hivyo, huoni unajivunjia heshima kwa kuwa na uhusiano na wanaume tofauti ndani ya kipindi kifupi tena baadhi yao wakiwa ni marafiki?
Nyie ambao mnajirahisi kwa wanaume mjue mnachoreka sana na mnaonekana msiyoithamini miili yenu.
Matokeo yake sasa watu wanapasiana kama mpira kwenye eneo la 18. Leo unatembea na Shabani, akikuchoka anamsukumia mshikaji wake John na wewe unakubali kirahisi.

Huku ni kujirahisi kulikopitiliza.
Ni sawa unaweza kuwa na sura na umbile zuri linaloweza kukufanya kila unapopita ukatongozwa. Hiyo inatakiwa kuwa changamoto kwako na siku zote simamia utu wako.

Kwa jinsi ulivyo, unatakiwa kuwa na mpenzi kama siyo mume, mtu ambaye anakupenda kwa dhati na aliyetayari kuchukua nafasi yake kama mpenzi. Mtu ambaye atakupa furaha, atakulinda, atakushauri kuhusu maisha na kukusaidia pale ambapo utahitaji msaada wake.
Usipokuwa na mtu ‘pamanenti’, hayo huwezi kuyapata. Utayapataje wakati uliyenaye anataka akuonje kisha kesho atafute sababu akutose na kuhamia kwa mwingine?Nadhani ifike wakati kama ni msichana ambaye unastahili kuwa na mpenzi, utulie na uchague mtu mmoja ambaye utampa dhamana ya maisha yako. Chukua muda kuwa peke yako kwa kipindi flani lakini siku moja amini utampata mtu atakayekulindia heshima yako.Kwa ulimwengu wa sasa siyo sifa kuwa na msururu wa wanaume. Hivi unadhani ni sifa kuwa umetembea na wanaume kibao katika eneo lako la kazi? Hivi unajisikiaje unapokuwa msichana ambaye umetembea na idadi kubwa ya wanaume katika mtaa wenu? 
Ukweli ni kwamba kila utakapopita utakuwa kama hujavaa nguo na ujue wanaume zaidi ya mmoja ambao wametembea na wewe wakikutana na kugundua wote wamekupitia, watakushusha thamani na watakuwa wa kwanza kukuponda kwa wengine kwamba wewe ni kicheche. 
Ifike wakati ujitambue na ujue thamani yako. Uzuri wako hautakuwa na faida yoyote kama kila anayekuambia vipi unamwambia poa! Unamjibu poa, dhamira yake unaijua? Unadhani ukishamuonjesha mara moja ndiyo atakuwa na wewe?
Kama ulikuwa hujui, wanaume wengi sasa hivi wanakwepa sana kuwa na wasichana wazuri. Wanahisi kutakuwa na ugumu katika kuwatuliza kwani wanaume kibao watawatolea macho. Lakini sasa shangaa, wanaume wengi wanajisikia ujiko sana kuwapitia wasichana wazuri. Yaani wanajiona ni wajanja kutongoza na kukubaliwa na akina dada warembo.
Ndiyo maana nasema, usipowajulia hawa watakufanya kama vile mpira wa kona kisha watakuacha na makovu ya aibu na usipate wa kukuoa. Kama atatokea lazima atakuwa ni mtu wa mbali asiyejua nyendo zako, kwa nini ujiwekee historia mbaya?
Tukubali kwamba kuna wakati tunakosea na tubadilike. Hapo ulipo jiulize ni wanaume wangapi ambao umewapa nafasi waujue mwili wako kirahisi? Huoni aibu? Badilika wewe, acha ushamba!
Read more >>

MADADA JE MNAPENDA UUME MKUBWA AU UFUNDI WA KITANDANI, SOMA ZAIDI HAPA


Nimekuwa nikifuatilia maoni ya akina dada wengi sana  mtandaoni, naona wengi wao wanakandia vibamia, lakini timu vibamia nao wanakuja juu wakidai ufundi ndio muhimu. Sasa je ni kweli ufundi ndio muhimu kuliko ukubwa wa mtwangio?
Read more >>

MAPENZI: MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA NDOA


Wapenzi wasomaji wa Jitambue Kwanza, hakuna asiyependa kufurahia utamu wa ndoa katika maisha yake yote ya ndoa. Leo ninakukumbusha tu baadhi ya vituvitakavyokufanya uishi katika ndoa yenye furaha na upendo siku zote.

1. SIRI - Ukiwa katika ndoa, siri ni kitu muhimu sana ambacho huenda ukikifuata kitakuepusha na mambo mbali mbali yatakayosababisha ndoa yako iteteleke. Chagua watu maalumu unaowaamini ili uwatumie katika kuomba ushauri kwamfano, wataalamu wa mambo ya ndoa au saikolojia, ndugu wa karibu au rafiki yako wa karibu sana, na wale wote unaowaamini. Ukifanya hivyo utawaepuka wale wote wenye nia mbaya na ndoa yenu.

2. KUWA MUWAZI KWA MWENZIO - Binadamu tumeumbwa tofauti tofauti, huenda kitabia pia tukawa hatujakamilika kuweza kumudu hali tofauti tofauti zinazotukabili katika maisha yetu, lakini yote hayo mwisho wa matatizo ni kuwa muwazi, kwani wahenga walisema; mficha maradhi kifo humuumbua. Mweleze mwenzi wako pale alipokosea ili ajirekebishe, kuliko kukaa kimia rohoni bila kusema.

3.JIFUNZE KUOMBA MSAMAHA UNAPOKOSA - Hakuna suluhu nzuri na nzito kama kuomba msamaha pale unapokuwa umekosa, maana ukithubutu kufanya hivyo kwa mwanadamu mwenzio, hata kwa Mungu utasamehewa. Jishushe pale mwenzio anapokuwa na ghadhabu juu yako, pengine unaweza kuwa hujakosa, lakini kushuka kwako kunaweza kukamfanya mwenzio ajutie kosa endapo kweli kama atakuwa amekosa. Lakini pia endapo ukijua wewe ndiye mwenye makosa, basi omba msamaha ili kuokoa muda.

4. MCHUKULIE MWENZI WAKO KAMA PACHA WAKO - Mara nyingi umri wa wanandoa hutofautiana sana au kidogo, lakini unapokuwa tayari katika ndoa, vipengele hivi hupotea. Ni vizuri ukamheshimu mkeo au mumeo kwasababu ya ndoa yenu na sio kigezo tu cha umri. Kuna baadhi ya wanaume kuwachukulia wake zao kama watoto na kutoa amri mbaya hata mbele ya watoto wao, hupaswi kufanya hivyo, kwani huo utakuwa ni unyanyasaji wa kijinsia.


5. KUWA MSAFI  - Unapoamua kuwa msafi, sio kuishia katika nguo na mwili wako tu, bali hata kwa watoto wenu pia. Hakikisha nguo za familia zinakuwa safi, na sio kurundika nguo chafu ndani kwa wiki nzima au kuloweka nguo wiki nzima. Uzuri wa nyumba ni pamoja na usafi.

6. MTUMAINI MUUMBA WAKO NA MEMA UTAYALA - Ndoa yoyote ile inayomcha Mwenyezi Mungu, itadumu hadi mwisho wa maisha yao. Wanandoa mnapaswa kumuhofu Mungu wakati wote, kwani mkifanya hivyo mtazibwa macho ya usariti, kiburi, michepuko na hata matamanio yaletayo magonjwa katika ndoa au familia yenu.

Basi msomaji wa uwanja huu wa Jitambue Zone, endelea kutembelea blog hii ili kupata dondoo nyingi za kijamii. Nakuachia ujumbe huu... "MICHEPUKO SIO DILI
Read more >>

MAPENZI:JIFUNZE JINSI YA KUTEKA HISIA ZA MPENZI WAKO, SOMA HII KUJUA


Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kwamba, mapenzi ni furaha na kama upo kwenye uhusiano ambao una mateso na kila aina ya matatizo, basi ujue kwamba haupo sahihi. Hakuna masimango kwenye mapenzi, kunyanyasana na maumivu.

Tafsiri hasa ya mapenzi ni upendo, sasa kama ndivyo, si sahihi kuwa kwenye upendo, halafu chuki inachanganyika ndani yake. Hayo niliyoyataja hapo juu, mama yake ni chuki! Ndugu zangu, nirejee kusema tena kwamba uwanja wa huba ni mpana sana na unahitaji elimu kila wakati.

TUNAJIFUNZA NINI?
Pamoja na kwamba sikuweza kuzungumza naye chochote mpaka naandika mada hii, niligundua mengi sana kutoka kwa dada yule ambaye kwa haraka nilimkadiria kuwa na umri kati ya miaka 22-28.

Ni msichana mrembo kwa kumtazama, lakini uso wake umepoteza matumaini. Anaonekana yupo kwenye uhusiano ambao kwake ni mateso. Nathubutu kusema kwamba, inawezekana kabisa yupo kwenye mapenzi ya utumwa.

rafiki zangu, inapofikia hatua mpenzi wako hakuamini kiasi kwamba ana-divert simu yako kwake, ujue hapo kuna tatizo. Niliagana na dada huyo nikimpa matumaini makubwa kwamba, tatizo lake lingeisha kwa kuwa hakuna kisicho na dawa.

Nilimwambia: “Samahani nashindwa kuongea na wewe sasa hivi kwa kuwa ni nje ya utaratibu, lakini pia nina majukumu mengi yanayonisubiri, ila nakuhakikishia tatizo lako limefika mwisho. Kwa kuwa umeonana na mimi, amini masaibu yako yameshapata dawa!”

Nashukuru aliondoka akitabasamu kidogo. Nilikuwa na matarajio makubwa ya kumpa dawa ya tatizo lake. Wiki ijayo nitawaletea mrejesho. Rafiki zangu, niliona hili liwe kama utangulizi wa somo letu.

HISIA NI NINI HASA?
Katika tafsiri ya kawaida hisia ni neno linalotokana na hisi, fikiri, buni. Kwenye uwanja wa mapenzi linanyambulishwa tofauti kabisa. Huku linajulikana kama mshawasha, mhemko, miliki n.k.

Kwa kifupi, hakuna tafsiri ya moja kwa moja ya neno hilo, lakini limebeba ile hali ya mwenzi kuwa na hamu, mapenzi, uhitaji zaidi kwa mwenzake. Ndiyo maana mtu anaweza akauliza, “Nitawezaje kuteka hisia za mpenzi wangu?”
Bila shaka tupo pamoja.

UNAZITEKAJE?
Hapo ndipo kwenye tatizo kwa watu wengi walio kwenye uhusiano. Wapo wasioweza kabisa kuteka hisia za wapenzi wao. Hawajui mbinu za kufanya hivyo. Rafiki zangu, suala la kumfanya mpenzi wako akupende, awe na hamu na wewe, akufikirie, asiwaze kukusaliti lipo mikononi mwako.
Ni kazi yako. Hapo unaanza na kujua ni mambo gani ambayo hayapendi na yapi anayapenda. Kujua jambo hilo, unakuwa unaelekea kwenye kuelewa namna ya kumaliza kabisa tatizo hilo.
Kuna ambao wapo kwenye uhusiano, halafu wanashangaa ghafla wapenzi wao wamebadilika.

Wanakuwa wakali bila sababu, wakorofi, hawana hamu ya kukutana nao faragha na mengine. Umewahi kujiuliza kwa nini? Jibu ni rahisi sana, AMEPOTEZA HISIA KWAKO!
Kama ndivyo, kazi ipo mikononi mwako ya kurejesha hisia hizo kama zamani. Yapo mambo mengi ambayo natakiwa kuzungumza na wewe kuhusu namna ya kurejesha hisia za mwenzi wako kwako. Ni rahisi sana, wiki ijayo nitakuletea.
Kitu kikubwa rafiki yangu, ninachotaka kukuacha nacho ni kwamba, matatizo mengi kwenye uhusiano husababishwa na kupoteza hisia. Mchunguze mpenzi wako, siku hizi anakukaripia? Anakusimanga? Hakusikilizi?

Anakudharau? Hapendi kukushirikisha kwenye mambo yake? Kama una matatizo haya ujue chanzo chake ni kupoteza hisia. Kazi yangu mimi ni kurejesha amani katika uhusiano wako, Naweka nukta. 
Read more >>

WANAUME KUOA WAKE WANNE NA WANAWAKE KUOLEWA NA MUME MMOJA, JE INARUHUSIWA? SHEKH ANAJIBU

SWALI:
Assalam alaikum, mimi nawa andikia nikiwa mgeni katika dini hiyi ya ALLAH ninayo mswali ambayo ningelipenda kujua majibu yake kwani yatachangia kuniweka sawa na kuifuata vyema dini ya ALLAH.
NATAKA KUJUA KWA NINI DINI YA ISLAM INARUHUSU MWANA UME KUOWA MKE ZAIDI YA MMOJA (NA KUSUDIA KUOWA WAKE WENGI) NA KWA NINI DINI HAIMRUHUSU MWANA MKEE WA KI ISLAM KUOLEWA NA MWANA UME ZAIDI YA MMOJA?



JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani ndugu yetu katika Iymaan kwa suala lako nyeti kuhusu mas-ala muhimu katika Dini yetu tukufu ya Uislamu. ni jambo linaloeleweka kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha ya mwanaadamu kwa ujumla na Waislamu hasa. Japokuwa mfumo huu ambao unamtoa mtu matatani unakimbiwa na wengi. Hakuna lolote isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wametuelezea. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema:
Hatukuacha Kitabuni mwetu kitu chochote” (6: 38).

Hakika muulizaji, wewe ulikuwa Muislamu lakini mazingira yamekufanya wewe ulelekee katika dini nyengine isiyo ya kimaumbile. Hilo ni kwa mujibu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Kila kinachozaliwa kinazaliwa katika Fitwrah (maumbile ya asli ya Uislamu ‘Tawhiyd’) ni wazazi wake ndio wanamfanya awe Myahudi au Mkristo au Majusi” (Al-Bukhaariy).

Ukweli ni kuwa si kila kitu kimeelezwa hekima yake lakini Wanachuoni wanajitahidi kuangalia hekima ya mambo kadhaa ambayo yamo katika Qur-aan Tukufu au Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo, Imani ya Muislamu ni kuwa hata asipopata hekima ya amri au katazo fulani basi yeye huwa ni mwenye kusema:
Tumesikia na tumetii” (2: 285).
Waislamu huwa kabisa hawafuati ile sifa ya Mayahudi ya kusema: “Tunasikia na tunakataa” (2: 93).

Kwa minajili hiyo, Muislamu huwa hapati shida kutii kwani anafahamu kuwa Yule Aliyemuumba Ndiye Anayejua lililo zuri kwake na lenye kumfaa na lililo baya kwake na lenye kumdhuru. Hii ni kanuni muhimu sana kwa kila mmoja kati yetu, Waislamu kuifahamu. Ni ajabu kuwa Mjapani anatengeneza gari akawa ni mwenye kufuatwa kikamilifu na aliyenunua gari. Mwenye gari huyo huwa hata mara moja haendi kinyume na maagizo yaliyotolewa na mtengenezaji huyo, kwani anajua kwa yakini kuwa akienda kinyume kwa mfano badala ya kutia petroli katika injini, yeye akatia maji! Hivyo gari halitaweza kufanya kazi. Vipi maagizo ya Allaah Aliyetukuka tuwe ni wenye kuyapuuza? Jambo haliingii akilini  lakini huwa tunakwenda kinyume katika maamrisho Yake mengi. Tutanabahi na turudi Kwake kabla hatujaondoka katika ulimwengu huu.

Hakika ni kuwa Uislamu umehalalisha uke wenza na ukaharamisha mwanamke kuolewa na wanaume wengi. Shari’ah hii iko wazi katika machimbuko ya shari’ah ya Dini juu ya yote ikiwa ni agizo katika Qur-aan. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema:
Basi oeni mnaowapenda katika wanawake wawili au watatu au wanne. Na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu basi oeni mmoja tu” (4: 3).
Hii ni Aayah ambayo itabaki kutumika mpaka siku ya Qiyaamah.

Katika Sunnah, Mama wa Waumimi, ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) amesema kuwa wakati wa Ujahiliya kulikuwa na ndoa aina nne:

1.     Kama ilivyo wakati huu wetu wa sasa (yaani wakati wao na mpaka sasa kwa mwanamume kwenda kumposa binti kwa wazazi wake).

2.     Mume kwa kutaka apate mtoto mwenye sifa fulani alikuwa akizungumza na mwanamume mwenye sifa hizo ili awe analala na mkewe. Katikahali hiyo alikuwa mume mwenyewe akitoka kwenye hiyo nyumba mpaka mkewe apate mimba. Akishika mimba alikuwa anarudi nyumbani, akitaka alikuwa akimuingilia au akimngojea mpaka azae.

3.     Mwanamke alikuwa anaolewa na wanaume wengi na pindi anapozaa alikuwa akiwaita wanaume wote. Mjuzi wa kulinganisha sura alikuwa akiitwa na atakaye chaguliwa alikuwa akichukua jukumu la kumlea mtoto huyo.

Madanguro ambamo wanawake walikuwa wakiuza miili yao na juu ya nyumba hizo kulikuwa na bendera yenye kuashiria hilo. Mtu yeyote alikuwa na uhuru wa kuingia na kukidhi haja zake.
Alipotumilizwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aina zote za mahusiano baina ya mume na mke zilikatazwa ila ile yiliyotaja katika ipengele cha kwanza (Al-Bukhaariy).

Swali la sisi kujiuliza ni, Je, uke wenza na utovu wa maadili? Kulijibu swali hili ni lazima tuangalie dini nyengine kama Uyahudi na Ukristo unasema nini kuhusu hilo kwani tushaona kuwa Uislamu umeruhusu mbali na kuwa imeweka masharti yake. Kulingana na Uyahudi na ukitazama hasa katika Agano la Kale utakuta kuwa Manabii watukufu wengi walikuwa na zaidi ya mke mmoja kwa mfano Abrahamu alikuwa na watatu, Daudi mia moja, Suleiman mia saba na wengineo. Hawa ni vielelezo kwa wenye kufuata dini hiyo.
Sasa ikiwa hawa wana wake zaidi ya mmoja upo ubaya gani kwa wafuasi kuwa na wake wengi. Ruhusa hii ya kuoa zaidi ya mke mmoja ilipigwa marufuku na kikao cha Marabai cha Worms katika karne ya 11. Katazo hili mwanzo lilitolewa kwa Mayahudi waliokuwa wakiishi Ujerumani na Kaskazini mwa Ufaransa lakini baadae ikawa ni kwa wafuasi wote.

Ukiangalia Ukristo utakuta kuwa, kwa kuwa Agano la Kale ni sehemu ya Biblia ruhusa hiyo itakuwepo bila ya matatizo yoyote. Ni yakini kuwa Yesu wa Biblia alisema hakuna kubatilisha wala kufuta kanuni za Taurati bali kutimiza. Na juu ya yote hayo hakuna hata msitari mmoja katika Agano Jipya unaokataza uke wenza.
Westermarck anasema kuwa hakuna kikao hata kimoja katika karne za awali za Kanisa zilizokataza uke wenza. Wafalme walikuwa wakioa zaidi ya mke mmoja kwa mfano mfalme wa Ireland kati ya karne ya sita alikuwa na malkia 2 pamoja na masuria wawili pia. Madhehebu kadhaa yaliruhusu ndoa hizo bila ya matatizo yoyote. Mwaka wa 1531 mhubiri wa Anabaptists akiwa Munster alitangaza hadharani kuwa yule anayetaka kuwa Mkristo wa kweli ni lazima aoe mke zaidi ya mmoja. Na ulimwengu wote unajua kuwa Mormons wanachukulia uke wenza kama agizo la Mungu.

Hizi ni dalili zifuatazo kuhusiana na hayo: 
 
Biblia inatueleza kuwa Ibrahimu (Abramu) alikuwa na wake watatu kama tunavyoelezwa: "…na Sarai mkewe Abramu…" (Mwanzo 11: 31). Tena: "Kisha, Sarai akampa Abramu Hagari, mtumwa wake wa kike, Mmisri, awe mke wake" (Mwanzo 16: 3).

Na pia: "Abrahamu alioa mke mwingine, jina lake Ketura" (Mwanzo 25: 1). Naye Ya'quub (Yakobo) alikuwa na wake wane kama tunavyoarifiwa na Biblia: "Kisha Yakobo akamwambia Labani, 'Muda wangu umetimia, kwa hiyo nipe mke wangu'. … Lakini jioni, Labani akamchukua Lea, binti yake mkubwa, na kumpeleka kwa Yakobo. Yakobo akalala naye" (Mwanzo 29: 21 – 23).

Pia: "Na Yakobo alipomtimizia Lea siku zake saba, Labani akampa Raheli, binti yake mdogo awe mke wake" (Mwanzo 29: 28). Tena: "Kwa hiyo Raheli akampa Yakobo mtumishi wake, Bilha, awe mkewe, naye akalala naye" (Mwanzo 30: 4).

Pia: "Lea alipoona ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mtumishi wake wa kike, na kumpa Yakobo ili awe mkewe" (Mwanzo 30: 9).

