CONFESSION! Kwa mara ya kwanza staa wa Bongo Fleva,
Emanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kuuelezea upande wa pili
wa maisha yake kuwa kabla hajawa mwanamuziki alikuwa mwizi balaa!
Akizungumza na paparazi wetu ana kwa ana jijini Dar es Salaam juzi, staa
huyo alikiri kupitia katika majanga kibao maishani mwake likiwemo la
kulala katika vituo mbalimbali vya polisi vya jijini Dar kufuatia
kufanya matukio ya uhalifu.
“Kwanza kabisa nilikuwa nalala Feri na watoto machokoraa. Nilikuwa
naona ndiyo maisha japokuwa nilijua kuna maisha mengine mazuri zaidi
lakini ningeyapate?
“Dah! Yaani kusema kweli nilipita kwenye majanga makubwa sana jamani!
Anyway, kimsingi ukweli wa maisha yangu siwezi kuuficha maana nitakuwa
najiongopea bure kwani ni kweli niliishi katika maisha ya matukio sana,”
alisema Nay.
Akizidi kutiririka mbele ya kinasa sauti cha Amani, Nay ambaye kwa
sasa anatamba na wimbo wa Mr Nay aliweka bayana kwamba kwa nyakati
tofauti aliwahi kuiba vitu mbalimbali (hakupenda kuvitaja) kwa watu wa
karibu yake akiwemo Prodyuza Paul Mathysse ‘P Funk’ na kwenye studio
moja iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.
“Enzi zangu nilikuwa balaa, Majani mwenyewe (P. Funk) nilishawahi
kumliza, nakumbuka pia kuna jamaa zangu walikuwa na studio ya muziki
pale Mwenge nao niliwapiga.
“Tena hawa jamaa wa studio nakumbuka
walikuja kinitaiti nikiwa kwenye msiba, wakanitia pingu na kunipeleka
kituo cha polisi lakini bahati nzuri marehemu John Mjema, alikuwa
mshikaji wangu sana, akaja kunitoa,” alisema Nay.
John Mjema ‘Bomba la Mvua’ alikuwa mwanamuziki wa Kizazi Kipya,
alifariki dunia Februari 10, 2008 kwa kujichoma kisu cha shingo nyumbani
kwake Mtoni Kijichi jijini Dar.
Nay akaongeza: “Kulala polisi nadhani ni kama mara saba hivi na mara
zote aliyekuwa akinitoa ni John Mjema. Yeye wakati ule alikuwa akifanya
kazi kule maeneo ya Feri.
Pamoja na matukio hayo ambayo Nay ameyafanya, alisema alishatubu na
kumwomba Mungu amsamehe kwani anaamini ujana ndiyo ulikuwa ukimsumbua.
“Yaliyopita si ndwele, kwa sasa naganga yajayo maana muziki unanilipa
na naendelea na harakati zangu kama kawaida, nilishasahau hayo matukio
ya ajabuajabu,” alimaliza Nay.
Miongoni mwa mafanikio makubwa aliyoyapata msanii huyo kupitia muziki
wa Bongo Fleva ni kujenga nyumba Kimara-Rombo jijini Dar na gari la
kutembelea aina ya Nissan Murano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment