MTOTO mwenye
umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la tatu katika
shule ya msingi Kibaha amenusurika kubakwa na njemba inayofahamika kama
Shukuru Abdalahman (49) anayeishi naye nyumba moja, asubuhi ya Julai
31, mwaka huu Kibaha Kwamatias.Akisimulia
tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Amina Rashid alisema mtoto wake
aliamka asubuhi na kuitwa na Shukuru chumbani kwake kwa madai ya kutaka
kumtuma dukani, lakini alipoingia chumbani alifunga mlango na baadaye
kumziba mdomo kwa vitambaa kumzuia asipige kelele.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Bi. Amina Rashid.
“Baada
ya kumtafuta kwa muda, nilikwenda chumbani kwa huyo baba, nikamkuta
mwanangu amefungwa vitambaa mdomoni, nilipomuuliza kwa nini hali iko
vile, akawa anababaika, nikamchukua mtoto na kumwambia baba yake,
tukamuuliza kulikoni, akasema alitaka kuingiliwa kwa ahadi kwamba
atapewa chokoleti na hela ya kutumia shuleni.
Baba wa mtoto aliyenusurika kubakwa.
“Tukamfuata
na kumuuliza akakataa, tukaenda kwa mjumbe, alipoitwa baada ya kubanwa
alikiri kutaka kumwingilia mtoto, akaomba yaishe kwa ahadi ya kutoa
faini ya 30,000, lakini akatoa 20,000 kwanza, baba mtu akaenda Polisi
kutoa taarifa,” alisema mama huyo na kudai kufunguliwa kwa faili lenye
namba MKZ/RB/414/2014 KUJARIBU KUBAKA.
Njemba inayofahamika kama Shukuru Abdalahman (49) ikiwa kituo cha Polisi.
Mwandishi
wa habari hizi alishuhudia njemba hiyo ambayo ilikuwa ikirejea nyumbani
usiku kuogopa aibu na kukamatwa, akinaswa na na polisi na kupelekwa
kituo cha Polisi cha Mkuza aliswekwa nyuma ya nondo kusubiri hatua zaidi
za kisheria.
Credit GPL
No comments:
Post a Comment