Biblia inatufahamisha tena kuwa kumbe anayefaa kuwa na mke mmoja ni askofu kumaanisha asiyekuwa askofu anaweza kuwa na zaidi ya mmoja. Hebu tusome: "Basi, askofu anapaswa kuwa mtu asiye na lawama; anapaswa awe na mke mmoja tu, awe mwenye kiasi, nidhamu na utaratibu" (1 Timotheo 3: 2). Sijui kwa nini maaskofu wa Kikatoliki hawaruhusiwi kuoa kabisa?

Mwingine anayefaa kuwa na mke mmoja ni mzee wa Kanisa kama tunavyoarifiwa: "Mzee wa Kanisa anapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye na mke mmoja tu, na watoto wake wanapaswa kuwa waumini" (Tito 1: 6).

Ni jambo linalojulikana kuwa hata wale wenye kufuata dini za kitamaduni hasa za Kiafrika wanachukua uke wenza kama jambo la kawaida kabisa. Hivyo, katika sehemu ya Kenya wamisheni walibidi wakubali hao kushika baadhi ya mila zao ili wawavutie kuingia katika Ukristo.

Ifahamike kuwa Aayah tuliyoinukuu juu (4: 3) ina maelezo ambayo yanafaa yaeleweke ili tuweze kuwa na ufahamu mzuri wa suala hili la uke wenza katika Uislamu. Dondoo zifuatazo zitatusaidia:
·         Uke wenza si lazima lakini ni jambo linaloruhusiwa.

·         Ruhusa hiyo si kutekeleza uchu wa mwanamume wa kujitosheleza kimapenzi bali ni kuweza kuwa na huruma kwa wajane, mayatima na wanawake wengineo.

·         Hata katika hali hiyo ya ruhusa uke wenza umewekewa kikwazo kuwa mwanamume hawezi kuoa zaidi ya wanne.

·         Mwanamume ni lazima awafanyie uadilifu wake zake   wote. Huu ni wajibu, na unahusu makazi, chakula, mavazi, na kuwatendea wema. Haya ni majukumu ya mume.

·         Aayah inasema “oa” sio kuteka nyara, kubaka au kutongoza. Kwa hiyo, mwanamke hawezi kushurutishwa au kupatiwa mwanamume ambaye yeye hamtaki.

Swali ambalo linaweza kujitokea ni kuwa, je uke wenza unaweza kuwa ndio suluhisho la matatizo yetu ya kijamii? Kabla ya kujibu swali hili tungependa kusema kuwa Uislamu umekuja na shari’ah yenye kuwafaa watu wote kwa zama zote na katika nchi zote. Kwa ajili hiyo haukuweka shari’ah kwa watu wa mijini na kuwasahau watu wa mashambani, au kwa nchi za baridi na kuwapuuza watu katika nchi za joto, au kwa nyakati fulani ikasahau zama zijazo na vizazi vijavyo. Uislamu unakisia dharura na haja za kila mmoja binafsi na jamii kwa ujumla wake.
Kadhaalika ni vizuri tutazame vipengele vifuatavyo:
1.     Mume anayegundua kuwa mkewe hazai kwa sababu ya utasa, maradhi au kwa sababu nyengine yoyote ile. Je, si bora kwa mwanamke, na ni afadhali kwake yeye mwanamume; kuoa yule atakayemhakikishia raghba hiyo ya kupata mtoto na kubaki na mkewe wa kwanza. Bila kufanya hivyo atabaki bila watoto na kukosa ubaba au amuache mkewe na kuoa mke mwengine. Suluhisho hizo mbili zote hazifai na inabaki kwetu kuukubali uke wenza.

2.     Mwanaume mwenye mke ambaye wakati wote ni mgonjwa au ana wakati mrefu wa hedhi. Mume anaweza kuwa na uchaguzi wa kukandamiza matamanio yake kwa uhai wake wote au amuache mkewe aliye mgonjwa wakati ambao mke anahitaji huruma zaidi au anaweza mume kubaki naye lakini akawa na vimada nje ya ndoa. Ukitazama haya mambo matatu utakuta kuwa la kwanza ni dhidi ya maumbile ya mwanadamu. Uislamu unatambua mahitaji ya kutimiza matamanio ya kimwili. Suluhisho la pili si la huruma hasa kukiwa na mapenzi baina ya wawili wapendanao. Suluhisho la mwisho ni dhidi kabisa na mafundisho ya Uislamu ambayo yanakataza zinaa wazi wazi. Kwa kuwa Uislamu uko dhidi ya utovu wa maadili, unafiki wa kitabia na talaka ila kwa dharura zisizoepukika, mbadala muafaka ni uke wenza.

