Si kweli! Mtoto mzuri Bongo Movies, Jennifer Kyaka
‘Odama’ amekanusha vikali madai ya kutembea na pedeshee mmoja anayedaiwa
kuwa ni mmiliki wa baa moja iliyopo maeneo ya River-Side, Ubungo jijini
Dar.
Baada ya kusomewa madai hayo ambayo yamesambaa kwenye mitandao ya
kijamii, Odama alikanusha vilivyo na kusema wanamsingizia tu.“Hee! Mbona
huyo mtu wala simjui, ndiyo kwanza nazisikia hizo habari wakizikuza
kwenye mitandao,” alisema Odama.
Kwenye madai hayo mtandaoni, Odama anadaiwa kuwa hajatulia na ndiyo
sababu ya kutomwanika baba mtoto wake, jambo ambalo mwenyewe amesema si
kweli bali ni utaratibu wa maisha yake aliojiwekea wa kutomuanika mzazi
mwenzake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment