Akilia baada ya kula kichapo.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Agosti 5, mwaka huu katika baa hiyo mpya iliyopo Sinza ya Afrikasana jijini Dar es Salaam. Ilidaiwa
kuwa, warembo hao waliambiwa mapema kuwa ifikapo alfajiri wasionekane
kwenye eneo la baa hiyo lakini wao waliendelea kupombeka mpaka jua
linachomoza ndipo mabaunsa walipowaondolea uvivu kwa kuwapa kipigo.
Mmoja
wa warembo hao ambaye alionekana kukerwa na kitendo cha mwenzake
kupigwa hadi kutokwa damu aliwalalamikia mabaunsa hao kuwa
hawajawatendea haki kwa kuwafukuza kama mbwa na kipigo juu.Akitokwa na damu juu ya jicho la upande wa kulia baada ya kuchezea kichapo kikali.
Kwa
vile hawakuwa na nguvu za kupigana na mabaunsa hao, warembo hao
waliporomosha matusi ya nguoni na kujaza watu waliokuwa wakienda
makazini asubuhi hiyo. Hata
hivyo, baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio, hasa wanaume
walisikika wakipongeza kitendo cha warembo hao kuchezea kichapo wakisema
wamezoea kukesha eneo hilo mpaka kunakucha.Mashuhuda hao walikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa wanahisi warembo hao wanajihusisha na biashara ya ‘udada poa’.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia mkasa huo.
“He!
Wamezoea hao! Ni sawa mabaunsa wawaoneshe kazi. Watu gani wapo baa hadi
muda huu wa asubuhi kweupe?” alisikika mmoja wa mashuhuda hao. Kilio
kikubwa cha mabaunsa hao kilikuwa ni kutaka kusimamia heshima ya baa
hiyo kwa vile wateja wanaofika hapo ni wenye heshima zao. “Msije
tena hapa, sisi hatuwataki muda wa asubuhi wala mchana, tulishasema
sana lakini hamsikii, mnataka kutukimbizia wateja siyo?” alisema mmoja
wa mabaunsa hao.
Wakishauliana jinsi ya kumsaidia mwenzao.
Mwisho
wa sakata hilo, warembo wengine walitafuta usafiri wa Bajaj na kumbeba
mwenzao aliyepigwa sana mpaka kutoka manundu na kuondoka huku
wakiendelea kuvurumisha mitusi kwa mabaunsa hao na kusema wanakwenda
kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar. Mapaparazi wetu waliifuatilia Bajaj hiyo na kuiona inaelekea maeneo ya Sinza ya Mapambano badala ya polisi. Baadhi
ya wateja wa baa hiyo walisema wakati wa Mfungo wa Ramadhan, warembo
walipungua eneo la baa hiyo lakini sasa wamerudi tena ambapo sasa
wanapatikana kuanzia saa moja jioni hadi jua linapochomoza kesho yake
No comments:
Post a Comment