3.     Kimaumbile wanaume wana shauku kubwa zaidi kuliko wanawake na hivyo kuweza kuwamudu wake wengi.

4.     Kimaumbile upo wakati mrefu ambapo mwanamke hawezi hutekeleza majukumu yake ya kindoa kwa mabadiliko ya kisaikolojia na kifiziolojia na kimwili kama wakati akibeba mimba, hedhi na nifasi. Katika hali ya kwanza wapo wanawake huwa hawataki kuonana hata na mwanaume na katika mbili za mwisho Uislamu umekataza mume kumuingilia mkewe.

5.     Inajulikana kuwa wanawake ni wengi zaidi katika ulimwengu. Na vita ambavyo vinaendelea ulimwengu mzima vinawaacha wajane wengi zaidi na watoto wanaokosa mapenzi ya baba. Je, hawa wanawake wa ziada watimize uchu wao vipi? Ni maslahi ya kijamii kuwa wanawake wawe ni wenye kuolewa na hivyo kupata himaya ya kifamilia. Kawaida hawa wanawake huwa wana hamu ya kuolewa, nao hawana ila njia tatu mbele yao: Kuishi umri wao bila ya kuolewa; au walegeze hatamu wakiishi huku wakitumiwa na wanaume kwa kutimiza matamanio yao; au waolewe na waume wengine wenye uwezo wa kuwatazama. Suluhisho ni kuchukua msimamo wa tatu wa kuoa wake wengi.

6.     Ipo shida kubwa sana Marekani na nchi za Bara Ulaya ambapo kumepigwa marufuku mume kuoa mke mwengine. Kwa sababu ya kanuni hiyo iliyo kinyume na maumbile ya mwanadamu utawakuta wanaume wengi wana vimada nje ya ndoa. Wanazaa nao watoto lakini hawana jukumu lolote la kuwatazama, kwao ni kutimiza haja yao ya kimapenzi tu.

7.     Mitume (‘Alayhimus Salaam) ambao ni kielelezo kwetu walikuwa na wake wengi hata katika Biblia kwa nini hatufuati mienendo yao kwani wao wamekuja na maisha yaliyo bora kabisa.

8.     Wanawake wengi katika jamii tofauti ulimwenguni wanafadhilisha waume wenye wake wengi (tazama Campbell, D., In the Heart of Bantuland, uk. 160).


Mbali na hayo yote tuliyoyasema linajitokeza swali:
Kwa nini mwanamke asiolewe na waume wengi?
Katika hili tunasema yafutayo:

1.     Ni hakika kuwa maumbile ya mwanamke kisaikolojia na fiziolojia ni tofauti na mwanaume. Kisaikolojia ni kuwa mwanamke anatosheka na mume mmoja. Kifiziolojia mwanamke hawezi kujimudu kuwa na wanaume zaidi ya mmoja kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mwili wake.

2.     Katika tamaduni zote, za zamani na sasa, uongozi wa nyumba (familia) ni wa mwanaume. Unaweza kufikiria katika familia ambayo ina kiongozi zaidi ya mmoja, nyumba hiyo itaendeshwa vipi? Ndio wahenga wakawa na msemo: “Fahali wawili hawakai kwenye zizi moja”.

3.     Mwanamke huyu ataweza vipi kuwaridhisha wanaume hao wote katika chakula na mapenzi. Tuseme kuwa utawagawia siku, mmoja wao anakuja na mke huyo yuko katika hedhi naye ana shauku ya juu sana, atafanyaje? Je, mke atachukua amri kutoka kwa nani?

4.     Mke anayeolewa na mume zaidi ya mmoja, anaposhika mimba itakuwaje? Mtoto huyo atakuwa wa nani? 

Hivyo, mke kuolewa na mume zaidi ya mmoja ni jambo ambalo halikubaliki wala haliwezi kutekelezeka na hii yote ndio hikma ya Mola Mtukufu Aliyetuumba na kutufahamu yanayotunufaisha na yanayotudhuru.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger